Tafuta

2026.02.05 Papa alikutana na  Edi Rama, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Albania. 2026.02.05 Papa alikutana na Edi Rama, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Albania.  (@Vatican Media)

Papa akutana na Waziri Mkuu wa Albania

Ijumaa tarehe 5 Februari 2026 Baba Mtakatifu alikutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Alibania na Ujumbe wake.Baadaye alikutana na Sekretarieti ya Vatican.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Kiti Kitakatifu imebainisha kuwa Ijumaa tarehe 5 Februari 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Albania, Bwana Edi Rama. Mara baada ya Mkutano huo, Waziri Mkuu huyo alikuwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, akisindikizana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa.

Waziri Mkuu wa Albania na wasindikizaji wake
Waziri Mkuu wa Albania na wasindikizaji wake   (@Vatican Media)

Katika mazungumzo yao na Sekretarieti ya Vatican, taarifa inabainisha kuwa, walionesha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Kiti Kitakatifu na Jamhuri ya Albania na walikabiliana  na mada za pamoja zinazowahusu hasa kati ya uhusiano wa pamoja na kikanisa na ule wa kiraia.

Waziri Mkuu wa Albania alikutana na Kardinali Parolin
Waziri Mkuu wa Albania alikutana na Kardinali Parolin   (@Vatican Media)

Wakiendelea na mazungumzo hayo, wamejikita pia na masuala Msingi wa kikanda, miongoni mwake ni kuhusu hali halisi katika nchi za kibalkani, Mashariki na hasa mchakato wa safari ya Albania kuelekea katika uungwaji kamili katika Umoja wa nchi za Ulaya.

 

05 Februari 2026, 16:24