Tafuta

Papa alikutana  mjini Vatican na Makapteni wa Jamhuri ya San Marino,Jumatatu 12 Januari 2026. Papa alikutana mjini Vatican na Makapteni wa Jamhuri ya San Marino,Jumatatu 12 Januari 2026.  (@VATICAN MEDIA)

Papa akutana na Wawakilishi wa Jamhuri ya San Marino

Matteo Rossi na Lorenzo Bugli walikaribishwa katika Jumba la Kitume la Vatican.Wakati wa majadiliano yao katika Sekretarieti ya Vatican na Kardinali Parolin na Askofu Mkuu Gallagher,waliakisi migogoro ya kimataifa,hasa ikihusu mgogoro wa Ukraine,ushirikiano katika diplomasia, na umuhimu wa mazungumzo kati ya dini mbalimbali.

Vatican News

Papa Leo XIV alikutana Jumatatu tarehe 12 Januari 2026, katika Jumba la  Kitume la Vatican, na Makapteni wa Jamhuri ya San Marino Yenye Utulivu Sana, Matteo Rossi na Lorenzo Bugli. Kisha  viongozi hawa walikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Papa alikutana na viongozi wawakilishi wa Jamhuri ya San Marino.
Papa alikutana na viongozi wawakilishi wa Jamhuri ya San Marino.   (@VATICAN MEDIA)

Majadiliano katika Sekretarieti ya Vatican

"Wakati wa majadiliano ya kirafiki katika Sekretarieti ya Vatican," taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican ilibainisha kuwa, "uhusiano mzuri  wa pande mbili uliopo uliakisiwa, pamoja na mchango wa Kanisa kwa jamii ya San Marino." Taarifa hiyo inaendelea kuwa,"Mazungumzo yaliendelea, yakizingatia migogoro ya kimataifa inayoendelea, hasa mzozo nchini Ukraine, ushirikiano katika diplomasia ya pande nyingi, na umuhimu wa mazungumzo kati ya dini mbalimbali katika kukuza amani."

viongozi wa San Marino walikutana  pia na Kardinali Parolin.
viongozi wa San Marino walikutana pia na Kardinali Parolin.   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

12 Januari 2026, 17:50