Tafuta

Maua na ujumbe mbele ya bara iliyoungua moto huko Grans Montana nchini Uswiss. Maua na ujumbe mbele ya bara iliyoungua moto huko Grans Montana nchini Uswiss.  (ANSA)

Ukaribu wa Papa Leo XIV kwa waathirika wa Moto,Uswiss

Papa Leo XIV anapenda kuonesha ukaribu kwa ndugu wa waathirika,ushiriki na wasiwasi.Anasali kwa Bwana ili awapokee marehemu wote katika Nyumba ya amani na mwanga na awadumishe kwa ujasiri wale wanaoteseka kimoyo au kimwili kufutaia na kupoteza wapendwa wao.Haya yamo katika Salamu za rambi rambi zilizotiwa saini na Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican,kufuatia na waathirika wa mkasa wa moto uliolipuka huku Crans-Montana nchini Uswiss katika usiku wa kuamkia tarehe Mosi Januari.

Vatican News

Ijumaa tarehe 2 Januari 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV ametuma telegram ya rambi rambi iliyotiwa saini na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin kufuatia na mlipuko wa moto uliosambaa huko Crans-Montan, Uswiss, katika Usiku wa kuamkia tarehe 1 Januari 2026 na kusababisha makumi ya vifo na majeruhi wengi.

Katika salamu hizo za Papa zinaonesha huzuni na “kushiriki uchungu wa familia na Shirikisho zima la Uswiss.” Kwa njia hiyo Papa anapenda kuonesha ushiriki wake na wasiwasi kwa ndugu wa waathirika. Papa “Anasali kwa Bwana ili awapokee marehemu wote katika Nyumba ya amani na mwanga  wake na awadumishe kwa ujasiri wale wanaoteseka kiroho au  kimwilini. Mama wa Mungu, katika huruma yake, awape faraja ya imani, wote walioathiriwa na msiba huu na kuwadumisha katika tumaini.”

Idadi ya awali ya vifo kutokana na mkasa wa mkesha wa Mwaka Mpya huko Crans-Montana imeongezeka hadi 47 waliokufa na 113 wamejeruhiwa, wengi wao wakiwa katika hali mbaya.  Mamlaka ziliripoti vifo lakini hii bado inapaswa kuzingatiwa kuwa ya muda kutokana na hali mbaya za majeruhi wengi waliopelekwa hospitalini. Mamlaka ya Uswisi yanaamini moto huo unatokana na tukio la "kuungua kwa moto", kuenea kwa kasi na kwa nguvu kwa miale ya moto. Umri wa wastani wa waliohudhuria sherehe iliyoandaliwa kusherehekea kuwasili kwa 2026 katika ukumbi maarufu katika eneo la mapumziko ya kuteleza kwenye theluji , huko  Crans-Montana, Uswiss linalomilikiwa na wanandoa wa Kifaransa, ulikuwa na umri wa miaka 20.  Ufikiaji wa Bar hiyo uliruhusiwa kuanzia umri wa miaka 16.

Rambi rambi Papa kwa Uswiss
02 Januari 2026, 14:44