Tafuta

2026.01.15 Papa akutana na wanafamilia wa vijana waliokufa na kujeruhiwa kwa ajali ya moto  huko Crans-Montana-Uswiss. 2026.01.15 Papa akutana na wanafamilia wa vijana waliokufa na kujeruhiwa kwa ajali ya moto huko Crans-Montana-Uswiss.  (@Vatican Media)

Papa kwa familia za wahanga wa Crans-Montana:maumivu ni mengi,nimeguswa sana

Papa Leo XIV alikutana wazazi na jamaa za vijana wa Italia waliouawa au kujeruhiwa na wengine wengi wakati wa janga kubwa sana la moto lililotokea katika klabu ya usiku katika mji wa Uswiss usiku wa Mwaka Mpya. Papa aliwahakikishia ukaribu wake na sala zake,pamoja na zile za Kanisa zima: "Mapenzi na maneno ya huruma ya kibinadamu ninayowaambia leo yanaonekana kuwa machache sana na hayana nguvu,lakini Mrithi wa Petro anathibitisha kwa nguvu:tumaini lenu si bure."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, Alhamisi tarehe 15 Januari 2026, alikutana na wazazi na jamaa wa vijana waliofariki katika Eneo la Mlimani huko Crans -Montana. Katika fursa hiyo Papa hakusitia kuonesha  hisia zake, mbele ya janga kubwa sana huko mji wa Uswiss ambapo moto katika klabu ya usiku siku ya Mkesha wa Mwaka Mpya uliua watu 40 na kuwajeruhi 116. Wengi wao walikuwa vijana sana, wakiwemo watoto wadogo. Baada ya siku kumi na tano ya mkasa huo, huku uchunguzi kuhusu hali hiyo ukiendelea na maombi na matumaini yote yanatolewa kwa ajili ya kupona kwa majeruhi waliolazwa hospitalini (kwa Waitaliano, vijana kumi na wawili kwa sasa wanatibiwa katika Hospitali ya Niguarda huko Milano, saba kati yao wako katika chumba cha wagonjwa mahututi),  Papa Leo aliwakumbatia. Kwa njia hiyo Kundi la watu wapatao 20 walikaribishwa saa sita mchana. katika Jumba la Kitume mjini Vatican, kabla ya mkutano huko Palazzo Chigi, Italia na viongozi wa Serikali.

Papa wakati wa kuingia Ukumbini
Papa wakati wa kuingia Ukumbini   (@Vatican Media)

Katika hotuba yake, alianza kwa ishala ya Msalaba “ Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amani iwe nanyi. Habari za asubuhi nyote, karibuni.” Papa alianza kuzungumza kwana kabla kusoma kuelezea hizia zake kwamba “Ninasema kwa dhati kwamba nimeguswa sana kukutana nanyi. Nilipogundua kwamba mtu kwa niaba yenu alikuwa ameomba mkutano huu, mara moja nilisema, "Ndiyo, tutapata wakati." Nilitaka angalau fursa ya kushiriki wakati ambao kwenu, katikati ya maumivu na mateso mengi, ni mtihani wa imani yetu, mtihani wa kile tunachoamini. Mara nyingi tunajiuliza,"Kwa nini, Bwana?"

Kwa nini Bwana?

Mtu fulani alinikumbusha wakati kama huo, hasa wakati wa Misa ya mazishi ambapo, badala ya kutoa mahubiri, Padre alizungumza kana kwamba ni mazungumzo kati ya mtu na Mungu mwenyewe, na swali hilo ambalo huambatana nasi kila wakati, "Kwa nini, Bwana, kwa nini?" Papa aliongeza  “katika wakati huu wa maumivu na mateso makubwa, mmoja wa wapendwa wenu,  wapendwa zaidi amepoteza maisha katika janga kubwa sana, au amelazwa hospitalini kwa muda mrefu, mwili wake umeharibika kutokana na matokeo ya moto mbaya ambao umeteka mawazo ya ulimwengu mzima. Kwa hiyo ilikuwa ni kwa wakati usiotarajiwa, katika siku ambayo wote walikuwa wakifurahia na kufanya siku kuu, kubadilisha matashi mema ya furaha na kushangilia.”

Papa akitoa hotuba yake
Papa akitoa hotuba yake   (@Vatican Media)

Ni kitu gani cha kusema katika muktadha huu? Ni maana gani ya kutoa kwa tukio hilo. Ni mahali gani pa kupata faraja kwa kile ambacho mnapitia, faraja ambayo isiwe iliyojengwa kwa maneno matupu na ya kijuu juu, lakini yanayogusa kwa kina na kuuisha matumaini? Kuna Neno moja tu, Kaka na dada ambalo linafaa: lile la Mwana wa Mungu akiwa juu ya Msalaba, ambapo ninyi mko karibu leo hii, ambapo kwa kina cha kuachwa kwake na kwa uchungu wake alipaza sauti kwa Baba: “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha(Mt 27,46).

'Jibu kusubiri kwa siku tatu na kufufuka kwa utukufu'

Jibu la Baba akiombwa na Mwanae, linafanya kusubiri kwa siku tatu, katika ukimya. Lakini jibu kubwa! Yesu anafufuka kitukufu, kwa kuisha daima katika furaha na mwaka wa milele wa Pasaka. Papa Leo XIV alikiri jinsi ambavyo hasingeweza kuwafafanulia vya kusha kwa  wapendwa hao kaka na dada kwa sababu, wao wanaitwa na wapendwa wao kukabiliana na jaribio hilo.  

Wanafamilia na jamaa wafiwa
Wanafamilia na jamaa wafiwa   (@Vatican Media)

Kwa upande mwingine, "Mapenzi na maneno ya huruma ya kibinadamu ya mateso ninayowaambia leo hii yanaonekana kuwa machache sana na hayana nguvu, lakini kama Mfuasi wa Petro, ambaye wao wamekuja kutiwa moyo leo hii naye hana budi kuwathibitishia kwa nguvu na kwa usadikisho kwa nguvu: tumaini lenu si bure” kwa sababu Kristo alifufuka kweli! Kanisa Takatifu, ni ushuhuda na anatangaza kwa uhakika.

'Kumtumaini Kristo katika maisha haya'

Mtakatifu Paulo, aliyekuwa amemwona hai, aliwambia wakristo wa Korinto kuwa “Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote. Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala”(1Kor 15,19.20). Katika hili, Papa aliongeza tena kifungu kingine kuwa: “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? (Rm 8,35), kwa jinsi hiyo Wapendwa wenu ambao wanateseka au ambao mlipoteza.”

Wakati wa Hotuba ya Papa
Wakati wa Hotuba ya Papa   (@Vatican Media)

Papa alisisitiza kuwa Imani ambayo inaishi ndani yetu inaangaza katika wakati wa giza zaidi na uchgu wa maisha yetu na mwanga usiobadilishwa, ambao unatusaidia kuendelea kwa ujasiri katika safari kuelekea hatima. Yesu anatutangulia katika safari ya kifo na ufufuko ambao unahitaji uvumilvu na subira.  Muwe na uhakika wa ukaribu wake na huruma yake. Yeye hayuko mbali na  kile mnachopitia kinyume chake, anashiriki na kukichukua na ninyi.”

'Uhakika wa sala za Papa kwa ajili ya Marehemu'

“Na wakati huo huo, Kanisa zima linabeba na ninyi. Muwe na uhakika wa sala zake, na sala zangu binafsi, kwa ajili ya pumziko la marehemu wenu, kwa ajili ya kuwafariji wale ambao mnawapenda na ambao wanateseka, kwa ajili yenu ambao mnawasindikiza kwa upole na upendo wenu. Baba Mtakatifu aliwaeleza kuwa “Moyo wenu umechomwa leo, kama ulivyokuwa wa Maria chini ya Msalaba, Maria, Msalabani, aliyemwona Mwanawe. Mama yetu wa Huzuni yuko karibu nanyi katika siku hizi, na ni kwake ninayewakabidhi. Elekezeni machozi yenu kwake bila kujizuia na mtafute kwake faraja ya kimama ambayo labda ni Maria pekee anayeweza kutoa na hakika anaweza kuwapatia.”

'Kama Maria wa subira, mateso na matumaini'

Papa kwa kusisitiza zaidi “Kama Maria, mtajua jinsi ya kusubiri kwa uvumilivu, katika usiku wa mateso lakini kwa uhakika wa imani, kwa siku moja, siku mpya itakayopambazuka; na mtagundua tena furaha. Kama ishara ya faraja na ukaribu, na ya kutaka kushiriki wakati huu nanyi, ninawaalika kusali pamoja, na ninawapa kila mmoja wenu, pamoja na wapendwa wenu wote wanaoteseka, Baraka ya Kitume. Tuombe pamoja: Baba Yetu... Na kwa Maria, Mama Yetu, Mama Yetu wa Huzuni, tuseme: Salamu Maria... Hatimaye  Papa alitoa Baraka na kuongeza: “Amani na faraja ya imani iambatane nanyi siku zote. Amina.”

Papa kwa wafiwa na majeruhi

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

15 Januari 2026, 15:57