Papa Leo XIV,Kwaresima 2026:Kusikiliza na kufunga na Kwaresima kipindi cha uongofu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
“Kusikiliza na kufunga. Kwaresima kama kipindi cha uongofu,” ndiyo kauli mbiu ya Ujumbe wa Baba Mtakatifu Leo XIV, uliochapishwa, Ijumaa tarehe 13 Februari 2026. Tukiwa tunaeleke katika kipinid hiki kikachofunguliwa na siku ya majivu kuanzia Jumatano ijayo tarehe 18 Februari, Baba Mtakatifu anaandika kuwa, Kwaresima ni kipindi ambacho Kanisa, kwa wasiwasi wake wa kimama, anatualika kujiweka katika fumbo la Mungu, katika kiini cha maisha yetu, kwa sababu imani yetu iweze kupata mwamko na moyo usipotelee kati ya wasiwasi na mahangaiko ya kila siku. Kila safari ya uongofu huanza wakati tunajiachia kufikiwa na Neno na kukaribisha kwa upole wa Roho. Kuna uhusiano, kwa njia hiyo kati ya zawadi ya Neno la Mungu, nafasi ya kukaribisha ambayo tunaitoa na mabadiliko ambayo hufanya. Kwa njia hiyo mchakato wa safari ya Kwaresima unakuwa fursa muafaka kwa ajili ya kutega sikio kwa sauti ya Bwana na kupyaisha maamuzi ya kufuata Kristo kwa kutembea naye katika njia ambayo inapanda Yerusalemu, mahali ambapo inatimizwa fumbo la mateso, kifo na ufufuko wake.
Kusikiliza
Baba Mtakatifu Leo XIV anaendelea fafanua kwamba, Mwaka huu anapenda kutoa umakini, awali ya yote juu ya umuhimu kwa kutoa nafasi katika Neno, kwa njia ya usikivu, kwa sababu, uwezekano wa kusikiliza ni ishara ya kwanza ambayo inaonesha shauku ya kuingia katika uhusiano na mwingine. Mungu mwenyewe, kwa kujionesha kwa Musa kutoka katika kichaka cha moto, anabainisha kwamba, kusikiliza ni tendo linalojitambulisha yeye ni nani: “Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimesikiliza kilio chao…” (Es 3,7). Kusikiliza kilio cha aliyekandamizwa ni mwanzo wa historia ya kuokolewa, ambapo Bwana anamwelekea Musa, kwa kumtuma afungue njia ya wokovu kwa wanae walioshia kuwa watumwa. Ni Mungu anayehusisha, ambaye leo hii anatufikia hata sisi kwa mawazo ambayo yanafanya kutetemeka moyo wake. Kwa njia hiyo, kusikiliza Neno katika Liturujia, linatuelimisha katika usikivu wa kweli zaidi wa uhalisia: kati ya sauti nyingi zinazokatisha maisha yetu na kijamii, Maandiko Matakatifu yatufanya kuwa na uwezo wa kujua yule anayepanda na mateso na ukosefu wa haki, ili aiweze kubaki bila jibu. Kuingia katika hali hii ya ndani ya upokeaji, maana yake ni kuacha kufundwa leo hii na Mungu kwa kumsikiliza Yeye, hadi kujitambua kuwa “hali ya umaskini unawakilisha kilio ambacho, katika historia ya binadamu, tunaalikwa kila mara katika maisha yetu, katika jamii yetu, mifumo ya sera za kisiasa na kiuchumi na si ya mwisho hata Kanisa.”
Kufunga
Baba Mtakatifu Leo XIV akiendelea kufafanu kuhusu kufunga, anabainisha kwamba, “ikiwa Kwaresima ni kipindi cha kuskiliza, kufunga inakuwa matendo ya thati ambayo yanahusisha na kupokea Neno la Mungu. Kufunga chakula, kiukweli ni zoezi la kale la kiibada na lisiloweza kubadilishwa katika safari ya uongofu. Kwa hakika ni kwa sababu linahusisha mwili, na kuufanya kuonekana kile ambacho tunacho yaani njaa na kile ambacho tunatambua kuwa muhimu kwa ajili ya kuishi. Inahitaji kwa njia hiyo, maang’amuzi na hamu ya kula ili kuweza kuthibiti njaa na kiu ya haki, kwa kuondoka katika kujizulu, na kujifunza ili kuweza kusali na kuwajibika kwa ajili ya jirani. Mtakatifu Agostino, Papa Leo anasisitiza kuwa, katika tasauti yake nyeti, anatazama mvutano kati ya kipindi kilichopo na utimilifu wa wakati ujao, ambao kwa njia hiyo ya ulinzi wa moyo hasa anaposema kuwa “ katika maisha ya hapa duniani, inahusisha watu kuwa na njaa na kiu ya haki, lakini kuridhika nayo ni kwa ajili ya maisha yajayo. Malaika wanashiba kwa mkate huo, chakula hicho. Watu kinyeme chake wana njaa, na wote wanaelekea shauku yake. Hii kuelekea katika shauku inapanu roho na kuongeza uwezo.” Kufunga, kwa maana hiyo , kunatufanya si tu kuwa na adabu ya shauku, ya kujitakasa na kufanya kuwa huru zaidi, lakini pia hata kuupanua kwa namna hiyo ambayo inamhusisha Mungu na kuelekeza kutenda kwa ajili ya wema.
Hata hivyo ili kufunga kuweze kuhifadhi ukweli wake wa kiinjili na kukimbia kishawishi cha kiburi, moyo lazima na daima uishi katika imani na katika unyenyekevu. Hii inahitaji kubaki umesimika mizizi katika ushirika na Bwana, kwa sababu Yeye asiyefunga kweli ni yule ambaye hajui jinsi ya kumwilishwa kwa Neno la Mungu. Kwa kuwa ni ishara inayoonekana ya jitihada zaidi za ndani za kutuondoa katika dhambi na ubaya kwa msaada wa neema, kufunga lazima kujumuishe hata aina nyingine za kujinyima ambazo mara nyingi utufanya kupata mtindo mmoja wa maisha matulivu zaidi, “kwa kuwa “Udhibiti tu ndio hufanya maisha ya Kikristo kuwa imara na ya kweli.” Papa Mtakatifu kwa njia hiyo anapenda kuwaalika katika mfungo mpana wa dhati na mara nyingi haupongezwi, yaani ule wa maneno ambayo yanagonga na kuumiza jirani zetu. Tuanze kuondoa silaha za lugha, kukataa maneno yenye ncha kali, hukumu za haraka, kumsema mwingine vibaya hasiyekuwepo na hasiweze kujitetea, na kashfa. Kinyume chake tujitahidi kupima, maneno kujifunza na kukuza ukarimu; ndani ya familia, kati ya marafiki, katika maeneo ya kazi, kwenye vyombo vya habari, katika mijadala ya kisiasa, kwenye njia ya mawasiliano, na katika jumuiya za kikristo. Kwa njia hiyo maneno mengi ya chuki yataacha nafasi kwa maneno ya mtumaini na ya amani
Kwa Pamoja
Katika kipengele cha Pamoja, Baba Mtakatifu Leo XIV, alisema “na mwisho, Kwaresima, inaweka wazi juu ya nafasi ya kijumuiya katika kusikiliza Neno na zoezi la kufunga. Hata Maandiko Matakatifu, yanasisitiza mantiki hii kwa namna nyingi. Kwa mfano yanasimulia katika Kitabu cha Nehemia, kwamba Watu walikusanyika kwa ajili ya kusikiliza Neno kwa umma kutoka kitabu cha Torati na kufanya zoezi la kufunga, walikiri imani yao wakaabudu kwa namna ya kupyaisha agano lao na Mungu(Neh 9,1-3.) Na wakati huo huo, parokia zetu, familia, makundi ya kikanisa na jumuiya za watawa zinaalikwa kutumza, katika kipindi cha Kwaresma mchakato wa safari ya ushirikishwaji, ambapo kuna kusikiliza Neno la Mungu, kama ilivyo kilio cha masikini na cha dunia, kugeuka kuwa mtindo wa maisha ya pamoja na kufunga, kunamaanisha kutubu kweli. Upeo huo, wa uongofu unatazama zaidi ya dhamiri ya kibinafsi hata mtindo wa mahusiano, ubora wa mazunguzo, uwezo wa kuacha kujiuliza kutokana uhalisia na kutambua kile ambacho kinaelekeza shauku kweli, iw ya jumuiya zetu za kikanisa, na ile ya ubinadamu wenye kiu ya haki na upatanisho.
Kwa kuhitimisha, Papa Leo XIV alibainisha kwamba tuombe neema ya Kwaresima ambayo inatufanya kuwa makini katika masikio yetu kwa Mungu na kwa walio wa mwisho. Tuombe nguvu za kufunga, ambayo ipitie hata katika lugha, kwa sababu maneno yanayohumiza yapungue, na kukua nafasa kwa ajili ya sauti ya mwingine. Na tujitahidi ili Jumuiya zetu zigeuke kuwa mahali ambapo kilio cha anayeteseka apate makaribisho na usikivu uzae michakato ya safari ya uhuru, kwa kutufanya kuwa tayari na wenye bidii katika kuchangia ujenzi wa ustaarabu wa upendo. Kwa myo wote Baba Mtakatifu anawabariki wote na kuwatakia safari njema ya Kwareseima.
Asante kwa kusoma makala haya. Ukitaka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida kwa kubofya hapa: cliccando qui.
