Papa Leo XIV:Olimpiki za Kipindi cha Baridi ziweze kukuza maadili
Vatican News
Olimpiki ya Majira ya Baridi kati ya Milano - Cortina, iwe "fursa nzuri ya kukuza maadili halisi ya michezo: uaminifu, heshima, roho ya timu na kujitolea, pamoja na ushirikishwaji wa kijamii na furaha ya kukutana." Hili ndilo tumaini lililooneshwa na Baba Mtakatifu Leo XIV, katika telegramu ya "salamu za dhati na za kuwatakia matashi mema watu wa Vikariate ya Bormio, wanaohusika katika maandalizi na uendeshaji wa Olimpiki," iliyoelekezwa kwa Kardinali Oscar Cantoni, Askofu Mkuu wa Como.
Vijana kutoka vyama vya michezo
Ujumbe huo, uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, ulisomwa wakati wa Misa iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo la Lombardia, Ijumaa tarehe 30 Januari 2026 saa 12:00 jioni, katika Parokia ya Bormio, kumkabidhi Mwenyezi Mungu Michezo ya 25 ya Olimpiki ya Majira ya Baridi huko Milano -Cortina 2026.
Sherehe hiyo, iliyofanyika katika Kanisa la Watakatifu Gervasius na Protasius, ilihudhuriwa na wanariadha vijana kutoka vyama vya michezo vya majira ya baridi, pamoja na mameneja wao, makocha, na wakufunzi, pamoja na wote wanaohusika katika kuandaa tukio hilo.
Parokia, Ishara ya Uwepo wa Kristo
Papa Leo XIV ambaye alionesha "shukrani kubwa kwa ushirikiano wa dhati katika tukio hili la michezo," kisha akawatia moyo "jumuiya za parokia mahalia kushiriki kwa uwazi katika tukio hili muhimu sana," ili waweze kutoa "ushuhuda wa Kikristo kwa ukarimu," na kuwa "ishara inayong'aa ya uwepo wa Kristo anayewaita kila mtu katika udugu." Akihitimisha telegramu yake, Papa aliwahakikishia sala zake na baraka zake za kitume, "ahadi ya neema nyingi za mbinguni."
Olimpiki ya Milano-Cortina itaanza tarehe 6 hadi 22 Februari 2026 na pia zitahusisha moja kwa moja eneo la Jimbo la Como, huku mbio hizo zikifanyika huko Livigno na Bormio.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here
