Tafuta

Olimpiki,Papa:kusaidia kukuza kukubalika,mshikamano na amani. Olimpiki,Papa:kusaidia kukuza kukubalika,mshikamano na amani. 

Olimpiki,Papa Leo XIV:Wasaidie kukuza kukubalika,mshikamano

Telegramu kutoka kwa Papa Leo XIV wakati wa kuwasili kwa Msalaba wa Wanamichezo Januari 29,katika Kanisa la Mtakatifu Babila huko Milano,ambapo utahifadhiwa kwa muda wote wa Michezo katika kipindi cha Baridi.Matumaini ya Papa ni kuwa tukio hilo litakuza urafiki na udugu,"likiimarisha ufahamu wa thamani ya michezo katika huduma ya maendeleo fungamani ya mwanadamu."

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Michezo ni kama mhamasishaji wa mshikamano na amani. Hili ndilo tumaini lililooneshwa na Baba Mtakatifu Leo XIV katika telegramu, iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, iliyoelekezwa kwa Askofu Mkuu Mario Delpini wa Jimbo Kuu la Milano. Telegramu hiyo kutoka kwa Papa Leo XIV ilikuwa inahusu kuwasili kwa Msalaba wa Wanamichezo tarehe 29 Januari 2026,  katika Kanisa la Mtakatifu Babila huko Milano, ambapo utahifadhiwa kwa muda wote wa Michezo ya Majira ya Baridi. Papa alielezea matumaini yake kwamba tukio hilo litakuza urafiki na udugu, "likiimarisha ufahamu wa thamani ya michezo katika huduma ya maendeleo fungamani ya binadamu."

Michezo ya Olimpiki na ihamasishe urafiki na udugu

Papa Leo XIV anaungana kiroho na wale wanaoshiriki kuanzia tarehe 29 Januari 2026, katika Kanisa la Mtakatifu Babila katika sherehe inayoongozwa na Askofu Mkuu, ambapo Msalaba wa Wanamichezo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki na Paralimpiki ya huko Milano-Cortina, itakayofanyika kuanzia tarehe 6 hadi 22 Februari 2026. Tumaini la Papa ni kwamba  tukio hili muhimu na lihamasishe hisia za urafiki na udugu, kuimarisha ufahamu wa thamani ya michezo katika huduma ya maendeleo fungamani ya binadamu.

Kujenga madaraja kati ya watu na tamaduni

Papa aliwahakikishia maombi yake: Siku hizi za mashindano yenye afya zichangie kujenga madaraja kati ya tamaduni na watu, kukuza kukubalika, mshikamano, na amani.

Kanisa la Mtakatifu Babila litakuwa Kanisa la wanariadha

Miongoni mwa wakonselebranti walikuwa Monsinyo Paul Tighe, Katibu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, na Padre Michele Gianola, Katibu Msaidizi wa Mkutano wa Maaskofu wa Italia (CEI) na Mkurugenzi wa muda wa Ofisi ya Kitaifa ya Huduma ya Kichungaji ya Burudani, Utalii, na Michezo. Wakati wa sherehe hiyo, ikitanguliwa na maandamano, sala maalum iliyotungwa kwa ajili ya tukio hilo na Delpini mwenyewe itasomwa.

Madhabahu ya Mtakatifu Babila itakuwa Kanisa la wanariadha huko Milano katika Michezo yote. Itakuwa na Msalaba wa Wanamichezo na paneli za maonesho zilizowekwa kwa maadili ya michezo, pamoja na marejeo ya kielimu na kiutamaduni. Pia itakuwa mwanzo wa Ziara ya Maadili ya Michezo, safari inayohusisha maelfu ya wasichana na wavulana kutoka shule, Klabu za vijana, na klabu za michezo, ikizingatia michezo kama uzoefu wa kibinadamu, kielimu, na kijumuiya.

PAPA OLIMPIKI CORTINA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.

29 Januari 2026, 17:46