Tafuta

2026.01.30 Wajumbe wa Mtando wa kimataifa wa Sala ya Papa 2026.01.30 Wajumbe wa Mtando wa kimataifa wa Sala ya Papa   (@Vatican Media)

Papa Leo akutana na wakuu wa Mtandao wa Sala ya Papa:Funda kizazi kwa maombi!

Papa Leo XIV alikutana na wakuu na wajumbe wa Mtandao wa Kimataifa wa sala na kuwasifu kwa utajiri wa utamaduni wa lugha na karama za Kazi za Kipapa.Alishukuru pia kwa ajili ya uenezaji wa Nia za Maombi ambazo zinakabiliana na changamoto za ubinadamu na utume wa Kanisa,kati ya Mamilioni ya waamini wanajiunga kwenye mtando huo:“Lazima kuwafunda vijana kuwa waombezi kwa mahitaji ya ulimwengu.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana, Ijumaa tarehe 30 Januari 2026, katika Ukumbi wa Mapapa katika Jumba la Kitume la Vatican na Wakuu na wajumbe wa Mtandao wa Kimatifa wa maombi ya Papa ambapo pamoja na mengine aliyosema ni kuhusu mahitaji ya ulimwengu ujao yanavyoelekezwa kwa vijana na kwamba labda hii pia ndiyo sababu wengi wao wanahisi hamu ya uhusiano wa kina na wa kibinafsi zaidi na Yesu Mfufuka. Katika upeo huo, njia inayoweza kuakisi barabara ya kuunganisha tamaduni, lugha. Awali ya yote Papa Leo XIV alianza na ishara ya Msalaba na kuwatakia amani. Waliniambia nizungumze Kiingereza, je, ni sawa? Nadhani nitafanya niwezavyo. Habari za asubuhi na karibu kwenu nyote, ninafurahi kukutana nanyi na kuwashukuru kwa huduma yenu kwa watu wa Mungu.”

MTANDAO KIMATAIFA WA NIA ZA PAPA
MTANDAO KIMATAIFA WA NIA ZA PAPA   (@Vatican Media)

Papa aliendelea kuwasalimia kwa  dhati Mkurugenzi wa Kimataifa wa Mfuko wa Mtandao Sala ya Papa Ulimwenguni, Padre Cristóbal Fones, pamoja na Bi. Bettina Raed na Padre Miguel Melo, Makamu Wakurugenzi. Pia aliwawakaribisha wote  ambao ni wanachama wa Ofisi ya Kimataifa, Waratibu, Bodi ya Wakurugenzi, washirika wa kudumu, na, kwa njia ya pekee, Mabalozi wa Mfuko huo wanaounga mkono utulivu na uhai wa utume huo kwa ukarimu wao. Kama wanavyojua, kila mwezi, baada ya utambuzi makini,  Papa aliongeza “mimi na watangulizi wangu tumeshiriki nanyi nia mbalimbali zinazogusa changamoto zinazowakabili wanadamu pamoja na maisha na utume wa Kanisa.”

MTANDAO WA KIMATAIFA WA NIA ZA MAOMBI YA PAPA
MTANDAO WA KIMATAIFA WA NIA ZA MAOMBI YA PAPA   (@Vatican Media)

Kwa njia hiyo alishukuru kwa juhudi zao za kuzisambaza kwa makumi ya mamilioni ya watu katika mtandao huu wa dunia nzima ambao kila siku huwasilisha mahitaji haya mbele za Mungu. Maombi kama hayo si nje ya kazi ya kiinjili ya Mwili wa Kristo, bali ni sehemu muhimu yake.” Kiroho cha utume wao wa maombi kimejikita katika Moyo wa Yesu, ambao huwaruhusu kumjua Bwana wetu kwa undani zaidi na kuwa na huruma na upole  zaidi wanapotoa msaada wa maombi kwa wale wanaohitaji. Katika suala hilo Papa aliongeza kwamba ratiba yao ya malezi, Njia ya Moyo, ni mwongozo muhimu wa jinsi ya kuishi kiroho hiki katika maisha ya kila siku. “Ni matumaini yangu kwamba kupitia utume wenu mtaendelea kuwasaidia waliobatizwa kuelewa kwamba wao ni marafiki na mitume wa Kristo.”

PICHA YA PAMOJA
PICHA YA PAMOJA   (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV vile vile aliwahimiza “kukuza ushiriki mkubwa zaidi katika Mtandao huu, unaounganisha tamaduni, lugha, na karama mbalimbali katika utume wa pamoja. Ni muhimu sana kuwaalika vijana kushiriki ili waweze kuunda kizazi kijacho cha waombezi kwa mahitaji ya ulimwengu mzima. Kwa kuwa wengi wao wanatafuta uhusiano wa kina na wa kibinafsi na Yesu Mfufuka, Harakati yenu ya Vijana ya Ekaristi inaweza kuwa njia yenye matunda hasa ya kuwasaidia kukua katika ukaribu wa kina na Bwana wetu.” Papa aliwashukuru tena kwa dhati kwa juhudi zao za kuhamasisha maombi duniani kote kwa ajili ya nia ya Papa, na kuwatia moyo kuendelea katika njia hii kwa roho ya furaha. Aliwapita  Baraka yake ya Kitume, kwa furaha ambayo pia aliwapatia  wanachama wote wa Mtandao huo. Papa alihitimisha kwa sala ya Pamoja ya Baba, Yetu na baraka , baadaye, aliongeza: "Muwe na siku njema, asante tena kwa huduma yenu na kujitolea kwenu katika huduma hii muhimu, asante.”

PAPA MTANDAO KIMATAIFA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

30 Januari 2026, 12:50