Tafuta

Tarehe 1 Machi 2026 Papa atatembelea Parokia nyingine ya Tatu kati ya Tano kabla ya Pasaka. Tarehe 1 Machi 2026 Papa atatembelea Parokia nyingine ya Tatu kati ya Tano kabla ya Pasaka.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV,Machi 1,atatembelea Parokia ya Quarticciolo:matumaini katika Eneo tete

Papa Leo XIV atatembelea Kanisa la Kupaa kwa Bwana Wetu Yesu Kristo Dominika Machi 1,kwa ziara yake ya tatu kati ya tano katika parokia za Jimbo la Roma kabla ya Pasaka.Papa atakutana na wajumbe mbalimbali wa jumuiya waliokabidhiwa kwa Mapadre wa Dehonian,wakiwemo watoto wa katekisimu,vijana na familia zao na mama wanne wa dawa za kulevya walio gerezani kwa sasa.Kisha ataadhimisha Misa saa 11.00 jioni.Paroko:"Tunasubiri kwa hamu kuwasili kwake."

 Vatican News.

Quarticciolo "kuna msisimko mkubwa wa kusubiri" ziara ya Papa Leo XIV ambaye  atawasili katika Parokia  ya Kupaa kwa Bwana Wetu Yesu Kristo (Njia ya Manfredonia, 5), iliyokabidhiwa kwa Mapadre wa Dehonian, Dominika tarehe 1 Machi 2026  saa 10 :00 jioni. Atakaribishwa, miongoni mwa wengine, na Kardinali  Baldo Reina, Makamu wake Jimbo Kuu la Roma na Padre Daniele Canali, Paroko wa Parokia ya Jumuiya hiyo.

Papa atakutana:watoto wa katekismu, vijana na familia zao kwanza

Papa atasimama kwanza katika uwanja wa ua wa Parokia  kwa hotuba fupi ambapo atakutana na wanafunzi wa katekisimu, vijana, na familia zao. Kisha, katika ukumbi wa parokia, atakutana na "jamii zilizo hatarini katika eneo hilo," kama Padre huyo wa parokia alivyowafafanua kuwa: uwakilishi wa wazee, wagonjwa, maskini, na walemavu, pamoja na watu wa kujitolea wanaowatunza. Miongoni mwao, katika kitongoji kinachochukuliwa kuwa mojawapo ya vituo vikubwa vya biashara ya dawa za kulevya jijini Roma, watakuwa mama wanne wa madawa ya kulevya walioko gerezani kwa sasa. "Hizi ni dalili za matumaini: mmoja ni katekista na mwingine ni mtu wa kujitolea wa Caritas," Padre Canali alibainisha

Msisimko na matarajio:kukutana na Baraza la Kichungaji la Parokia

Papa Leo atakutana na baraza la Kichungaji la Parokia hiyo katika ukumbi wa Parokia na saa 11:00 jioni, ataadhimisha Ibada ya Misa katika Kanisa la Parokia. Hatimaye, atakutana na jumuiya ya Mapadre. Kwa wale ambao hawataweza kuingia kanisani, Skrini kubwa itawekwa nje. "Hii ni ziara ya tatu ya Papa katika jumuiya yetu," Paroko wa parokia alikumbuka. "Mtakatifu Yohane XXIII alifika tarehe 3 Machi 1963, na Mtakatifu Yohane Paulo II alifika tarehe 3 Machi 1980." Na sasa ni zamu ya Papa Leo XIV. "Kuna msisimko na matarajio makubwa kwa ziara hii," Padre Canali aliongeza, akisisitiza: "Tunajiandaa sio tu kwa vitendo, kwa mpangilio wa vyumba vyote, lakini zaidi ya yote kiroho, na hotuba ya kila Juma. Makundi yote yametafakari juu ya Sura ya Petro."

Ishara ya Kuzaliwa Upya

Uwepo wa Papa ni ishara kubwa ya matumaini kwa eneo kama Quarticciolo. "Jumuiya hii ya parokia ni ndogo na imepitia nyakati ngumu sana kwa eneo hili," Padre huyo alisisitiza na kuongeza, "lakini lazima nishuhudie kwamba hakuna mtu aliyewahi kukata tamaa; jumuiya imekuwa ikisimama imara kila wakati. Kifungu kutoka Nabii Isaya kinanijia akilini: 'Mlinzi, ni nini kilichobaki cha usiku?' Papa anakuja kutuambia kwamba mchana umekaribia. Ninaona kama ishara ya kuzaliwa upya kwetu."

ZIARA YA PAPA KICHUNGAJI ROMA

Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

26 Februari 2026, 16:54