Tafuta

Moja ya picha huko Sahel. Moja ya picha huko Sahel.  (AFP or licensors)

Sheria Mpya kwa ajili ya Utume wa Mfuko wa Kipapa wa Sahel

Katika andiko la Kisheria,Papa Leo XIV aliidhinisha Sheria mpya ya Mfuko wa Yohane Paulo II kwa ajili ya Sahel,ulioanzishwa mwaka 1984 kwa utashi Papa wa Poland ili kupunguza mateso ya watu wa eneo hilo la Afrika,wanaosumbuliwa na ukame,jangwa na njaa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Baba Mtakatifu Leo XIV akikutana na Kardinali, Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, tarehe 29 Januari 2026, kwa kuzingatia hitaji la kurekebisha hadhi ya kisheria ya Mfuko wa  "Yohane Paulo II kwa ajili ya Sahel", ukilinganisha na mfumo wa sasa wa udhibiti wa vyombo vya kisheria vya Curia Romana,  na Sheria kuhusu urithi wa Kiti Kitakatifu, amekubali kuidhinisha kwa Sheria iliyorekebishwa ya Chombo hicho hicho. Hii ilitangazwa katika Hati iliyochapishwa  tarehe 5 Februari 2026, na Ofisi ya Habari ya Vatican. Baba Mtakatifu pia ameamuru kwamba Sheria hiyo ichapishwe katika Gazati la Osservatore Romano, na baadaye, katika ufafanuzi rasmi wa Acta Apostolicae Sedis, yaani Hati za Kiti cha Kitume, na kuanza kutumika leo.

Historia ya Mfuko

Katika  maneno ya Papa Yohane Paulo II, yaliyosemwa tarehe 10  Mei 1980, huko Ouagadougou, mji mkuu wa Upper Volta (sasa Burkina Faso), yaliwasha cheche iliyosababisha kuundwa kwa Mfuko wa Sahel, ambao bado una jina lake hadi leo hii. Ikikabiliwa na ukosefu wa maji na chakula na kuenea kwa jangwa, Papa wa Poland alitoa wito mzito wa kuchukua hatua kwa ulimwengu mzima, na kuwa "sauti ya wale wasio na sauti: sauti ya wasio na hatia waliokufa kwa sababu walikosa maji na mkate; sauti ya baba na mama waliowatazama watoto wao wakifa bila kuelewa."

Mfuko wa Yohane Paulo II wa Sahel ulianzishwa, kwa idhini ya Papa ya sheria zake, mnamo tarehe 22 Februari 1984, ili wito wake mzito utekelezwe na kubaki ishara madhubuti ya upendo wake kwa kaka  na dada zake wa Kiafrika. Mkataba huo unaanzisha Mfuko huo kama chombo muhimu cha kisheria cha Baraza la Kipapa la Kuhamaisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu, unaoongozwa na kanuni ya Vatican na sheria za kiraia zinazotumika kwa vyombo vya kisheria vilivyoko Jijini Vatican. Ofisi iliyosajiliwa ya Mfuko huu ipo Vatican, huku makao makuu ya utendaji kazi yake yako Ouagadougou.

Mkataba mpya, matokeo ya mchakato mrefu na wa pamoja wa mageuzi

Mjumbe wa Kipapa la Baraza laKuhamaisha Maendeleo Fungamani ya  Binadamu, katika taarifa yake, lilionesha kuridhika na kuchapishwa kwa Mkataba mpya, "matokeo ya mchakato mrefu na wa pamoja wa mageuzi ya kitaasisi ya Mfuko." "Uteuzi, mnamo Desemba 2024, wa mjumbe wa kipapa, Askofu Florent Hassa Koné, wa  Mali, na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko, ulifanywa, kwa lengo la kusindikiza na hatua za mwisho za mchakato huu katika mazungumzo ya mara kwa mara na Vatican." Safari hii, inasisitizwa, imefuatiliwa na Baraza la Kipapa kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Vatican, ya Uchumi, na Gavana. Kwa mujibu wa Katiba mpya, taarifa hiyo inasema, "Mfuko unazidi kuwa karibu na Kanisa Mahalia  ukiambatana kwa urahisi na michakato kuelekea maendeleo ya haraka na endelevu zaidi na kukabiliana hasa na changamoto nyingi zinazokabili eneo hilo."

 Kutenda katika roho ya maendeleo ya binadamu jumuishi na yanayounga mkono

Mfuko huu unajumuisha nchi tisa katika eneo la Sahel: Burkina Faso, Cape Verde, Gambia, Guinea-Bissau, Mali, Mauritania, Niger, Senegal, na Chad. "Lengo kuu la Mfuko," inasema Sheria yake, "ni kukuza mafunzo ya watu wanaojitolea kuitumikia nchi yao na wanadamu wenzao, bila ubaguzi, katika roho ya maendeleo fungamani ya  binadamu na yanayounga mkono, kupambana na kuenea kwa jangwa na sababu zake na kutoa msaada kwa waathiriwa wa ukame katika nchi za Ukanda wa  Sahel."

Kwa hivyo, Mfuko unaweka kipaumbele katika mafunzo ya wawezeshaji na wataalamu wa ndani, pamoja na kufadhili mipango katika maeneo yafuatayo: maendeleo ya kiufundi, huduma za kijamii na afya, maendeleo ya kijamii na kilimo, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, maendeleo fungamani, na mazingira. Papa hutoa mapato ya makusanyo yaliyopangwa  ulimwenguni kote kwa manufaa ya Sahel kwa Mfuko hip. Mihimili inayoongoza ya Mfuko ni Bodi ya Wakurugenzi, Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu, Mkaguzi, na Mweka Hazina. Mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi utafanyika katikati ya Februari huko Dakar, Senegal.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

05 Februari 2026, 16:32