Tafuta

2026.02.27 Mheshimiwa Padre Darius Assande Ekou, Askofu Mteule wa Jimbo la Agboville nchini Ivory Coast. 2026.02.27 Mheshimiwa Padre Darius Assande Ekou, Askofu Mteule wa Jimbo la Agboville nchini Ivory Coast. 

Papa amteua Askofu wa Jimbo la Agboville,Ivory Coast,Padre Assandé Darius Ekou

Baba Mtakatifu Leo XIV amemtaua Askofu wa Jimbo la Agboville nchini Ivory Coast,Mheshimiwa Assandé Darius Ekou,ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Msimamizi wa Madhabahu ya Familia Takatifu ya Nazareth na Mkrugenzi wa Kituo cha Kijimbo cha Mtakatifu Kizito cha Abengourou.

 Vatican News.

Mweshimiwa Padre Assandé Darius Ekou aliyeteuliwa na Baba Mtakatifu tarehe 27 Februari 2026 alizaliwa tarehe 27 Aprili 1968 huko Bongouanou, katika Jimbo la Abengourou nchini Ivory Coast.  Mafunzo yake ya Falsafa na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Moyo Safi wa Maria huko Anyama.

Alipewa Daraja la Upadre tarehe 7 Septemba 1996.

Nyadhifa

Padre Assandé Darius Ekou ni Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Agbovile ameshika nafasi zifuatazo na kukamilisha masomo zaidi: Amehudumia  Kanisa Kuu la Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu huko Abengourou (1996-1998); Mkurugenzi wa Parokia ya Mtakatifu Bernadette huko Ebilassokro (1998-2001); Padre  Moyo Mtakatifu wa Koun-Abronso (2001-2002);

Masomo ya udaktari katika Mafundisho Jamii ya Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano,  Roma (2002-2009); Huduma ya Kichungaji katika Parokia ya Mtakatifu Lorenzo Shahidi huko Formello (Jimbo la  Civita Castellana) na katika Abasia ya Montevergine (Jimbo la Avellino) (2002-2009); Katibu wa Curia ya Abengourou (2009-2010);

Paroko wa Moyo Mtakatifu wa Yesu  huko Arrah (2010-2011); Paroko wa Mama Yetu wa Amani,  huko Abengourou-Plateau (2011-2014); Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme Abengourou (2014);  Hudma ya Sekta ya Moronou na Sekta ya Kituo cha Abengourou na Mkurugenzi wa Kazi Katoliki za Jimbo  na Mkurugenzi wa Kazi za Kimisionari za Kipapa kijimbo (PMS)(2011-2014); Profesa (2011-2014) na Gambera (2014-2025) wa Seminari Kuu ya Mama Yetu wa Guessihio-Gagnoa; Msimamizi wa Parokia-Madhabahu ya Familia Takatifu ya Nazareth na Mkurugenzi wa Kituo cha Jimbo  cha Mtakatifu Kizito huko Abengourou(tangu 2025). Mjembe wa Tum  ya Mapadre ,Seminari na Huduma ya Miito.

27 Februari 2026, 16:52