Papa Leo XIV:kila wakati ni mzuri wa kutangaza Injili ya Bwana!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Ikiwa ni “Dominika ya tatu ya Kipindi cha Kawaida, ni Dominika ya Neno la Mungu ambayo ilianzishwa na Papa Francisko miaka saba iliyopita ili kuhamaisha maarifa ya Maandiko Matakatifu katika Kanisa na kuzingatia Neno la Mungu, katika liturujia na katika maisha ya jumuiya, pia ni hitimisho la Juma la Kuombea Umoja wa Kristo wakati Mama Kanisa akikumbuka Uongofu wa Mtakatifu Paulo Mtume wa watu, Dominika tarehe 25 Jannauri 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV alitoa tafakari yake kwa waamini wengi na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, asubuhi iliyokuwa inaonekana kuwa na mvua, lakini matokea yakawa kwa Waamini wengi kuwa chini ya anga la blu na mawingi meupe katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Baba Mtakatifu aliwageukia akiwasalimia na kuwatakia Dominika njema!
Papa aliendelea “Mara baada ya kupokea Ubatizo, Yesu alianza kuhubiri kwake na kuwaita mitume wa kwanza , Somoni, aitwaye Petro, Andrea, Yakobo na Yohane(Mt 4,12-22). Kwa kutazama muktadha huu kwa karibu, wa Injili ya leo, tunaweza kujiuliza maswali mawili: moja kuhusu wakati ambao Yesu alianzisha utume na jingine kuhusu mahali ambapo anachagua kwa ajili ya kuhubiri na kuwaita mitume. Tujiulize: alianza lini” ni wapi alianzia? Awali ya yote Mwinjili anatueleza kuwa Yesu alianza kuhubiri kwake, wakati aliposikia kwamba Yohane alikuwa amefungwa (Mt 4, 12): Kwa njia hiyo ulitokea wakati ambao haukuwa mwafaka: Mbatizaji wakati huo punde alikuwa amefungwa, kwa hiyo viongozi wa watu hawakuwa tayari kusikiliza mapya ya Masiha. Hii ilikuwa na maana ya wakati ambao unahitaji busara, na kinyume chake ni katika hali hiyo ya giza ambayo Yesu alianza kupeleka mwanga wa habari njema kuwa: “ Ufalme wa Mungu huko Karibu (Mt 14,17).
Papa aliongeza kusema kuwa “Hata katika maisha yetu kibinafsi na ya kikanisa, wakati mwingine kutokana na upinzani wa ndani au hali ambazo hatukuona kuwa nzuri, sisi tunafikiria kuwa siyo wakati mwafa kwa ajili ya kutangaza Injili, kuchukua maamuzi, kufanya uchaguzi na kwa kubadili hali fulani. Hatari lakini ni ile ya kubaki umezuiwa katika kufanya maamuzi au kubaki mfugwa kwa kuwa na busara kupita kiasi, wakati Injili inatuomba tuthubutu kwa imani: Mungu ndiye anatenda katika kila wakati, kila muda wowote ule ni mwema kwa ajili ya Bwana, hata kama sisi hatuhisi kuwa tayari au katika hali ambazo utafikiri hazifai. Simulizi ya Kiinjili inatufanya tuone hata mahali ambapo Yesu alinzia utume wake kwa umma: Yeye alitoka Nazareh na kwenda kukaa huko Kapernaumu(Mt 14,13). Alibaki hata hivyo Galilaya, katika eneo ambalo hasa waliishi wapagani, kwa sababu ya biashara na hata ilikuwa ardhi ya kupitia na ya mikutano; tunaweza kusema kuwa ilikuwa eneo la tamaduni nyingi zilizopitia na watu kutoka sehemu mbali mbali na zenye tabia za dini mbali mbali.
Kwa mtindo huo, Injili inatueleza kuwa Masiha anakuja kutoka Israeli, lakini anavuka mipaka ya ardhi yake ili kuweza kutangaza Mungu ambaye anajifanya kuwa karibu kwa wote, na ambaye habagui yeyote, ambaye hakuja kwa ajili ya wema tu, bali badala yake anajichanganya katika hali na katika mahusiano ya kibinadamu. Hata sisi Wakristo, kwa namna hiyo tunapaswa kushinda kishawishi cha kujifungia: Injili kwa dhati inapaswa kutangazwa na kuiishi kwa kila muktadha na kwa kila mazingira, ili udugu na amani vieweze kuwa chachu kati ya wat , kati ya tamaduni, dini na watu. Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV alisisitiza kuwa kama mitume wa kwanza tunaitwa kupokea wito wa Bwana katika furaha ya kujua kuwa, kila wakati na kila mahali pa maisha yetu vinatembelewa na Yeye na kupitiwa na upendo wake. Tuombe Bikira Maria, ili aweze kutujalia imani hii ya kina na kutusindikiza katika safari.
