Tafuta

Mazishi ya Patriaki wa Kikatoliki wa  Georgia Ilia II huko Tbilisi. Mazishi ya Patriaki wa Kikatoliki wa Georgia Ilia II huko Tbilisi.  (AFP or licensors)

Papa atuma salamu za Rambirambi huko Georgia:Patriaki Ilia II alikuwa sauti ya upatanisho!

Katika ujumbe uliosomwa wakati wa misa ya mazishi ya Patriaki wa kikatoliki wa Georgia,Papa Leo XIV,anamfafanua kama sauti ya upatanisho na mjenzi asiyechoka wa umoja.Alisindikiza nchi ya Giorgia katika kipindi kigumu na pia kukumbuka shauku yake kwa muziki ambao ni msukumo wa kutafuta uzuri'unaounganisha Makanisa.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV  alituma salamu za rambimbi kufuatia na kifo cha Patriaki Mkatoliki wa Nchi ya Giorgia yote, Ilia II, na Askofu Mkuu wa Mtskheta-Tbilisi, Abkhazia na  Bichvinta kilichotokea  tarehe 17 Machi 2026. Katika salamu zilizoelekezwa kwa Mkuu wa Senaki na Chkhorotsku na Sinodi  yote ya Kanisa la Kiothodox la Georgia, awali ya yote anamfafanua marehemu kama Sauti ya ushirika, inayoweza kusikika kwa undani zaidi kupitia nguvu ya muziki: kichocheo cha kutafuta umoja huo unaozidi kuwa muhimu katika nyakati ngumu na mabadiliko ya kihistoria, ambayo Georgia haijabaki bila kujali. Ujumbe wake uliosomwa na Kardinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo, wakati wa ibada ya mazishi na kuchapishwa Dominiak tarehe 22 Machi 2026.

Papa anaungana nao katika sala 

Ni kwa huzuni kubwa niliyopata kujua kuhusu kifo cha Patriaki  Ilia II, Mchungaji Mkuu wa Georgia Yote. Katika kutuma salamu zangu za rambirambi ninamhakikishia Mkuu wa  Sinodi Takatifu, na Kanisa lote la Kiorthodox la Georgia mshikamano wangu wa kidugu katika huzuni yenu.” Papa aidha aliandika kuwa “katika wakati huu mgumu kwa watu wenu, ninajiunga nanyi katika sala na katika kumbukumbu yenu ya shukrani kwa Mchungaji na Baba aliyewaongoza kwa wema, hekima na nguvu ya kiinjili kwa miaka mingi. Katika maisha yake marefu, Patriaki Ilia II alikuwa shuhuda aliyejitolea wa imani katika Kristo Mfufuka. Huduma yake iliwasindikiza watu wa Georgia kupitia nyakati ngumu na mabadiliko makubwa ya kihistoria, kwa upendo akihifadhi mila na tamaduni na kufungua mioyo na jamii kwa matumaini.”

Sauti ya upatanisho na mjenzi asiyechoka wa umoja

Baba Mtakatifu pia alipenda kukumbusha kwa “shauku yake kubwa ya muziki, ambayo ni kichocheo cha utafutaji wa uzuri wa Mungu na inaweza kuunganisha watu, na kuyaleta Makanisa pamoja zaidi ya tofauti za kiutamaduni na kitaalimungu. Kwa wengi, alikuwa baba wa kiroho, sauti ya upatanisho na mjenzi asiyechoka wa umoja. Alikutana na watangulizi wangu wawili  Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili na Papa Francisko ambapo kila wakati katika roho ya ukarimu na udugu."  Papa Leo XIV aliandika kuwa, wanapomkabidhi Bwana mtumishi huyu mwaminifu, maneno ya Mtume Paulo yanasikika kwa nguvu, yakitukumbusha kwamba ufufuko wa Yesu ndiyo msingi wa imani yetu na chanzo cha tumaini letu. Kwa maana ikiwa Kristo hajafufuka, basi imani yetu ni bure (taz. 1 Kor 15:14).” Kwa hivyo, “tukikabiliwa na kifo cha Mchungaji, mioyo yetu haikati tamaa. Badala yake, imefunguliwa kwa uhakika kwamba maisha hayaondolewi bali hubadilishwa.” 

Mioyo yetu haikati tamaa

Papa Leo XIV  alibainisha katika ujumbe huo kuwa,  kwa hisia hizo alimwelekea ukaribu wake wa kidugu mkuu huyo wa Kiordhox, anapobeba uzito wa huduma ya Locum Tenens. Na anaomba kwamba Bwana ampe mwanga, utambuzi na ushujaa, ili uweze kusindikiza  Kanisa la Kiorthodox la Georgia kwa upendo ule ule wa kichungaji uliomhuisha marehemu Patriaki. Na Pia Papa anamwomba Mama Mtakatifu wa Mungu amlinde Mkuu wa Sinodi Takatifu, na watu wote wa Georgia kwa vazi lake la faraja na upendo.

PATRIAKI WA GIORGIA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

 

 

22 Machi 2026, 15:19