Tafuta

Kardinali Konrad Krajewski Kardinali Konrad Krajewski 

Papa amteua Kard.Krajewski,kuwa Askofu Mkuu wa Łódź,Poland

Papa Leo XIV amemteua aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la huduma ya upendo Kardinali Krajewski kuwa Askofu Mkuu wa Łódź nchini Poland."Miaka ishirini na minane ya huduma na Mapapa wanne,"Kardinali alisimulia akizungumza na Vatican News.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV, tarehe 12 Machi 2026 alimteua Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Łódź nchini Poland Kardinali,  Konrad Krajewski, aliyekuwa Msimamizi wa Sadaka ya Papa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo.

Wasifu wake

Alizaliwa huko Łódź nchini Poland kunako tarehe 25 Novembre 1963. Baada ya kujiunga na Seminari ya Jimbo Kuu la Łódź mnamo 1982, alipata shahada ya Taalimungu kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Yohane  Paulo II huko Lublin, Ireland. Alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 11 Juni 1988. Ameshika nafasi mbalimbali na  kukamilisha masomo zaidi: Makamu wa Parokia huko Rusiec na Łódź; Mafunzo na Leseni ya Liturujia kutoka Taasisi ya Liturujia ya Kipapa ya Mtakatifu Anselm Jijini Roma; Mshereheshaji wa Jimbo Kuu la  Łódź; Profesa katika Seminari ya Jimbo na Seminari ya Wafransiskani  na Wasalesiani ya Jimbo Kuu la  Łódź; Profesa katika Chuo Kikuu cha Warsaw; Mkuu wa Seminari ya Jimbo Kuu la Warsaw;

Aidha ni Daktari wa Taalimungu, na mwenye utaalamu wa Liturujia, kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas Aquinas huko Roma; Msaidizi wa Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa, Padre Mhudumu wa Kliniki ya Mifupa na Maumivu ya Kiwewe ya Chuo Kikuu cha 'La Sapienza' cha Roma. Mwaka 2013, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Sadaka ya Baba Mtakatifu na shemasi wa Kanisa la Mtakatifu Maria Asiye na dhambi kwa kupokea wakfu wa kiaskofu mnamo tarehe 17 Septemba iliyofuata. Na kutoka kwa Papa Francisko alimuunda kuwa Kardinali kunako tarehe 28 Juni 2028 akiwa na  Kanisa la Maria Asiye na dhambi  la Esquilino. Tangu 2022, Kardinali Krajewski,  amekuwa Mkuu wa Baraza la Kipapa kwa Huduma ya Upendo.

Katika mji wake wa asili

Kardinali Krajewski, mwenye umri wa miaka 62, kwa hiyo anarudi katika mji wake wa asili. Alizungumza na Vatican, akijibu simu kwa sauti safi, mtulivu, mwenye furaha, na tayari kuondoka, au tuseme, kurudi nyumbani. Kardinali Konrad Krajewski aliyeteuliwa na Papa Leo XIV kuwa Askofu Mkuu wa Jiji Kuu la  Łódź, mji wake wa asili. "Miaka ishirini na minane ya huduma na Mapapa wanne," Kardinali alisimulia: "Nilikuwa kando ya Papa Yohane Paul II katika miaka saba ya mwisho ya maisha yake alipokuwa mgonjwa. Kisha ukawa upapa wa Benedikto XVI, ule wa Papa Francisko, na  kwa miezi 10 ya Papa Leo XIV. Nilipata mambo tofauti kwa sababu kila Papa alilipatia Kanisa kitu kipya, kila moja akiwa na msisitizo tofauti." Kwa kifupi, anarudia utume wake na upendo wake kwa Kanisa la ulimwengu wote, ambalo alilitumikia "katika miaka yake bora." Ukuaji wa kibinadamu na kiroho uliotajirishwa na ukaribu wake na maskini.

Il Papa insieme al cardinale Krajewski all'inaugurazione dell'ambulatorio San Martino

Papa Leo XIV akiwana Kardinali  Krajewski wakati wa uzinduzu wa Kliniki ya Mtakatifu Martino(@VATICAN MEDIA)

Katika ndege ya kurudi kutoka WYD

"Nilipomfuata Papa Francisko kwenda Rio de Janeiro kwa Siku ya Vijana Duniani, nilitumia masaa mawili kati ya 13 nikimsikiliza. Alinielezea kile nilichopaswa kufanya kama Msimamizi wa Sadaka ya Papa akiniomba nilale na maskini, niondoke Vatican, niwe na akaunti tupu kila wakati mwisho wa siku kwa sababu kila kitu kilitengwa kwa ajili ya kazi za upendo. Lakini kuna kitu ambacho kimebaki nami kila wakati, kitu ambacho Papa Francisko aliniambia: 'Ikiwa hujui la kufanya, muulize Bwana kila wakati na uulize angefanya nini badala yako.'" "Pia nimefanya makosa mengi," Kardinali alikiri, "lakini nilifanya hivyo kwa nia njema, na Papa amekuwa akinielewa na kunisamehe kila wakati."

Kukumbuka Poland

Kuhusu jukumu jipya linalomsubiri, alisema kwamba Papa Leo  XIV alikuwa amemuuliza kwa uangalifu ikiwa alitaka kwenda, na ikiwa alitaka kupeleka uzoefu wote alioupata katika Kanisa la Ulimwengu wote kwa Kanisa lake mahalia. "Nilikubali kwa furaha kwa sababu mema ya Kanisa yanatokana na ukaribu na waamini. Jimbo langu ni kubwa, ikiwa na wakazi milioni mbili na nusu, na niko tayari kutumikia." "Sijawahi kuondoka Poland," alikiri, "Nimebaki miongoni mwa watu siku zote, na hata nilikuwa natamani sana kurudi nyumbani."

Il cardinale rende omaggio alle vittime ucraine a Bucha

Kardinali alitoa heshima kwa waathirika wa Ukraine huko Bucha

Pamoja na Ukraine

Akikumbuka uzoefu wake, alitaja misheni zake kumi za kwanda Ukraine kusaidia, kwa niaba ya Papa, idadi ya watu walioharibiwa na vita. Kwa tabasamu, pia aliitaja milio ya risasi iliyomfikia kwa bahati nzuri mwaka 2022,  bila kupata majeraha yoyote. Alikumbuka  akipeleka binafsi magari ya wagonjwa au magari manane yaliyoandaliwa kwa ajili ya kukabiliana na dharura nchini Ukraine. Alikumbuka nyuso za mateso za jamaa za wale wanaoishi Gaza ambao alikutana nao wakati wa safari yake kwenda Nchi Takatifu wakati wa Noeli  2023.

I cardinali Pizzaballa e Krajewski a Gerusalemme

Kardinali  Pizzaballa na Kardinali  Krajewski huko Yerusalemu 

Chumba cha Dharura cha upendo

Kwa maskini, katika kipindi cha miaka 13 iliyopita, "chumba cha dharura cha upendo kama Kardinali Krajewski alivyokuwa  akikiita  Ofisi ya Huduma ya Upendo ya Papa, kimeibua mashirika mengi yanayotoa msaada na usaidizi kwa walio katika mazingira magumu zaidi, kwa maelekezo ya Papa Francisko. Mnamo Februari 2015, bafu zilifunguliwa chini ya  nguzo za Mtakatifu Petro huku watu wengi wa kujitolea kuendelea na huduma hii, iliyoundwa ili kuwapa heshima, kuwakomboa kutokana na unyanyapaa na harufu mbaya ya barabarani. Kila siku, karibu watu 150 hutumia bafu hizo. Hapa wanaweza kupokea kila kitu wanachohitaji kwa ajili ya kufua, ikiwa ni pamoja na nguo za ndani safi, chai ya moto, na sandwichi asubuhi. Kinyozi na kliniki ya "Mama wa Huruma" pia zimefunguliwa mlango ulio karibu, hivi karibuni zikijumuishwa na kliniki ya "Mtakatifu  Martino", ambayo Papa Leo XIV  alitembelea tarehe 14 Novemba  2025

Vituo viwili, vyenye wafanyakazi 120 wa madaktari, wauguzi, mafundi wa matibabu, wafamasia, na watu wa kujitolea, hutoa huduma maalum za kimatibabu, huduma ya meno, na vipimo vya maabara, pamoja na upatikanaji wa dawa na matibabu muhimu bila malipo. Msaada kwa maskini hutolewa katika mabweni kadhaa yaliyofunguliwa karibu na  Uwanja wa Mtakatifu Petro. La kwanza liko kwenye Njia ya Via Penitenzieri, iitwayo "Dono di Misericordia," jengo lililotolewa na Wajesuit na kufunguliwa mnamo Oktoba 2015. Linahifadhi wanaume wapatao 30 na linaendeshwa na Masista wa Mama Teresa. Linakamilisha"Dono di Maria," mabweni ya wanawake yenye vitanda vipatavyo 50. Mwaka wa 2019, Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo  iliteua Jumuiya ya  Mtakatifu Egidio kusimamia Jengo a Migliori, ambalo ni la kihistoria la karne ya 19 lililobadilishwa kuwa makazi ya wasio na makazi, wazee, na walemavu. Pamoja na haya yote, kuna malipo ya bili na usaidizi kwa familia zenye uhitaji, na jitihada ndefu, ya kimya, na ya kimaombi.

Il cardinale insieme ai ragazzi del Circo ront Roller a cui ha impartito la Cresima e la Prima Comunione

Kardinali akiwa katika pamoja na wavulana wa Sarakasi ya Rony Roller  ambao aliwapatia Kumnyo ya Kwanza na  Kipaimara

Maskini na Injili

Ujumbe wa mwisho wa Kardinali Konrad Krajewski ni kwa ajili ya wapendwa wa Mungu, maskini ambao wamekuwa wakimwita "Don Corrado" na ambao wamesafiri naye, kama vile Torino kwa ajili ya maonyesho ya Sanda Takatifu ya Torin omwaka 2015, au kula pizza baada ya siku moja ufukweni, au kuzungumza, lakini kila mara nikiwa na haraka kwa sababu kulikuwa na jambo la dharura la kushughulikia. "Lazima niwashukuru wote," anasema kwa hisia kidogo, "walinifundisha kusoma Injili, kuishi kwa njia mpya."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here

12 Machi 2026, 15:10