Papa Leo XIV:Msingi wa maisha ya Mwili wa Kristo ni upendo wa Baba
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana Alhamisi tarehe 29 Januari na Washiriki wa Mkutano wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, katika Ukumbi wa Clementina mjini Vatican, ikiwa ni hitimisha la Mkutano wa wa Jumla ulionza Jumanne tarehe 27 Januari 2026. Hawa walikuwa ni Maafisa na wakuu wa Baraza la Kipapa, wakiongozwa na Kardinali Victor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza hilo. Papa Leo XIV alitoa shukrani zake ta dhati kwa huduma ambayo inahitaji uangalizi mkubwa wa kukaribisha na kusindikiza kwa ukarimu na hukumu zote, Maaskofu na wakuu wote hawa ambao wanaitwa kushughulikia kesi za uhalifu zilizo chini ya Baraza la Kipapa husika. Mara baada ya kuwakaribisha na salamu kwa Mwenyekiti wa Baraza hilo na wakuu na maafisi, Papa Leo XIV alisema wanavyojua vyema huduma ya thamani wanayoifanya, kwa lengo -, kama isemavyo katika Katiba ya Praedicate Evangelium ya "kumsaidia Baba Mtakatifu wa Roma na Maaskofu katika kutangaza Injili ulimwenguni kote, kukuza na kulinda uadilifu wa mafundisho ya Kikatoliki kuhusu imani na maadili, kutumia kutoka katika amana ya imani na kutafuta uelewa wa kina zaidi wa hilo mbele ya maswali mapya"(n. 69).
Ufafanuzi kuhusu Mafundisho ya Kanisa
Papa Leo XIV aliendelea kuwa, kazi yao ni kutoa ufafanuzi kuhusu mafundisho ya Kanisa, kupitia mwongozo wa kichungaji na kitaalimungu kuhusu masuala ambayo mara nyingi ni nyeti sana. Kwa lengo hilo, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Baraza la Kipapa limechapisha hati kadhaa; ambapo Papa alitaja muhima kama vile: la Nota Gestis verbisque, kuhusu uhalali wa Sakramenti (Februari 2, 2024), ambayo ilitoa maelekezo wazi ya kutatua kesi zenye mashaka kuhusu uendeshaji wa shughuli zao; Tamko la Dignitas infinita, kuhusu utu wa binadamu (Aprili 2, 2024), ambalo lilithibitisha tena utu usio na kikomo wa kila mwanadamu, ambaye leo hii yuko hatarini sana, hasa kutokana na vita vinavyoendelea na uchumi unaoweka kipaumbele katika faida; Kanuni za kuendelea katika Utambuzi wa Madai ya Matukio yasiyo ya Kawaida (Mei 17, 2024), ambazo zimesaidia kutatua kesi zinazohusiana na matukio kama hayo, ikiwa ni pamoja na ile inayohusu uzoefu wa kiroho wa Medjugorje, ambayo inahusu Ujumbe wa "Malkia wa Amani"(Septemba 19, 2024); Hati ya "Antiqua et Nova," iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu (Januari 28, 2025), ambayo inatoa uzingatiaji mpana na sahihi wa uhusiano kati ya akili Mnemba na akili ya binadamu;
Andiko la Mafundisho "Mater Populi Fidelis," kuhusu majina fulani ya Maria yanayorejeea kwa ushirikiano wa Maria katika kazi ya Wokovu (Novemba 4, 2025), ambayo inahimiza ibada maarufu ya Maria kwa kuchunguza misingi yake ya kibiblia na kitaalimungu, huku pia ikitoa ufafanuzi sahihi na muhimu kwa Elimu ya Maria (Mariology); Na mwisho Dokezo la Mafundisho,la "Una caro,” kuhusu Sifa ya Ndoa ya Mke Mmoja," kuhusu Thamani ya Ndoa kama Muungano wa Kipekee na Uhusiano wa Pamoja (Novemba 25, 2025), ambayo inachunguza kwa njia ya asili umoja wa ndoa kati ya mwanamume na mwanamke. Kazi hii hakika itafaidi sana ukuaji wa kiroho wa Watu wa Mungu watakatifu na waamini. Katika muktadha wa mabadiliko ya kihistoria tunayoyapitia, inawapatia waamini neno wazi na la haraka kutoka kwa Kanisa, hasa kuhusu matukio mengi mapya yanayojitokeza katika eneo la kihistoria. Pia inatoa mwongozo muhimu kwa Maaskofu kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zao za kichungaji, na pia kwa wataalimungu katika huduma yao ya masomo na uinjilishaji.
Papa anathamini mkutano wao kuhusu uenezaji wa imani
Baba Mtakatifu aidha alisema anavyothamini sana ukweli kwamba katika "Mkutano huu" huu wameanzisha mjadala wenye matunda kuhusu mada ya uenezaji wa imani, jambo la dharura kubwa katika wakati wetu. Hatuwezi kupuuza ukweli kwamba, katika miongo ya hivi karibuni, kumetokea kuvunjika kwa uenezaji wa imani ya Kikristo miongoni mwa Wakatoliki, na kwamba, hasa katika muktadha wa uinjilishaji wa kale, idadi ya wale ambao hawaoni tena Injili kama rasilimali ya msingi kwa ajili ya kuwepo kwao inaongezeka, hasa miongoni mwa vizazi vipya. Hakika, kuna vijana wengi wa kiume na wa kike wanaoishi bila kumrejeea Mungu na Kanisa, na ingawa hii inatuletea maumivu sisi waamini, lazima pia ituongoze kugundua upya "furaha tamu na yenye kufariji ya uinjilishaji," ambayo iko katikati ya maisha na utume wa Bibi arusi wa Kristo. Papa Leo aidha alisema kama alivyokumbusha katika hafla ya Mkutano Mkuu Maalum wa hivi karibuni, "tunataka kuwa Kanisa lisilojitazama lenyewe, yaani, kuwa la kimisionari, linatazama zaidi ya, kwa wengine; Kanisa linalotangaza Injili, zaidi ya yote kupitia nguvu ya mvuto, kama watangulizi wake Papa Benedikto XVI na Francisko walivyorudia kusema.
Kristo ni Upendo wa Baba
“Msingi wa maisha ya Mwili wa Kristo ni upendo wa Baba, uliofunuliwa kwetu katika Mwana aliyefanyika mwanadamu, aliyepo na anayefanya kazi ndani yetu kupitia kipaji cha Roho:” Kwa hivyo, "sio Kanisa linalovutia, bali Kristo, na ikiwa Mkristo au jumuiya ya Kanisa inavutia, ni kwa sababu kupitia "njia" hiyo huja damu ya uhai ya Upendo inayotiririka kutoka Moyo wa Mwokozi." Kanisa linamtangaza Kristo, bila upendeleo au upekee, na ndani yake, kila mtu ni na lazima ajitambue kama "mtendakazi rahisi na mnyenyekevu katika shamba la mizabibu la Bwana."
Kabla ya kuhitimisha Papa Leo alipenda kutaja huduma nyingine yao ambayo aliishukuru na ambayo ameikabidhi kwa uangalizi wao ile ya kukaribisha na kusindikiza, kwa wema na hukumu zote, Maaskofu na Wakuu wametakiwa kushughulikia kesi za uhalifu zilizotengwa kwa ajili ya Baraza la Kipapa. Hili ni eneo nyeti sana la huduma, ambapo ni muhimu kuhakikisha kwamba madai ya haki, ukweli, na upendo yanaheshimiwa na kuheshimu kila wakati. Baba Mtakatifu aliwashukuru tena kila mmoja wao kwa mchango muhimu wanaotoa kwa maisha na kazi ya Baraza la Kipapa na Kanisa zima, hasa wakati mchango huu unatolewa kwa unyenyekevu na busara. Ishara ya shukrani hii ni Baraka ya Kitume ambayo amewapa kwa moyo wote wao, na wapendwa wao, Papa alihitimisha.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here
