Tafuta

Msumbiji imekumbwa na mafuriko makubwa baada ya majuma kadhaa ya mvua kubwa. Msumbiji imekumbwa na mafuriko makubwa baada ya majuma kadhaa ya mvua kubwa. 

Papa Leo XIV:'Mawazo yangu yanawaendea watu wapendwa wa Msumbiji'

Mara baada ya katekesi yake ya Kila Juma Jumatano Januari 28, Papa Leo XIV aliwakumbuka "watu wapendwa wa Msumbiji," waliokumbwa na mafuriko makubwa, na alitoa sala zake kwa ajili ya waathiriwa na kuwahakikishia ukaribu wake na wapendwa wao, waliohamishwa makazi, na wafanyakazi wa uokoaji.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Leo XIV alieleza mawazo yake kwa waliopata na maafa mara baada ya Katekesi yake  ya kila, Jumatano tarehe 28 Januari 2026,  kwa waamini na mahujaji waliokuwa katika Ukumbi wa Paulo wa VI mjini Vatican. Akitoa salamu zake kwa wanaozungumza Kireno, aliwakumbuka wale walioathiriwa na janga la asili nchini Msumbiji.

“Mawazo yangu yanawaendea hasa watu wapendwa wa Msumbiji, ambao wamekumbwa na mafuriko makubwa. Ninapowaombea waathiriwa,  na ninaelezea ukaribu wangu kwa wale ambao wamehamishwa makazi yao na kwa wote wanaowapa msaada," Papa alisema, huku akiongeza, "Bwana awasaidie na awabariki!"

Mafuriko kutokana na mvua nyingi nchini Msumbiji
Mafuriko kutokana na mvua nyingi nchini Msumbiji

Inasadikika kuwa watu 137 wamefariki na takriban 812,000 wameathiriwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Msumbiji tangu Oktoba 2025. Taasisi ya Kitaifa ya Usimamizi wa Maafa (INGD) iliripoti Jumanne Januari 27, huku ikitoa takwimu kuhusu janga hilo. Nchi hiyo iliyo kusini mashariki mwa Afrika kwa sasa iko katika kilele cha msimu wa mvua, ambao ulianza Oktoba 2025 na unatarajiwa kuisha mnamo Machi 2026.

Kuhamishwa kwa watu kutokana na mvua kali Msumbiji
Kuhamishwa kwa watu kutokana na mvua kali Msumbiji   (AFP or licensors)

Wakati huo huo, akizungumza na  mahujaji wa Poland, Papa alikumbusha kwamba miaka thelathini na mitano imepita tangu kurejeshwa kwa Ofisi ya Kijeshi ya Poland, "ambayo kazi yake," alisema, "ni kuunda dhamiri za wale waliojitolea kwa utumishi wa Mungu na wa Nchi mahalia."

Katika muktadha huo, Papa Leo alisema, "Uaminifu kwa Neno la Mungu na kwa Mapokeo ya Kanisa uwe dira ya huduma ya kichungaji, hasa katika utoaji wa sakramenti katika hali ya majaribu na ukosefu wa usalama ni muhimu.”  

Vile vile aliwaalika mahujaji wanaozungumza Kiarabu "kulinda amana ya imani na kuiwasilisha kwa uaminifu, daima wakiwa wameangazwa na Roho Mtakatifu anayeongoza Kanisa kuelekea utimilifu wa ukweli."

Mahujaji kutoka sehemu mbali mbali
Mahujaji kutoka sehemu mbali mbali   (@Vatican Media)

Akizungumza kwa mahujaji wanaozungumza Kifaransa, Papa alikumbusha kwamba Kanisa leo hii 28 januari inaadhimisha ukumbusho wa Mtakatifu Thomas wa Aquinas, Mwalimu wa Kanisa.  Kwa njia hiyo aliomba kwamba Mtakatifu mpendwa "atuongoze katika uelewa wa Maandiko, ambayo aliyatoa maoni yake kwa hekima kubwa, ili tuweze kuelewa jinsi Mungu anavyotupenda na kutamani wokovu wetu."

Baada ya Katekesi: 28 Januari

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

28 Januari 2026, 13:35