Tafuta

2026.02.14 Wanachama wa Shirikisho la Kitaifa la (Misericordie d'Italia) Mashirika mbali mbali ya msaada na huruma. 2026.02.14 Wanachama wa Shirikisho la Kitaifa la (Misericordie d'Italia) Mashirika mbali mbali ya msaada na huruma.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:muwe wajumbe wa matumaini,upendo na amani

Papa Leo XIV akikutana na Wanachama wa Shirikisho vya Vyama vya Huruma(Misercordie)vya Italia,Februari 14,aliwahimiza kuendelea na kujitolea kwao,kama jumuiya ambayo imani huishwa kwa bidii na upendo hutekelezwa.Walenge kukua katika roho na kutumikia kwa furaha na unyenyekevu,wakiwa mbali na mantiki yoyote ya nguvu wakijitolea kwa sifa ya Mungu na wema kwa wale ambao Bwana anawaweka katika njia zao.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tasaufi ya kiroho, upendo na  umakini kwa mahitaji ya leo hii, ilikuwa ni kiini cha hotuba ya Baba Mtakatifu Leo XIV kwa wanachama wa Shirikisho la Kitaifa la Misericordie yaani wa huruma nchini Italia  aliokutana nao mjini Vatican, Jumamosi tarehe 14 Februari  2026. Akianza na ishara ya Msalaba, salamu na kuwakaribisha, Papa alionesha furaha ya kukutana  nao wote, wengi sana, kutoka sehemu mbalimbali za Italia. Papa alimsalimu Askofu Mkuu Franco Agostinelli, msimamizi mkuu na msaidizi wa kiroho, Maaskofu wengine waokuwapo na  Dkt. Domenico Giani, Rais wa Kitaifa wa Shirikisho, Wasaidizi  na wawakilishi wa ofisi mbalimbali nchini Italia na nje ya nchi. Shirikisho la Misericordie,  lina historia ya karne nyingi, yenye mizizi katika Enzi za Kati, inayojumuisha vipimo vitatu muhimu vya maisha ya Kikristo ya walei: tasaufi za kiroho, upendo, na kuzingatia mahitaji ya leo hii.

Shirikisho la vyama vya Huruma na upendo nchini Italia
Shirikisho la vyama vya Huruma na upendo nchini Italia   (@Vatican Media)

Papa alianza kudadavua kuwa “Kwanza, hebu tufikirie tasaufi ya kiroho. Tangu mwanzo wake, ushirika wao  umepata nguvu na msukumo hasa kutoka kwa maisha ya imani na utendaji wa kisakramenti wa washiriki wake.  Hivyo ndivyo ilivyokuwa enzi ya kati, katika karne ya 13 huko Firenze katikati ya vita na migogoro ya ndani, ndani ya jamii za kiraia na za kikanisa, kutokana na kazi ya watu mashuhuri kama vile Mtakatifu Petro shahidi  na Piero di Luca Borsi, baadhi ya waamini wa kawaida waliamua kuanza njia tofauti, ya kujitolea na huduma. Mfano wao, labda kwa sababu ya unyenyekevu wa kweli, ulienea kwa haraka kwa wengi, kwanza nchini Italia na kisha katika nchi zingine, hadi Ureno na kutoka hapo hadi Amerika. Mbegu ambayo kwao ni mti mkubwa ni sehemu yake ulichipuka na kukua kwa hivyo ni wa kisakramenti, ambayo imejengwa juu ya Ubatizo na kwa hivyo maadili na kujinyima.

Papa alikutana na Shirikisho la Vyama vya Huruma na Upendo Italia
Papa alikutana na Shirikisho la Vyama vya Huruma na Upendo Italia   (@VATICAN MEDIA)

Baba Mtakatifu aliendele kusema kuwa hili linamaanisha kwao, kwamba ili mmea uendelee kukua, jukumu la kukuza, kwanza kabisa, kwa kujitolea sana, malezi ya Kikristo ya washiriki wao kupitia sala, katekesi, uaminifu kwa Sakramenti hasa Misa za kila Dominika, kitubio na mshikamano wa maadili wa chaguo na mitindo wao wa maisha, kulingana na maadili ya Injili na mapokeo ya chama kama yanavyothibitishwa na Sheria zao. Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili aliwakumbusha washiriki wa Shirikisho lao  kuhusu hili, akisema: "Kwa kupokea Sakramenti kwa bidii, mtakuwa mashuhuda  wenye furaha wa maisha halisi ya Kikristo na mtasaidiwa katika hatua zenu mkimfuata Bwana wa uzima, ambaye kupitia nyinyi anataka kufichua kwa ulimwengu wa leo, kwa watu wa wakati huu wa kushangaza na usio na utulivu, uso wa kweli wa Mungu, 'mwingi wa rehema” (Efe 2:4)" (Hotuba kwa wanachama wa Shirikisho la Misericordie za Italia, Juni 14, 1986).

Waisaidizi na wasafiri wenza katika huduma 

Katika mtazamo huo Papa aliongeza  “utangulizi kati yenu wa sura ya Walinzi wa Huruma, walei wanaowahuisha walei wengine, ni muhimu; pamoja na jina "warekebishaji," ambalo mnawaita Wasaidizi wa Kiroho, ambao hawaonekani kama viongozi wa nje ya jumuiya, bali kama "wasaidizi, wawezeshaji na wasafiri wenzao, ambao huduma yao inatekelezwa na kukaribishwa katika mazingira ya uwajibikaji , hisia za pamoja, na ushirika, ambapo wote ni wahusika wakuu katika juhudi za pamoja za kukua katika ukamilifu wa Kikristo.

"Maisha lazima yatiririke katika usikivu wa mahitaji ya wengine na huduma ya ukarimu"

Papa alidadavua kipengele cha  pili kuhusu upendo. Historia yao inashuhudia kwamba, maisha halisi ya imani hayawezi kuishia katika  uroho roho usio na mwili, bali lazima yatiririke katika usikivu wa mahitaji ya wengine na katika huduma ya ukarimu na isiyo na kikomo. Papa katika hilo aliwafikiria kaka na dada zao  wengi ambao wamelipa kibinafsi, hata kwa gharama kubwa, kwa uaminifu wao kwa kazi waliyopewa: kwao iliwaendea  shukrani zeti   za dhati na sala zetu. Popote pale panapohitajika, Wanachama wa   Huruma(Misercodie) wapo, katika hali za dharura maalum,  katika maeneo ya vita, na pia katika huduma nyingi sana zilizofichwa za mshikamano wa kila siku, "kutoa ushuhuda," kama Papa Francisko alivyosema kuwa, "kwa Injili ya upendo miongoni mwa wagonjwa, wazee, walemavu, watoto, wahamiaji, na maskini" (Hotuba kwa Vikundi vya Wamisricordie na Undugu  vya Italia, Juni 14, 2014).

Shirikisho la vyama vya Huruma na Upendo Italia
Shirikisho la vyama vya Huruma na Upendo Italia   (@Vatican Media)

Kupitia Nyumba zao,  Mashirika ya Mshikamano, Benki za Chakula, huduma za nyumbani, huduma za ushauri na usaidizi, wanaanzisha uhusiano wa uaminifu na watu na njia za kuunganishwa tena kijamii, ambazo zinaenda mbali zaidi ya utoaji rahisi wa huduma, hata kama zina sifa gani. “Hamjiwekei kikomo cha "kutendea," bali mnajitolea "kutembea na," mkitambua kwa wengine kaka na dada, kila mmoja akiwa na hadhi na historia yake,” kwamba wote  watapata shukrani kwa zawadi ya pamoja na nani wa kutembea naye pamoja katika njia ya utakatifu.

Wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Huruma Italia
Wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Huruma Italia   (@Vatican Media)

"Umakini kwa mahitaji ya leo hii"

Papa vile vile alielezea  jambo jingine moja la mwisho na la kuzingatia kwamba ni: umakini wao kwa mahitaji ya leo, ambayo pia yanawatambulisha. Hakika, kutokana na msingi imara wa kiroho na kijamii na ari kwa ajili ya mema ya wengine, Wanachama wa Huruma (Misericordie) kwa karne nyingi wamekuwa mashuhuda wa uwezo wa kubadilika na kusasisha, wakionesha kwamba kufanya kazi "pamoja" na kufanya kazi "kwa upendo" pia hutusaidia kutenda kwa uhuru na ubunifu (Papa Francisko Hotuba kwa wanachama wa Caritas Italiana kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwake, Juni 26, 2021).

Shirikisho la Vyama vya Huruma na Upendo nchini Ialia
Shirikisho la Vyama vya Huruma na Upendo nchini Ialia   (@Vatican Media)

“Hili linaonekana katika shughuli nyingi na tofauti ambazo mmekumbatia kwa mamia ya miaka, kulingana na mahitaji ya wengine; kama ilivyo uwepo, katika ukumbi huu,” Papa alongeza “ pamoja na kaka na dada, na ndugu, waliojiunga hivi  karibuni ili kukuza utamaduni wa kutoa kupitia mchango wa damu, viungo, na tishu; na pia "Huruma Ndogo," ambapo mtu hujifunza kufanya kazi ya upendo tangu mwanzo, akiwa mtoto.”

"Daima muwe wajumbe wa matumaini, upendo na amani"

Papa Leo aliwahimiza kwa njia hiyo kuendelea na kujitolea kwao, kama jumuiya ambayo imani huishwa kwa bidii na upendo hutekelezwa. Walenge kukua katika roho na kutumikia kwa furaha na unyenyekevu, wakiwa mbali na mantiki yoyote ya nguvu, wakiwa wamejitolea kwa sifa ya Mungu na wema wa wale ambao Bwana anawaweka katika njia zao. Daima wawe wajumbe wa matumaini, upendo, na amani, kama inavyooneshwa na Alama ya Jubilei ambayo, kwa safari ndefu, imetembelea Jumuiya  nyingi na sasa imewasilishwa kwa kaka na dada zetu nchini Ukraine. Papa alihitimisha kwa kuwashukuru kwa yote wanayofanya, anawakumbuka katika sala zake, aliwapatia   kwa furaha nyinyi na familia zao, Baraka ya  Kitume.

Magari ya Shirikisho la vyama vya Huruma na Upendo Italia
Magari ya Shirikisho la vyama vya Huruma na Upendo Italia   (@Vatican Media)
Uwakilishi wa Shirikisho la Vyama vya Huruma Italoa
Uwakilishi wa Shirikisho la Vyama vya Huruma Italoa   (@Vatican Media)
Papa Leo XIV kwa Misercordie

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

14 Februari 2026, 12:44