Papa Leo XIV:Sisi ni wamoja!Tayari tuko pamoja!Tutambue na kuonekana!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV, aliongoza Masifu ya jioni katika Basilika ya Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta mjini Roma, Dominika tarehe 25 Januari 2026 ambayo yalihitimisha Juma la 59 la Kuombea Umoja wa Wakristo, sambamba na sherehe ya kuongoka kwa Mtume wa Mataifa, Mtakatifu Paulo. Baada ya sala na somo, Baba Mtakatifu Leo XIV alianza mahubiri yake kwa ndugu wa Makanisa tofauti na ushirika wa Kikristo waliokuwa katika Kanisa Kuu hilo alisema: “Wapendwa kaka na dada, katika mojawapo ya vifungu vya Maandiko ambavyo tumesikia hivi punde, Mtume Paulo anajiita "mdogo zaidi kati ya mitume" (1 Kor 15:9). Anajiona hastahili cheo hiki kwa sababu hapo awali alikuwa mtesaji wa Kanisa la Mungu. Hata hivyo, yeye si mfungwa wa wakati huo uliopita, bali ni "mfungwa katika Bwana" (Efe 4:1).”
Kwa Neema ya Mungu Paulo alimjua Yesu aliyefufuka
“Kiukweli, Papa Leo XIV aliendelea, ilikuwa kwa neema ya Mungu kwamba Paulo alimjua Bwana Yesu aliyefufuka, ambaye alijifunua kwanza kwa Petro, kisha kwa Mitume wengine na kwa mamia ya wafuasi wengine wa Njiani, na hatimaye pia kwake, mtesaji (taz. 1 Kor 15:3-8). Kukutana kwake na Bwana aliyefufuka kulileta uongofu tunaoukumbuka leo hii. Kina cha uongofu huu kinaonekana katika mabadiliko ya jina lake kutoka Sauli hadi Paulo. Kwa neema ya Mungu, yule aliyemtesa Yesu hapo awali amebadilishwa kabisa kuwa shuhuda wake.” Yule ambaye hapo awali alipinga vikali jina la Kristo sasa anahubiri upendo wake kwa bidii kubwa, kama ilivyoelezwa wazi katika wimbo tuliouimba mwanzoni mwa sherehe hii (tazama Excelsam Pauli Gloriam, mst. 2)."
Utume wa Paulo ni utume wa Wakristo wote
“Tunapokusanyika mbele ya mabaki ya Mtume wa Mataifa, tunakumbushwa kwamba utume wake pia ni utume wa Wakristo wote leo: kumtangaza Kristo na kuwaalika kila mtu kumwekea imani yake. Kila kukutana na Bwana kiukweli ni wakati wa mabadiliko unaotoa maono mapya na mwelekeo mpya kwa ajili ya kazi ya kujenga Mwili wa Kristo (taz Efe 4:12). Mwanzoni mwa Katiba ya Mtaguso wa II wa Vatican( Second Vatican Council,)kuhusu Kanisa, ulionesha hamu yake kubwa ya kutangaza Injili kwa viumbe vyote (taz. Mk 16:15) na hivyo “kuwaletea wanadamu wote nuru ya Kristo inayong’aa juu ya uso wa Kanisa”(Lumen Gentium, 1). Ni jukumu la pamoja la Wakristo wote kusema kwa unyenyekevu na furaha kwa ulimwengu: “Mtazameni Kristo! Mkaribieni! Karibuni neno lake linaloangazia na kufariji!” (Mahubiri ya Misa ya Mwanzo wa Upapa wa Papa Leo XIV 18 Mei 2025- (Homily of the Mass for the Beginning of the Pontificate of Pope Leo XIV).
Kila Juma la Kuombea Umoja wa Kikristo ni mwaliko wa kufufua utume wetu
Papa Leo XIV alisisitiza kwa waamini waliokuwa katika Kanisa Kuu hilo kwamba, “kila mwaka Juma la Maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo linatualika kufufua kujitolea kwetu kwa ajili ya utume huu mkuu, tukikumbuka kwamba mgawanyiko kati yetu - ingawa hauzuii nuru ya Kristo kung'aa - hata hivyo hufanya uso ambao lazima uiangazie kwa ulimwengu usiwe na mwanga mwingi.” Mwaka 2025, Papa alikubusha jinsi ambavyo, “tulisherehekea kumbukumbu ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicaea. Patriaki Bartholomew, wa Kiekumeni, alitualika kusherehekea kumbukumbu hiyo huko İznik,( , invited us to celebrate the anniversary in İznik ) na hivyo Papa ameongeza kusema anavyo mshukuru Mungu kwamba, tamaduni nyingi za Kikristo ziliwakilishwa katika kumbukumbu hiyo miezi miwili iliyopita. Kukiri Imani ya Nicaea pamoja mahali pale ilipoanzishwa ilikuwa ushuhuda mkubwa na usiosahaulika wa umoja wetu katika Kristo.” Wakati huo wa udugu pia ulituruhusu kumsifu Bwana kwa yale aliyoyatimiza kupitia Mababa wa Nicaea, akiwasaidia kuelezea wazi ukweli wa Mungu aliyetukaribia katika Yesu Kristo.”
Roho Mtakatifu atupatie akili tulivu ili kutangaza imani kwa sauti moja
Roho Mtakatifu atupatie akili tulivu hata leo hii, ili tuweze kutangaza imani kwa sauti moja kwa wanaume na wanawake wa wakati wetu! Katika kifungu kutoka Barua kwa Waefeso kilichochaguliwa kama mada ya Juma la Maombi ya mwaka huu, tunasikia mara kwa mara kivumishi "moja": mwili mmoja, Roho mmoja, tumaini moja, Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, Mungu mmoja (taz. Waefeso 4:4-6). Baba Mtakatifu aliendelea kuwaeleza kuwa “maneno haya yaliyoongozwa na roho yanawezaje kutotugusa sana? Mioyo yetu haiwezi kuwaka ndani yetu tunapoyasikia? Ndiyo, “tunashiriki imani moja katika Mungu mmoja na wa pekee, Baba wa watu wote; tunasadiki pamoja Bwana mmoja na Mwana wa kweli wa Mungu, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu mmoja, anayetuongoza na kutusukuma kuelekea umoja kamili na ushuhuda wa pamoja wa Injili”(Barua ya Kitume In Unitate Fidei, 23 Novemba 2025, 12).
Tayari tupo pamoja,tutambue na tufanye uoenekane umoja
Sisi ni wamoja! Tayari tuko pamoja! Tutambue, tupate uzoefu na tufanye uonekane! Papa Leo XIV aliongeza kuwa, Mtangulizi wake Papa Francisko( Pope Francis,) alisema kwamba, safari ya sinodi ya Kanisa Katoliki "ni na lazima iwe ya kiekumeni, kama vile safari ya kiekumeni ilivyo ya sinodi”(Address to His Holiness Mar Awa III, 19 Novemba 2022). Hili lilijitokeza katika Mikutano miwili ya Sinodi ya Maaskofu mwaka 2023 na 2024, iliyooneshwa na ari kubwa ya kiekumeni na kutajirishwa na ushiriki wa wajumbe wengi wa kidugu. Ninaamini hii ni njia ya kukua pamoja katika ufahamu wa pamoja wa miundo na tamaduni zetu za sinodi. Tunapoelekea maadhimisho ya miaka 2,000 ya Mateso, Kifo na Ufufuko wa Bwana Yesu mwaka 2033, hebu tujitolee kuendeleza zaidi desturi za sinodi za kiekumeni na kushiriki sisi ni nani, tunachofanya na tunachofundisha (taz Francisko, Kwa Kanisa la Sinodi, 24 Novemba 2024, 137-138).
Shukrani za Papa
Baba Mtakatifu bado aliendelea kusema kuwa huku Juma la Kuombea Umoja wa Kikristo likikaribia kukamilika, ninatoa salamu za dhati kwa Kardinali Kurt Koch, kwa wajumbe, washauri na wafanyakazi wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo(Dicastery for Promoting Christian Unity,) na kwa wajumbe wa majadiliano ya kitaalimungu na mipango mingine inayoendelezwa na Baraza la Kipapa hilo. Ninashukuru kwa uwepo katika Liturujia hii wa viongozi wengi na wawakilishi wa Makanisa mbalimbali na Ushirika wa Kikristo duniani kote, hasa Metropolitan Polykarpos, wanaowakilisha Upatriaki wa Kiekumeni, Askofu Mkuu Khajag Barsamian, kutoka Kanisa la Kitume la Armenia, na Askofu Anthony Ball, kwa niaba ya Ushirika wa Kianglikani. Pia nawasalimu wanafunzi wa ufadhili wa masomo wa Kamati ya Ushirikiano wa Kiutamaduni na Makanisa ya Kiorthodox na ya Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki kutoka Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo, wanafunzi wa Taasisi ya Kiekumeni ya Bossey ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni, pamoja na vikundi vya kiekumeni na mahujaji wanaoshiriki katika sherehe hii.”
Vifaa vya kutumia kwa Juma la Maombi 2026,vimetayarishwa na Makanisa ya Armenia
Vifaa vya Juma la Maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo vya mwaka huu 2026 vilitayarishwa na Makanisa nchini Armenia. Kwa shukrani kubwa, tunakumbuka ushuhuda wa Kikristo wa ujasiri wa watu wa Armenia katika historia yote, historia ambayo mauaji ya kishahidi yamekuwa sifa ya kudumu. Tunapomalizia Juma hili la Maombi, tunaheshimu kumbukumbu ya Mtakatifu Nersès Šnorhali “Mwenye Rehema,”Kiongozi Mkuu aliyefanya kazi kwa ajili ya umoja wa Kanisa katika karne ya 12. Alikuwa mbele ya wakati wake katika kuelewa kwamba kutafuta umoja ni kazi iliyokabidhiwa waamini wote, na kwamba inahitaji uponyaji wa kumbukumbu.
Mtakatifu Nerses anatufundisha kufuata safari yetu ya kiekumeni
Kama mtangulizi wangu Mheshimiwa Mtakatifu Yohane Paulo II alivyokumbusha kwamba, Mtakatifu Nerses pia anatufundisha mtazamo tunaopaswa kuufuata katika safari yetu ya kiekumeni: “Wakristo lazima wawe na imani kubwa ya ndani kwamba umoja ni muhimu, si kwa faida ya kimkakati au faida ya kisiasa bali kwa ajili ya kuhubiri Injili” (Mahuburi katika Sherehe ya Kiekumeni, 26 Septemba 2001-Homily at the Ecumenical Celebration). Kulingana na utamaduni, Armenia ilikuwa taifa la kwanza la Kikristo, baada ya Mfalme Tiridates kubatizwa na Mtakatifu Gregori aliyeangaziwa katika mwaka 301. Tunatoa shukrani kwa watangazaji jasiri wa Neno la wokovu walioeneza imani katika Yesu Kristo kote Mashariki na Magharibi mwa Ulaya. Tunaomba kwamba mbegu za Injili ziendelee kuzaa matunda katika bara hili kwa umoja, haki na utakatifu, kwa faida ya amani miongoni mwa watu na mataifa ya ulimwengu mzima.”
