Papa Leo:Papa:Mustakabali wa ubinadamu upo katika udugu,si mikakati ya kijeshi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika 5 ya Kipindi cha Mwaka wa Kawaida na Mama Kanisa akiwa anamkumbuka Mtakatifu Josephine Bakhita, Mtawa, tarehe 8 Februari 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV aliwageukia waamini waliokufanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na kwamba:“ Jana huko Huércal-Overa, Nchini Hispania, Padre Salvatore Valera Parra, Padre wa Parokia aliyejitolea kikamilifu kwa watu wake, mnyenyekevu na makini katika upendo wake wa kichungaji, alitangazwa kuwa Mwenyeheri. Mfano wake kama Padre anayezingatia mambo muhimu uwatie moyo mapadre wa leo hii kuwa waaminifu katika maisha yao ya kila siku, wakiishi kwa urahisi na umakin.”
Papa Leo aliongeza kusema kuwa “Ni kwa huzuni na wasiwasi kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya jumuiya mbalimbali nchini Nigeria, ambayo yamesababisha vifo vingi. Ninaelezea ukaribu wangu wa maombi kwa waathiriwa wote wa vurugu na ugaidi. Ni matumaini kwamba mamlaka husika zitaendelea kufanya kazi kwa dhati ili kuhakikisha usalama na ulinzi wa maisha ya kila raia.”
Kumbukizi ya Mtakatifu Bakhita
Leo, katika ukumbusho wa Mtakatifu Josephine Bakhita, tunaadhimisha Siku ya Maombi na Tafakari Ulimwenguni dhidi ya Biashara Haramu wa Binadamu. Ninawashukuru Watawa na wote waliojitolea kupambana na kuondoa aina za sasa za utumwa. Pamoja nao, ninasema: amani huanza na utu!” Alisema hilo kama kauli Biu ya Toleo hilo lilioanzishwa na Hayati papa Francisko kunako mwaka 2015.
Maombi ya Papa kwa Ureno, Morocco na Hispania
Papa Leo XIV aliendelea kusema kuwa “Ninawahakikishia maombi yangu kwa ajili ya watu wa Ureno, Morocco, Hispania, hasa Grazalema huko Andalusia, na kusini mwa Italia, hasa Niscemi huko Sicilia, waliokumbwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi. Ninawahimiza jamii kubaki na umoja na mshikamano, kwa ulinzi wa Mama wa Bikira Maria.”
Salamu kwa mahujaji
Papa aliwakaribisha wote, Warumi na mahujaji kutoka Italia na nchi mbalimbali. Aliwasalimu waamini kutoka Melilla, Murcia, na Malaga nchini Hispania; wale kutoka Belarus, na Latvia; wanafunzi kutoka Olivenza, Hispania; na wanakipaimara kutoka Malta. Pia ninawasalimu vijana wanaojiunga nasi kutoka kwenye mihadhara mitatu katika jimbo la Brescia.
"Tuendelee kuombea amani:mustakabali wa ubinadamu inapatika katiak heshima na udugu na sio nguvu za kijeshi"
Tuendelee kuombea amani. “Historia ya inatufundisha kuwa Mustakabali wa Ubinadamu haupatikani katika mikakati ya nguvu za kiuchumi na kijeshi, bali Wakati ujao upo katika heshima na udugu miongoni mwa watu”. “Ninawatakia kila mmoja Dominika njema.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.
