Tafuta

Papa Leo XIV:Mungu hawezi kutumiwa katika mzunguko wa giza!

Upendo una uso na miguu ambayo inaongoza katika Kanisa,mikono inayotoa kwa maskini na macho yanayotambua mwenye kuhitaji.”Ni katika mahubiri ya Papa Leo XIV katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu huko Ponte Mammolo,Roma,Alasiri Dominika Machi 15."Kwa sasa katika ulimwengu kuna kaka na dada zetu wanateseka kwa sababu ya vurugu za migogoro,zinazosababishwa na suluhishi za kipuuzi za matatizo na tofauti kwa vita badala ya mazungumzo ya amani."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV Dominika, alasiri tarehe 15 Machi 2026  alitembelea Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu huko Ponte Mammolo. Mara baada ya kufika alikutana na kundi la watoto na vijana, baadaye akafanya mkutano na wazee na wagonjwa, ilifuatia ibada ya Misa Takatifu  na kuhitimisha na mkutano na Baraza la Kichungaji, mara baada ya misa Takatifu. Papa Leo XIV wakati wa mahubiri yake alianza kusema:  maaadhimisha ya Ekaristi, leo hii kuliko hapo awali yanaashirika furaha. Kiukweli, uzuri wa mkutano wetu huu unajikita katika muktadha wa Dominika iitwayo Laetare, yaani Furahi  kutoka maneno ya Isaya: “Furahi Yerusalem”, katika wimbo wa mwanzo (Si 66,10. Hii inatufanya kutafakari.

PAPA KATIKA PAROKIA YA MOYO MTAKATIFU ROMA
PAPA KATIKA PAROKIA YA MOYO MTAKATIFU ROMA   (@Vatican Media)

Kaka na dada wanaoteseka kwa vita:wengine wanatumua jina la Mungu kuhalalisha vita

Papa Leo XIV alitazama Ulimwengu wa sasa uliogubikwa na migogoro na kusema: "Kwa sasa katika ulimwengu ambao kaka na dada zetu wanateseka kwa sababu ya vurugu za migogoro, zinazosababishwa majidai ya kipuuzi ya kusuluhisha matatizo na tofauti kwa vita, wakati inahitajika kuzungumza bila kuchoka juu ya amani. Mwingine kisha anajidai hata kuhusika kwa kutumia jina la Mungu katika chaguzi hizi za kifo, lakini Mungu hawezi kutumiwa katika mzunguko wa giza. Yeye zaidi anakuja daima, kutoa mwanga, matumaini na amani kwa ubinadamu, na ni amani ambayo lazima kuitafuta kwa wale ambao wanaiomba.

Parokia ya Ponte Mammolo
Parokia ya Ponte Mammolo   (@Vatican Media)

Kristo anakuja kuleta mwanga

Ujumbe wa Dominika hii, Papa Leo XIV alisisitiza, mbali na kila giza nene ambalo mtu anaweza kuangukia kwa sababu ya dhambi zake, Kristo anakuja kuleta mwanga wa nguvu zaidi, wenye uwezo wa kuondoa kutoka kwenye upofu wa mabaya ili kuanza maisha mapya. Mkutano kati ya Yesu na kipofu tangu kuzaliwa (Yh 9,1-41) kwa hakika, unaweza kufananishwa na suala la kuzaa, shukrani kwa hilo, kama mtoto ambaye anakuja katika mwanga, anagundua dunia mpya ya  kuiishi mwenyewe, kwa ajili ya wengine na maisha kwa macho ya Mungu (1Sam 16,9).

Misa ya Papa
Misa ya Papa   (@Vatican Media)

Nini maana ya mtazamo huo wa kutazama kwa macho ya Mungu?

Baba Mtakatifu Leo XIV kwa njia hiyo, aliomba kujiuliza maswali: Je mtazamo huo unahusu nini? Unatuonesha nini? Ina maana gani ya kusema “ kutazama kwa macho ya Mungu? Kwa kujibu, Papa alisema, “kwa mujibu wa simulizi ya Mwinjili  Yohane, awali ya yote maana yake ni kushinda hukumu za yule ambaye mbele ya mtu anayeteseka, aona picha ya kudharau, au tatizo la kukwepa, kwa kujifunga katika mnara ulifungwa sana na ubinafsi.

Mkutano wa Yesu unakuwa fursa ya kuonesha matendo ya Mungu

Mara nyingi inasikika wakisema sentesi kama vile: hadi wakati mambo yalikuwa yakienda vizuri, walikuwa marafiki wengi; katika wakati wa majaribu, wengi walitoweka!” Yesu hafanyi hivyo; anatazama kipofu kwa upendo na si kama mtu wa chini au uwepo  wake ni usumbufu, bali ni kama mtu mpendwa na mwenye kuhitaji msaada. Na kwa njia hiyo katika mkutano wao, ukageuka kuwa fursa ili wote waweze kuonesha matendo  ya Mungu. Katika “Ishara,” na katika “muujiza”, Yesu anaonesha uwezo wake wa kimungu na mtu, karibu kupitia ishara za uumbaji kama: tope, mate, na anarudia kuonesha kwa ukamilifu uzuri wake na hadhi yake ya uumbaji ulitengenezwa kwa sura na mfano wa Mungu. Kwa hiyo anaona tena na anakuwa shuhuda wa mwanga.

Hakika Papa Leo alisema hiyo ni kazi ngumu inayodai: inabidi azoee vitu ambavyo hakuwa anajua, ajifunze kutenganisha kati ya rangi na umbo, kuweza kuunda mahusiano yake na siyo rahisi. Badala yake vizingiti ambavyo vinamzunguka vinakua, vinamsababishia na hata wazazi wake hawakuweza kumtetea (Yh 9, 18-23). Hata cha kushangaza zaidi, kwa yule aliye karibu yake anataka kufuta kile ambacho kilitokea. Na si hilo tu, katika mahojiano ambayo alipewa kipofu  na ambaye sasa anaona, anayemweka kwenye mchakato  hasa ni Yesu, aliyeshtakia kwa sababu ya kukiuka sheria kwa  kumponya siku ya Sabato.

Misa ya Papa
Misa ya Papa   (@Vatican Media)

Hakuna Sabato inayoweza kuzuia tendo la Upendo wa Mungu

Hapa Papa alisema,  unajionesha, upofu mwingine, tofauti na bado mbaya zaidi: ule wa kutoona mbele yako, uso wa Mungu, kwa njia hiyo wanabadilishana uwezekano wa mkutano wa ukombozi kwa usalama tasa ambao unawapatia wao utekelezaji wa kisheria wa nidhamu rasmi. Mbele ya udhaifu  huo,  Yesu hasimami, kwa kuonesha kuwa hakuna “Sabato ambayo inaweza kuzuia tendo la Upendo. Zaidi ya hayo maana ya mapumziko ya Sabato, kwa watu wa Israeli, na kwetu sisi ni Dominika, ni siku ya Bwana, ambayo ni kuadhimisha maisha kama zawadi, ambayo hakuna mtu anayeweza kudharau kilio cha msaada wa kaka na dada anayeteseka.

Nyakati hizo  za shida na vizingiti. Lakini wao hawakukata tamaa

Labda, wakati mwingine katika maana hiyo, vipofu tunaweza kuwa hata sisi, wakati hatuwezi kuwatambua wengine na wenye matatizo. Kinyume chake Yesu anatuomba tuishi kwa namna tofauti, kama yeye alivyokuwa ametambua Jumuiya za kwanza za Kikristo, ambamo, kaka na dada, walikuwa wakisali, wakishirikshana yote kwa furaha na urahisi wa moyo(Mdo 2,42-47). Hapakukosekana,  hata katika nyakati hizo za shida na vizingiti. Lakini wao hawakukata tamaa: Wakiwa na  nguvu ya ubatizo, waliijibidisha wakati huo huo,  kuishi kama viumbe vipya, kwa kuishi katika umoja na amani kwa wote na kupata katika jumuiya familia moja ambayo  iliwasindikiza na kuwasaidia.

Misa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu
Misa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV aliendelea kudadavu kuwa haya ni matunda ambayo “sisi tunaalikwa kupeleka kwa wana wa nuru(1Ts 5,4-5);”na katika Parokia yao karibu kwa miaka 90 wanaishi kwa uaminifu wa utume kwa namna ya  pekee ya utunzaji wa hali halisi ya maskini waliotengwa na dharura, kwa umakini wa uwepo katika eneo, Nyumba ya wafungwa ya Rebibbia, na kwa ishara nyingine za kuhushwa  na mshikamano. Baba Mtakatifu Leo, aliwaeleza anavyojua kuwa wanasaidia kaka na dada wengi wanaotoka nchi nyingine, ambao wamejumuishwa humo: wakijifunza lugha, kutafuta nyumba yenye hadhi, na kutafuta ajira yenye heshima na usalama.

Hapakosekani matatizo kwa bahati mbaya ambayo mara nyingi yanaletwa na  yule hasi na dhamiri safi, kwa kutumia nafasi za umaskini na hali ya wadhaifu, kufanya mambo yake binafsi. Papa alieleza anavyotambua  wale ambao wanaishi wakijibidisha kukabiliana na changamoto hizo, kwa njia ya huduma  ya Caritas, Nyumba za familia, kwa kupokea wanawake na mama wenye matatizo na shughuli nyingine zinazoanzishwa. Kwa njia hiyo kama alivyo taarifiwa, Papa Leo XIV alisema, kuna ukaribu wa kila aina ambao wanajikita nao kwa ajili ya elimu kwa vijana na barubaru, katika vituo vyao na mapendekezo mengine  ya mafunzo.

Misa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu huko Pomte Mammolo
Misa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu huko Pomte Mammolo   (@Vatican Media)

Upendo una miguu ambayo inaongoza katika Kanisa

Mtakatifu Agostino, akizungumza kuhusu uso wa Mungu, ambao sisi sote tunaitwa kuwa kioo katika ulimwenngu alikuwa anasema kwa wakristo wa wakati wake: “Upendo una uso gani? Ni umbo gani, status yake, miguu gani, na mikono gani?(…) una miguu ambayo inaongoza katika Kanisa; una mikono ambayo inatoa kwa maskini; una macho ambayo yanakuja kutambua yule mwenye kuhitaji(In Epistolam Joannis ad Parthos, 7, 10)” na alikuwa ameongeza kuandika  kuhusiana na upendo kwamba: “Ushikilieni, ukumbatieni: hakuna kilicho kitamu zaidi kama huo.” Papa Leo XIV kwa njia hiyo alisema: “tazama zawadi ya mwanga ambayo imekabidhiwa kwenu, kwa sababu muifanye ikue ndani mwenu, na kati yetu kwa utamu wake na kuineza katika ulimwengu, kwa sala, kuudhuria sakrameni na kutoa sadaka. Mwendelee kwa jitihada hizi katika safari yenu.” Moyo Mtakatifu wa Yesu, ambao Parokia yao imewekwa, iwaunde na kuwalinda daima zaidi katika jumuiya hiyo nzuri ,kwa sababu ndizo hisia za Kristo (Fil 2,5), kuishi na kushuhudia kwa furaha kujikita katika hazina ya neema ambayo waliipokea.

Papa Leo XIV huko Ponte Mammolo
Papa Leo XIV huko Ponte Mammolo   (@VATICAN MEDIA)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

15 Machi 2026, 18:00