Papa kwa mapadre na waseminari Wafocolari:Kuweni mashuhuda wa matumaini
Vatican News
Wakati mara mbili pamoja na Papa, mawasiliano ya moja kwa moja na kisha kama wapokeaji wa salamu iliyopokelewa kutoka katika umati kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro. Huu ulikuwa uzoefu wa waseminari 35 na mapadre vijana wa majimbo kutoka nchi 18 na mabara manne, wanachama wa Harakati ya Wafocolari, walioshiriki katika mkutano huko Castel Gandolfo kuanzia Desemba 26 hadi 30 kuhusu mada ya "Kuishi Ukaribu," iliyoongozwa na maneno Papa Leo XIV aliyowaandikia waseminari wakati wa Jubilei kuwa: "Leo, katika muktadha wa kijamii na kiutamaduni uliojaa migogoro na kujipenda, tunahitaji kujifunza kupenda na kufanya hivyo kama Yesu."
Mwaliko wa Papa
Mnamo tarehe 29 Desemba 2025 akiwa huku Castel Gandolfo, kama kawaida anavyofanya kati ya Jumatatu na Jumanne za majuma haya, Papa mwenyewe aliwakaribisha nyumbani kwake ili kusalimiano na kila mmoja wao kuwa kupenana mikono na kuwatia moyo katika huduma ambayo wamejiweka wakfu au wanajiandaa kufanya hivyo.
Akithamini fursa ya uwepo wao huko Roma kwa ajili ya hija mwishoni mwa Jubilei, Papa Leo XIV aliwaalika "kutafuta zawadi ya matumaini" na kuwa mashahidi wake "mtakaporudi katika nchi zenu za asili." Hata baada ya Sala ya Bwana Dominika tarehe 28 Desemba 2025, Papa alirudia kueleza kuwa: "Sote tutembee pamoja, tukijitahidi kuwa mashahidi na tumaini kila siku."
Kongamano
Wakati wa Kongamano, mawasilisho na ushuhuda vilishughulikia changamoto za maisha ya seminari leo, hususan mada za ukaribu na hisia, kutafsiri vipengele vya wito kwa kuzingatia karama ya umoja ambayo ndiyo msingi wa Harakati iliyoanzishwa na Chiara Lubich. Rais wa Harakati hiyo, Margaret Karram, alishirikiana na washiriki wa kongamano na kujibu maswali, akiwatia moyo waumbwe na Neno, Ekaristi, na roho ya huduma, ili wawe makuhani walio wazi kwa ushirika.
Wakati wa kongamano, hilo kadhalika mapadre na waseminari walipata siku ya hija iliyowapeleka kwenye Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu na kwenye kaburi la Papa Francisko, kisha hhadi Mtakatifu Petro ili kushiriki ksala Malaika wa Bwana na hivyo Jumatano tarehe 31 Desemba 2025 wakashiriki Katekesi ya mwisho ya mwaka na Papa Leo XIV.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here
