Safari ya Papa ya kwenda Ufalme wa Monaco inatazamiwa!
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Ziara ya Papa Leo XIV kwenda Ufalme wa Monaco inazingatiwa. Kwa mujibu wa Ofisi ya Habari ya ya Vatican ilitangaza hili kujibu maswali kutoka kwa mashirika kadhaa ya habari. Itakuwa siku moja mwishoni mwa mwezi Machi. Ikiwa itathibitishwa, Ziara ya kwenda Monaco itakuwa ya pili kwa Papa Leo XIV tangu mwanzo wa upapa wake, na ziara ya kwanza ya Papa kwenda Ufalme katika historia ya kisasa. Hija ya kwanza ya Papa Leo XIV nje ya Italia ilifanyika nchini Uturuki na Lebanon kuanzia Novemba 27 hadi 2 Desemba 2025.
Katika safari ya kurudi, akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu safari za baadaye, Papa alionesha hamu yake ya kusafiri kwenda Algeria kutembelea maeneo ya Mtakatifu Augustine, lakini pia kuendeleza mazungumzo kati ya ulimwengu wa Kikristo na Kiislamu. "Ni wazi," alisema, "Ningependa sana kutembelea Amerika Kusini," akimaanisha Argentina na Uruguay, ambazo zina uhakika katika ziara ya Papa, na pia Peru, nchi ambayo Robert Prevost alikuwa mmisionari kwanza na kisha Askofu.
Mnamo tarehe 17 Januari 2026, Papa Leo XIV alimpokea Mfalme Albert II wa Monaco katika mkutano wa pamoja mjini Vatican, ambaye baadaye alikutana na Sekretarieti ya Vatican. Mkutano huo, kwa mujibu wa Ofisi ya Habari ya Vatican iliripoti wakati huo, kuwa "ulilenga uhusiano mzuri wa pande mbili uliopo na mchango wa Kanisa Katoliki katika maisha ya kijamii ya ya Ufalme huo. Pamoja na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, mkutano huo ulijadili masuala yenye maslahi ya pamoja, kama vile ulinzi wa mazingira, misaada ya kibinadamu, na ulinzi na ukuzaji wa utu wa binadamu. Mada hizo pia zilijumuisha masuala ya kimataifa ya sasa, hasa kuhusu amani na usalama."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.
