Tafuta

2026.02.28 Papa akutana na waseminari na walezi wao kutoka majimbo tofauti ya Hispania. 2026.02.28 Papa akutana na waseminari na walezi wao kutoka majimbo tofauti ya Hispania.  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV:Maisha ya kiroho huzaa matunda kwa kusimika mizizi ndani ya Mungu

Mwanadamu hakuumbwa kuishi amefungwa ndani yake mwenyewe,bali katika uhusiano hai na Mungu.Ni katika Hotuba ya Papa Leo XIV kwa Waseminari na Walezi wao kutoka Seminari 4 za Hispania,mnamo Jumamosi Februari 28.“Ni nini kinachoweza kuwa kisicho cha kawaida zaidi kuliko mseminari au Padre anayezungumza kuhusu Mungu kwa ujuzi,lakini anaishi ndani kana kwamba uwepo wake upo tu kwa kiwango cha maneno na si katika kina cha maisha?

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumamosi tarehe 28 Februari 2026 alitoa hotuba yake kwa Jumuiya Nne za Seminari za Kihispania: Alcalá de Henares, Toledo, na muungano wa majimbo ya Cataluña Cartagena, aliokutana nao katika Ukumbi wa Clementina mjini Vatican. Katika hotuba hiyo kwa lugha ya kihipania  Papa alisema kwamba, katika seminari daima ni ishara ya matumaini kwa Kanisa; kwa njia hiyo  alipenda kuungana nao  wote ambao wako kwenye mchato wa safari ya wito huo na wale  wanahusika na usindikizaji, kwamba kwake yeye "ni sababu ya kweli ya furaha."

Baba Mtakatifu  Leo XIV alieleza jinsi ambavyo angeweza kujadili mengi muhimu ya malezi yao, lakini ambayo alisema kuwa,  alikuwa tayari amewatumia barua kwa Seminari ya Mtakatifu Carlo na Mtakatifu Marceli huko nchini Peru, taasisi  ambayo pia alihudhuria yeye mwenyewe na  ambapo aliwatia moyo waisome barua hiyo  watakapokuwa na nafasi.  Papa Leo XIIV lakini alisema kwa siku hiyo alipenda kuelezea "kitu ambacho kingekuwa msingi wa kimya kimya wa kila kitu kingine, ambacho, hasa kwa sababu hiyo, kina hatari ya kuchukuliwa kirahisi bila kukuzwa ile hali ya: kuwa na mtazamo wa ajabu juu ya uhalisia."

Papa na waseminari kutoka majimbo kadhaa ya Hispania
Papa na waseminari kutoka majimbo kadhaa ya Hispania   (@VATICAN MEDIA)

Kuishi kwa kumtegemea Mungu

Papa Leo XIV alisisitiza kwamba “kuna msemo wa Chesterton ambao unaweza kutumika kama ufunguo wa kuelewa kila kitu ambacho” alipenda kushirikishana nao: "Ondoa kisicho cha kawaida, na hutapata cha asili, bali kisicho cha asili" (taz Heretics-Wazushi,VI). Mwanadamu hakuumbwa kuishi amefungwa ndani yake mwenyewe, bali katika uhusiano hai na Mungu. Uhusiano huu unapofichwa au kudhoofika, maisha huanza kufunguka kutoka ndani. Kisicho cha kawaida si kile tu kinachokashifu, kinatosha kuishi bila Mungu katika maisha ya kila siku, tukimwacha pembezoni mwa vigezo na maamuzi ambayo tunakabiliwa nayo kuwepo.”

Papa aliendelea kusema kuwa na “kama hili ni kweli kwa kila Mkristo, ni kweli hasa katika safari ya malezi kuelekea ukuhani. Ni nini kinachoweza kuwa kisicho cha kawaida zaidi kuliko mseminari au Padre  anayezungumza kuhusu Mungu kwa ujuzi, lakini anaishi ndani kana kwamba uwepo wake upo tu kwa kiwango cha maneno, na si katika kina cha maisha? Hakuna kitu kingekuwa hatari zaidi kuliko kuzoea mambo ya Mungu bila kuishi kwa kumtegemea Mungu. Kwa hivyo, hatimaye, kila kitu huanza na kila mara hurudi, kwenye uhusiano ulio hai na halisi na Yule aliyetuchagua bila sifa yoyote yetu wenyewe.”

Papa akutana na waseminari na walezi wao kutoka majimbo tofauti ya Hispania
Papa akutana na waseminari na walezi wao kutoka majimbo tofauti ya Hispania   (@VATICAN MEDIA)

Mti hauzai matunda kwa kukosekana matatizo,bali umesimika mizizi

Kuwa na mtazamo usio wa kawaida Papa alieleza “haimaanishi kutoroka ukweli, bali kujifunza kutambua kitendo cha Mungu katika matukio halisi ya kila siku; mtazamo ambao hauwezi kutengenezwa au kukabidhiwa, bali kujifunza na kutekelezwa katika hali za kawaida za maisha.” Na kwa sababu hiyo Papa alikazia  “hasa, ikiwa maono yasiyo ya kawaida ni muhimu sana kwa maisha ya Kikristo, ni zaidi kwa wale watakaotenda katika Kristo wa kibinafsi, na yanastahili kulindwa kwa uangalifu maalum kuanzia hatua ya malezi, kwa sababu ni kanuni inayotoa umoja kwa kila kitu kingine.” Mtazamo huu wa kuamini ukweli lazima ubadilike kuwa chaguo halisi za maisha kila siku; la sivyo, hata mazoea mazuri ya ndani, kusoma, kusali, maisha ya kijumuiya, yanaweza kuwa tupu ndani na kupotoshwa, na kuwa utimilifu wajibu tu.

"Njia rahisi na iliyothibitishwa ya kukuza mtazamo huu - Papa alifafanua  "ni kufanya mazoezi ya uwepo wa Mungu, ambao huweka mtazamo wa moyo na maisha yakielekezwa kwake kila wakati. Maandiko Matakatifu yanaelezea ukweli huu kwa picha rahisi katika Zaburi 1, yanapowaelezea wenye haki kama "mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, unaozaa matunda yake kwa majira yake, na jani lake halinyauki kamwe" (Zab 1, 3).” Papa alisistiza kuwa “Hauzai matunda kwa sababu ya  kukosekana kwa matatizo, bali ni katika mahali ambapo umesimika mizizi. Upepo, majira ya baridi kali, ukame, au kupukutika ni sehemu ya ukuaji wake, lakini dhoruba wala ukame hauuharibu wakati mizizi yake iko ndani na karibu na chanzo. Hata hivyo, Maandiko yenyewe yanatambua msemo wa mtini ambao hauzai matunda licha ya utunzaji unaopokea (taz Lk 13:6-9).

Kusimika mizizi kwa Mungu ili kutonyauka kama miti mikavu

Papa Leo alibainisha kwamba, “Inasemekana kwamba miti "hufa ikiwa imesimama:" hubaki wima, ikidumisha mwonekano wake, lakini ndani tayari imekauka. Kitu kama hicho kinaweza kutokea katika maisha ya seminari na baadaye katika ukuhani, wakati uzaaji unachanganywa na uzito wa shughuli au kwa umakini wa nje tu katika umbo. Papa alikazia kusema kuwa “Maisha ya kiroho huzaa matunda si kwa kile kinachoonekana, bali kwa kile kilicho na mizizi ndani ya Mungu. Mzizi huu unapopuuzwa, kila kitu hukauka kutoka ndani, hadi, kimya kimya, "kinakufa kwa miguu yake." Hatimaye, mtazamo wa ajabu hutoka katika kipengele rahisi na cha uamuzi zaidi cha wito wa “ kuwa na Bwana.” Yesu aliwaita wale aliowachagua "kuwa pamoja naye" (Mk 3:14).

Papa akutana na waseminari na walezi wao kutoka majimbo mbali mbali ya Hispania
Papa akutana na waseminari na walezi wao kutoka majimbo mbali mbali ya Hispania   (@Vatican Media)

Yote huanza katika mambo ya kawaida ya kila siku

Papa Leo XIV alisisitiza kwamba, "Huu ndio msingi wa malezi yote ya kikuhani: kubaki naye na kujiruhusu kuumbwa kutoka ndani; kumwona Mungu akitenda na kutambua jinsi anavyofanya kazi katika maisha ya mtu mwenyewe na ya watu wake. Kwa hivyo, ingawa rasilimali watu, saikolojia, na zana za malezi ni za thamani na muhimu, haziwezi kuchukua nafasi ya uhusiano huu.” Mhusika mkuu wa kweli wa safari hii ni Roho Mtakatifu,” ambaye huunda moyo, anatufundisha kuitikia neema, na kuandaa maisha yenye matunda katika huduma ya Kanisa.

Yote huanza sasa, katika mambo ya kawaida ya kila siku, ambapo kila mtu anaamua kama abaki na Bwana au kutafuta kujitegemeza kwa nguvu zake mwenyewe.” Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV aliwashukuru kwa  niaba ya Kanisa, kwa ukarimu wao  katika kuchagua kumfuata Bwana. “Daima fanyeni hivyo kwa uhakika kwamba hamtembei peke yenu: Kristo anawatangulia, Maria Mtakatifu awasindikize, na Kanisa lote linawaunga mkono kwa maombi yake. Kwa kuamini uhakika huu, endeleeni kwa amani na uaminifu. Bwana awabariki.”

Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

28 Februari 2026, 12:55