Tafuta

2026.01.31: Papa na Washiriki katika mkutano wa "Hackathon ya Ubunifu wa Kisiasa:ubinadamu mmoja,sayari moja." 2026.01.31: Papa na Washiriki katika mkutano wa "Hackathon ya Ubunifu wa Kisiasa:ubinadamu mmoja,sayari moja."  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV,wanasiasa Vijana:hakuwezi kuwa na amani kwa kuwatupa wanyonge

Kwa kundi la vijana wa kisiasa kutoka mabara yote,washiriki wa mkutano:"Ubinadamu Mmoja,Sayari Moja,"Januari 31 katika Ukumbi wa Clementine,Vatica,Papa Leo XIV alieleza:Kazi yao ina maana inapofanya kazi kwa ajili ya ubinadamu wenye amani katika haki."Ikiwa hatuwezi kukuza maelewano ndani ya chuo kikuu au mahali pa kazi,au miongoni mwa vyama vya kisiasa na vyama vya kiraia,tunawezaje kutumaini kujenga amani ndani ya jamii nzima,au kati ya watu na mabara?

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumamosi tarehe 31 Januari 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana katika Ukumbi wa Clementine mjini Vaitican na vijana ambao tangu Januari 26 hadi Februari 1, wanashiriki mjini Roma, Juma la mwisho la makazi ya mpango wa miaka miwili ya mafunzo katika hatua za kisiasa unaaohamasishwa na Shirika Lisilo la Kiserikali la Ubinadamu Mpya, la Harakati ya Kitume ya Wafocolare, kwa ushirikiano na Tume ya Kipapa ya Amerika Kusini na kwa usaidizi wa Mfuko wa Porticus. Mpango huo unatumia mbinu ile ya Hackathon, ambapo ni  warsha kubwa kwa washiriki ambao wanaweza kufanya kazi ili kupata suluhisho la matatizo ya pamoja. Wawakilishi wa vituo vya Harakati ya Wafocolare ya Umoja wa Kisiasa pia walihudhuria Mkutano wa pamoja na Baba Mtakatifu.

Wanasiasa vijana
Wanasiasa vijana   (@VATICAN MEDIA)

Utofauti si chanzo cha mgawanyiko, ni fursa ya ushiriki wa kisiasa 

Papa Leo XVI  katika hotuba yake, alifurahi kukutana nao vijana kutoka kila sehemu ya dunia, wakiwa wameunganishwa na kujitolea kwa pamoja kwa ajili ya kutafuta manufaa ya wote kupitia ushiriki wa kisiasa. Hawa wanatoka katika mataifa, tamaduni na desturi tofauti za kidini. Lakini utofauti huu si chanzo cha mgawanyiko miongoni mwao. Badala yake, ni fursa ya ushirikiano na ukuaji katika mtindo wa sinodi. Njia yao  ya kuendelea - kusikiliza kwa makini na kupambanua pamoja - si muhimu kwa maswali wanayoyashughulikia; badala yake, hutumika kama lenzi muhimu ambayo wanaipitia wanaitazama dunia. Kama aina ya ushirika, sinodi inatufundisha kuzingatia mitazamo ya wengine, badala ya kutegemea yetu wenyewe. Inatuhimiza kukuza mitazamo pana inayoheshimu ugumu bila kuchanganyikiwa, na kutafuta ukweli bila hofu ya mzozo. Katika suala hilo Papa alipenda, kutoa shukrani zake  kwa mipango mingi ambayo wanashiriki, hasa mpango wa "Ndoto Nne" unaoendelezwa na Tume ya Kipapa ya Amerika Kusini na kuhuishwa na maono ya Papa Francisko. Katika Wosia wa Kitume Querida Amazonia, alitualika kuota pamoja upya wa kikanisa, ikolojia, kijamii na kiutamaduni.

Picha ya pamoja
Picha ya pamoja   (@VATICAN MEDIA)

Ni muhimu sana tujitoe kwa bidii katika ndoto hizi, hasa katika nyakati zilizojaa dhuluma, vurugu na vita! Leo hii, jukumu lao kama viongozi lina jukumu maalum kwa kazi ya ujenzi wa amani. Jukumu hili halihusu tu uhusiano kati ya mataifa, bali pia sehemu halisi za maisha ya kila siku: wanapoishi, wanaposoma, na wanapofanya kazi. “Ikiwa hatuwezi kukuza maelewano ndani ya chuo kikuu au mahali pa kazi, au miongoni mwa vyama vya siasa na vyama vya kiraia, tunawezaje kutumaini kujenga amani ndani ya jamii nzima, au kati ya watu na mabara? Papa alisisitiza kuwa “Kwa mioyo safi na akili safi, tafuteni amani daima — kama zawadi, agano na ahadi. Amani, kiukweli, kwanza kabisa ni zawadi. Tunaipokea kutoka kwa wale waliotutangulia, na kwa hili tunapaswa kushukuru. Amani pia ni agano, ambalo hutufungamanisha sisi kwa sisi na kutufanya tuilinde pale ilipo na kuifuatilia pale ilipo. Hatimaye, amani ni ahadi, kwa sababu inatufungulia tumaini la ulimwengu bora, tumaini linaloshirikishwa na watu wote wenye mapenzi mema.

Wanasiasa vijana kutoka Ulimwenguni
Wanasiasa vijana kutoka Ulimwenguni   (@Vatican Media)

Siasa ina jukumu:kufanya kazi na kuruhusu raia wote kushiriki maisha ya kitaasisi ya mataifa yao

Siasa ina jukumu muhimu katika kazi hiyo. Kwa sababu hiyo, Papa aliwahimiza “kufanya kazi pamoja katika kujifunza aina za ushiriki zinazowaruhusu raia wote, wanaume na wanawake sawa, kushiriki katika maisha ya kitaasisi ya mataifa yao. Juu ya msingi huo, inawezekana kujenga udugu huo wa ulimwengu ambao tayari unaanza kujitokeza miongoni mwao vijana, ishara ya enzi mpya.

Askofu wa Roma kwa vijana hao wanasiasa aliwaeleza kuwa “Kiukweli, kujitolea kwao kunafikia utimilifu wake wa hali ya juu kunapomtumikia mwanadamu anayetafuta na kupata amani kupitia haki. Kwa kuzingatia hilo Papa aliwaalika kutafakari “ukweli kwamba hakuwezi kuwa na amani huku ubinadamu ukipigana vita dhidi yake,  kwa kuwatupa wanyonge, kuwatenga maskini, na kubaki bila kujali wakimbizi na wanaokandamizwa.” Ni wale tu wanaowajali walio wadogo kati yetu ndio wanaoweza kutimiza yaliyo makubwa kweli. Katika muktadha huo Papa alimkumbuka, Mama Teresa wa Calcutta ,  mtakatifu wa "maskini zaidi kati ya maskini" na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, ambaye alisema kwamba "mharibifu mkuu wa amani leo ni utoaji mimba" (taz Hotuba ya Maombi ya Kitaifa, 3 Februari 1994).

Wanasiasa vijana kutoka Ulimwenguni
Wanasiasa vijana kutoka Ulimwenguni   (@Vatican Media)

“Maneno yake yanabaki kuwa ya kinabii. Hakuna sera inayoweza kuwahudumia watu kikweli ikiwa inawanyima watoto ambao hawajazaliwa zawadi ya uzima, au ikiwa inapuuza kuwasaidia wale wanaohitaji, iwe katika hali zao za kimwili au katika dhiki yao ya kiroho. Katikati ya changamoto nyingi za wakati wetu, jipeni ​​moyo! Kumbukeni kwamba hamko peke yenu katika kutafuta udugu wa ulimwengu wote,”Papa Leo  XIV aliwashauri.

“Mungu mmoja aliyetukabidhi Sayari:Ubinadamu Mmoja, Sayari Moja,"

Mungu mmoja ambaye ametukabidhi dunia kama makao ya pamoja kwa watu wote; kwa hivyo, kichwa cha mkutano wenu, "Ubinadamu Mmoja, Sayari Moja," kinapata usemi wake kamili kinapokamilishwa na maneno "Mungu Mmoja." Kwa kumtambua ndani yake Muumba wetu mwenye upendo na ukarimu, tamaduni zetu za kidini zinatuita kuchangia maendeleo ya kijamii kwa kutafuta kila wakati mema ya pamoja, ambayo yanategemea misingi imara ya amani na haki. Kwa imani hiyo kutoka moyoni mwake, Papa aliwapa  Baraka yake ya Kitume vijana wote, wale wanaowasindikiza na wapendwa wao.

Papa na Vijana
Papa na Vijana   (@Vatican Media)
PAPA NA WANASIASA VIJANA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

31 Januari 2026, 13:45