Tafuta

Papa Leo XIV:Baba anatufanya kuwa wa haki kwa njia ya Kristo,Mwokozi!

Kama nuru katika giza,Bwana anajifanya kupatikana pale ambapo hatukutegemea:Ni Mtakatifu kati ya wadhambi,anayetaka kuishi katikati yetu bila kuweka umbali,badala yake anawajibika kwa kwa kuwa yote ya kina ambayo ni ya kibinadamu.“Haki ya Mungu ambaye katika Ubatizo wa Yesu anatenda kwa ajili ya haki yetu: katika huruma yake isiyo na kikomo.Ni mahubiri ya Papa katika Sherehe za Utabatizo wa Bwana,Januari 11 na kuwabatiza watoto 20 wa wafanyakazi wa Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Kikanisa cha Sistine mjini Vatican,  katika Sherehe za Ubatizo wa Bwana, na kuwabatiza watoto ishirini ambao ni wa wafanyakazi, Dominika tarehe 11 Januari 2026. Akianza mahubiri yake kwa kuongozwa na Injili iliyosomwa, alisema wakati Bwana anaingia katika historia, anakuja kukutana na maisha ya kila mmoja kwa moyo ulio wazi na mnyenyekevu. Yeye anatafuta mtazamo wetu kwa mtazamo wake uliojaa upendo, na anazungumza nasi kwa kutonesha Neno la Wokovu. Aliyefanyika mwanadamu, Mwana wa Mungu  anatimiza kwa wote, uwezekano wa kushangaza, ambao unazindua wakati mpya na matarajio tangu manabii.”

Mshumaa wa Pasaka katika ishara ya Ubatizo
Mshumaa wa Pasaka katika ishara ya Ubatizo   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV alidadavua kuhusu hilo kuwa, “aligundua haraka Yohane Mbatizaji, ambaye anauliza Yesu: “Ni mimi ninayehitaji kubatizwa na wewe, na wewe unakuja kwangu?(Mt 3,4).  Kama nuru katika giza, Bwana anajifanya kupatikana pale ambapo hatukutegemea: Ni Mtakatifu kati ya wadhambi, ambaye anataka kuishi katikati yetu bila kuweka umbali, badala yake anawajibika kwa kwa kuwa yote ya kina ambayo ni ya kibinadamu. “Acha afanye,” Yesu alijibu Yohane, “kwa sababu inafaa kutimiza kila haki (Mt 3,15).”

Kubariki maji
Kubariki maji   (@Vatican Media)

Katika hilo, Papa aliuliza swali: “Je ni haki gani? Ile ya Mungu, ambaye katika Ubatizo wa Yesu anatenda kwa ajili ya haki yetu: katika huruma yake isiyo na kikomo, Baba anatufanya kuwa wenye haki kwa njia ya Kristo wake, Mwokozi pekee wa wote. Je hilo linatokeaje? Yule aliyebatizwa na Yohane katika Jordan, anafanya ishara hiyo, alama mpya ya kifo na ufufuko, ya msamaha na muungano. Na ndiyo Sakramenti ambayo tunaadhimisha kwa watoto hawa: kwani Mungu anawapenda, ndani mwao wanageuka kuwa wakristo, kaka na dada zetu.”

Ubatizo wa watoto
Ubatizo wa watoto   (@VATICAN MEDIA)

Baba Mtakatifu akiwageukia wazazi wa watoto aliwaeleza kwamba “watoto mliowashikilia mikononi, wamegeuka kuwa viumbe vipya. Kama ninyi wazazi mlipokea uhai, ndiyo sasa mnapokea maana ya kuuishi: yaani Imani. Tunapotambua kuwa wema ni msingi, kwa haraka tunautafuta kwa ajili ya wale ambao tunawapenda. Ni nani kati yetu kiukweli, angeweza kuacha mtoto aliyezaliwa bila nguo au bila chakula, kwa subira kwamba akiwa mzima achague namna ya kujivarisha, na nini cha kuweza kula? Kwa  hiyo Papa aliongeza,  “Ikiwa chakula na nguo ni vya lazima ili kuishi, imani ni zaidi ambayo ni ya lazima, kwa sababu kuwa na Mungu, maisha yanapata wokovu.”

Misa ya Ubatizo katika kikanisa cha Sistine mjiniVatican
Misa ya Ubatizo katika kikanisa cha Sistine mjiniVatican   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV aliwalekea wazazi tena kwamba, “Majaliwa ya “Upendo wake, unajionesha duniani kwa njia yenu, mama na baba ambao mnaomba imani kwa ajili ya watoto wenu. Hakika, itafika siku ambayo watakuwa wazito  kuwanyanyua mikononi: na itafika siku ambayo hata wao wataweza kuwasaidia ninyi. Ubatizo ambao unatuunganisha katika familia moja ya Kanisa, utakatifuze kila wakati familia zenu zote, kwa kuwapatia nguvu na upendo wa dhati ambao unawaunganisha.”

Kuzaliwa upya katika Kristo
Kuzaliwa upya katika Kristo   (@Vatican Media)

Kwa kuelezea kile ambacho kinahusu ubatizo, Papa Leo alisema, “Ishara ambazo muda mfupi tutatimiza ni ushuhuda mzuri sana: maji ya kisima ni osheo la Roho, ambalo linatakasa kila dhambi; nguo nyeupe ni Vazi jipya ambalo Mungu Baba anatupatia kwa ajili ya siku kuu ya Milele ya Ufalme wake; mshumaa uliowaka kutoka Mshumaa wa Pasaka ni mwanga wa Kristo mfufuka ambaye anaangaza safari yetu. Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu alisema “ Ninawatakia muendelee na furaha ya mwaka mefu ambao umeanza hivi karibuni na kwa maisha yote, kwa hakika kwamba Bwana anatasindikiza daima hatua zenu.”

Mwishoni mwa misa, Baba Mtakatifu Leo XIV aliwazawadia wazazi wa watoto medali inayoonesha picha ya Bikira Maria.

Papa akitoa zwadi kwa wazazi wa watoto Medali ya Bikira Maria
Papa akitoa zwadi kwa wazazi wa watoto Medali ya Bikira Maria   (@Vatican Media)
mahubiri Papa Sistine

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

11 Januari 2026, 11:00