Papa akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania
Vatican News.
Papa Leo XIV, kabla ya Katekesi yake Jumatano tarehe 28 Januari 2026, alikutana na Balozi Mahmoud Thabiti Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania. Waziri yuko anatimiza ziara ya Kimataifa na alikuwa Mwakilishi wa Ujumbe wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliyethibitishwa kuongoza tena Tanzania katika uchaguzi wa Mwezi Oktoba iliyopita.
Kama itakumbukwa katika siku za upigaji kura, mwishoni mwa mwezi Oktoba 2025, kulitokea mapigano na vurugu ambazo kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kimataifa, zilisababisha mamia ya vifo.
Rais wa Tanzania aliunda Tume ya Uchunguzi ambayo tayari inafanya kazi kwa ajili ya ujenzi mpya wa kile kilichotokea na ambacho kinawakilisha mshtuko mkubwa kwa Nchi, ambayo hadi wakati huo ilikuwa tulivu na mahali ambapo hapakurekodiwa mvutano maalum wa kijamii. Vurugu hizo zilikuwa zimelaaniwa na viongozi wakuu wa Makanisa na kidini nchini Tanzania, Maaskofu na Maimamu, kwa kuomba kufanyika uchunguzi wa kujitegemea ili kubaini hali hiyo na wahusika.
Papa Leo XIV alikuwa amezungumza wazi kwa umma kuhusu hali hiyo ya nchi wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 2 Novemba 2025 akisema kuwa:“ Tusali hata kwa ajili ya Tanzania, mahali ambapo baada ya uchaguzi uliopita wa kisiasa, iliibuka mivutano na kusasabisha waathirika. Ninawaalika wote kuepuka kila aina ya vurugu na kuchuchumalia njia ya amani.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here
