Papa Leo XIV:Sala ya kufufua matumaini katika Ulimwengu mpya
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Leo XIV katika sala yake kwa njia ya video na sauti inayozindua mpango wa "Sali pamoja na Papa," inayohamasishwa na Mtandao wa Maombi Ulimwenguni na Baraza la Kipapa la Mawasiliano anafafanua kuwa ni “Nuru inayoongoza hatua zetu, kulisha wakati wa uchovu, tumaini gizani na nguvu katika Jumuiya zetu." Nia ya kwanza ya maombi kwa mwaka 2026, mwezi ambao utakuwa na Dominika ya Neno la Mungu litakaloandhimishwa tarehe 25 Januari, inaongozwa na mada: "Kwa ajili ya Sala na Neno la Mungu." Ni mwaliko wa kugundua upya nguvu ya kiroho ya Maandiko Matakatifu kama mahali pazuri pa kukutana na Kristo.
Injili, pumziko kwa moyo usiotulia
Papa Leo XIV anasali sala hiyo kwa lugha ya Kiitaliano, Kiingereza, na Kihispania katika Kanisa la Mtakatifu Pellegrino mjini Vatican, ambalo ni Kanisa la Kikosi cha Ulinzi na Usalama Vatican(Gendarmerie), mahali pa ukimya na uaminifu pia kwa wafanyakazi wa Vatican. Papa Leo XIV alisisitiza kwamba "Yesu, Neno lililo hai la Baba" ni "nuru inayoongoza hatua zetu." Tunajua kwamba moyo wa mwanadamu unaishi bila utulivu, una njaa ya maana, na ni Injili pekee inayoweza kuupatia pumziko na utimilifu.
Lishe na Matumaini
Mwaliko wa Baba Mtakatifu ni kujifunza kusikiliza Maandiko kila siku, kupingwa na kushangazwa na sauti yake, kutambua maamuzi tunayopaswa kufanya kwa ukaribu na moyo wake. Neno lako liwe lishe katika uchovu wetu, tumaini gizani, na nguvu katika jumuiya zetu.
Ulimwengu mpya
"Bwana," Papa Leo XIV anathibitisha, "Neno linalotufanya wana na ndugu, wanafunzi na wamisionari wa Ufalme wako lisipungue kamwe midomoni mwetu au mioyoni mwetu." Tufanye Kanisa linalosali kwa Neno, linalojenga juu yake na kulishiriki kwa furaha, ili tumaini la ulimwengu mpya liweze kuzaliwa upya katika kila mtu.
Kukutana na msamaha
Sala inayokuwa kitendo: hili ndilo tumaini la Papa Leo XIV, kwa sababu ni katika kukutana na Neno ambapo kila kitu hubadilika... Kutuhimiza kutoka moyoni kuwafikia wengine, kuwahudumia walio hatarini zaidi, kusamehe, kujenga madaraja, na kutangaza uzima
Kusali na Papa Leo
Sala ya "Sali pamoja na Papa" inapatikana kwenye tovuti na majukwaa ya kidijitali ya Mtandao wa Sala ya Papa Ulimwenguni ambao, pamoja na Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Vyomvo hivi vinakusudia kutoa msukumo mpya kwa usambazaji wa nia za maombi, waaminifu kwa utume wa awali lakini kwa lugha na zana zinazozidi kuwa za kisasa. Video ya Januari, pamoja na Kiingereza, Kihispania, na Kiitaliano, pia imepewa kichwa cha habari katika lugha zingine. Mtandao wa Maombi wa Papa Duniani ni Kazi ya Kipapa iliyokabidhiwa kwa Jumuiya ya Yesu. Ipo katika nchi zaidi ya 90 na inaleta pamoja jumuiya ya kiroho ya watu zaidi ya milioni 22. Katikati ya utume huu kuna nia za maombi za kila mwezi za Papa, ambazo zinatualika kuzingatia changamoto za ubinadamu na utume wa Kanisa.
