Tafuta

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Amerika ya Kusini na Caribbean CELAM, limewaandika ujumbe wa matumaini watu wa Mungu kutoka Venezuela wanaosafiri katika kipindi hiki kigumu cha historia na maisha ya nchi yao. Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Amerika ya Kusini na Caribbean CELAM, limewaandika ujumbe wa matumaini watu wa Mungu kutoka Venezuela wanaosafiri katika kipindi hiki kigumu cha historia na maisha ya nchi yao. 

Ujumbe wa Mshikamano wa CELAM na Watu wa Mungu Nchini Venezuela

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Amerika ya Kusini na Caribbean CELAM, limewaandika ujumbe wa matumaini watu wa Mungu kutoka Venezuela wanaosafiri katika historia, kuendelea kusherehekea Fumbo la Umwilisho, Kristo Yesu anapojifunua kwa walimwengu kama: Mfalme, Kuhani na Mkombozi wa dunia. Hiki ni kipindi cha kupyaisha imani, matumaini na mapendo; Mwenyezi Mungu ambaye yuko karibu na kati ya waja wake; Mungu anayetembea nao!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Ni katika muktadha wa shambulio kubwa la jeshi la Marekani nchini Venezuela, Baba Mtakatifu Leo XIV baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 4 Januari 2026 alisema kwamba, anafuatilia kwa karibu sana yale yanayoendelea kujiri nchini Venezuela. Anasema: Utu, heshima na haki msingi za watu wa Mungu nchini Venezuela zinapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza, ili hatimaye, kushinda vurugu na kuanza safari ya majadiliano katika: Ukweli, haki na amani; kwa kuheshimu uhuru wa nchi ya Venezuela, Sheria za Kimataifa sanjari na kuhakikisha utawala wa sheria uliowekwa katika Katiba, kuheshimu haki za binadamu na za kiraia za kila mtu, na kufanya kazi kwa umoja, ili hatimaye kuweza kujenga mustakabali tulivu wa ushirikiano kwa kutoa kipaumbele cha pekee kwa maskini wanaoendelea kuteseka kutokana na hali mbaya ya kiuchumi. Mwishoni mwa tamko lake, Baba Mtakatifu Leo XIV aliwaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kusali na kuyakabidhi maombi yao chini ya ulinzi na usimamizi wa Bikira Maria wa Coromoto na ya Watakatifu José Gregorio Hernández na Sr. Carmen Rendiles.

CELAM Ujumbe wa mshikamano na matumaini kwa watu wa Venezuela
CELAM Ujumbe wa mshikamano na matumaini kwa watu wa Venezuela

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Amerika ya Kusini na Caribbean CELAM, limewaandika ujumbe wa matumaini watu wa Mungu kutoka Venezuela wanaosafiri katika historia, kuendelea kusherehekea Fumbo la Umwilisho, Kristo Yesu anapojifunua kwa walimwengu kama: Mfalme, Kuhani na Mkombozi wa dunia. Hiki ni kipindi cha kupyaisha imani, matumaini na mapendo ya watu wa Mungu nchini Venezuela; Mwenyezi Mungu ambaye yuko karibu na kati ya waja wake; Mungu anayetembea bega kwa bega sanjari na kuwaangazia watu wake Nuru ya uso wake. Kama Mamajusi, CELAM inaendelea kutafuta nyota itakayowaongoza kwa Kristo Yesu; kwa kutoa kipaumbele cha kwanza kwa: utu, heshima, ustawi wa watu wa Mungu nchini Venezuela kama anavyokazia Baba Mtakatifu Leo XIV na kama kielelezo cha udugu na mshikamano wa kibinadamu.

RaisMaduro akiwa amekamatwa na vyombo vya Usalama Marekani
RaisMaduro akiwa amekamatwa na vyombo vya Usalama Marekani

CELAM inasema iko pamoja na inatembea pamoja na watu wa Mungu nchini Venezuela, ikihimiza juhudi za kujenga madaraja yanayowakutanisha watu; kuganga na kuponya majeraha; Kukuza na kudumisha mchakato wa majadiliano yanayosimika katika ukweli na uwazi kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Venezuela, bila ya kumtenga mtu awa yote. Kanisa linaitwa na kutumwa kuwa ni nyumba ya wazi, nafasi ya kukutana, na sauti tulivu inayotia matumaini, hata katikati ya matatizo na changamoto mamboleo. CELAM ina amini kwamba, watu wa Mungu nchini Venezuela, wataweza kutembea pamoja; watasikilizana na kuheshimiana; wakijikita katika kutafuta ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Popote palipo na ukweli, haki, rehema, na utunzaji wa maskini na wale walioko hatarini zaidi, Mwenyezi Mungu anajidhihirisha kwa mara nyingine tena, kati yao kama ilivyokuwa mjini Bethlehemu.

Ujumbe wa CELAM
07 Januari 2026, 15:08