Tafuta

Moja ya Picha ya Papa akiwa ndani ya Ukumbi wa Paulo VI. Moja ya Picha ya Papa akiwa ndani ya Ukumbi wa Paulo VI.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kwa La Repubblica:Vyombo vya habari vitende kwa uwazi,haki na huru!

Papa Leo XIV alituma ujumbe kwa gazeti La Repubblica likiwa linaadhimisha miaka 50,tangu kuanzishwa kwake.Anakumbusha kwamba limejikita katika jiji la Roma,Jimbo la Papa na kuhimiza kuendelea kutafsiri ukweli kwa uhuru,likikaribisha maoni mbalimbali:"Natumaini mtajenga mawasiliano huru na ya mazungumzo kila wakati,yakiongozwa na utafutaji wa ukweli,bila ubaguzi na kutoa fursa ya majadiliano ambayo,yasipokuwa ya uadui,yanachangia kwa manufaa ya wote na umoja wa wanadamu.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Uhusiano wa kudumu na wasomaji, uhuru kama kigezo cha kusimulia miaka hamsini ya historia ya Italia, dunia, na Kanisa, mazungumzo kama njia ya upendeleo ya kujenga amani. Ndiyo maneno yanayosikia ya Baba Mtakatifu Leo XIV aliyoandika na mengi katika ujumbe wake kwa Mario Orfeo, mhariri mkuu wa La Repubblica, Gazeti la kila siku la Italia ulioandikwa katika fursa ya kuadhimisha kumbukumbu muhimu inayoadhimishwa siku hizi ya miaka hamsini.

Ilikuwa mnamo tarehe 14 Januari 1976, toleo la kwanza la gazeti lililoanzishwa na Eugenio Scalfari lilichapishwa. Scalfari alibaki kama mhariri hadi 1996, kisha akachangia kama mwandishi wa tahariri hadi kifo chake. Kwa njia hiyo kutoka Vatican, tarehe 14 Januari  2026, Papa anaandika kuwa “Mhariri Mpendwa, ninafurahi kutoa matashi  yangu mema kwako na kwa waandishi wa habari wa La Repubblica katika maadhimisho ya miaka hamsini ya kuanzishwa kwa gazeti lako.

Kukuza uhusiano na wasomaji

Papa aliendelea kuwa “Kila siku mmesimulia historia ya nusu karne, mkikuza uhusiano na wasomaji wenu ambao wamewafikisha hapa. Gazeti lenu limejikita katika miji mingi, lakini lenye makao yake makuu mjini Roma, Jimbo la Papa, ni sehemu yenye upendeleo wa matukio nchini Italia na duniani.”

Kusimulia Historia ya Kanisa ndiyo maana ya huru licha ya tofauti

Baba Mtakatifu katika barua hiyo aliongeza kusema: “Mmesoma kurasa za miaka hii hamsini kwa uhuru. Na mmesimulia historia ya Kanisa. Hii ndiyo maana ya uhuru wa vyombo vya habari: licha ya utofauti wa maoni, mitazamo, na tamaduni, lazima kila mara mtende kwa uwazi na haki, na kutoa fursa ya majadiliano ambayo, yasipokuwa ya uadui, yanachangia kwa manufaa ya wote na umoja wa wanadamu.”

Papa Leo XIV kwa kuhitimisha alibainisha, “kwa hivyo mazungumzo yanapita yasiyojulikana na hujenga amani. Natumaini mtajenga mawasiliano huru na ya mazungumzo kila wakati, yaliyoongozwa na utafutaji wa ukweli na bila ubaguzi. Heri ya kumbukumbu ya miaka 50!”

Papa kwa La Repubblica

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

15 Januari 2026, 09:25