Tafuta

2026.01.31 Uzinduzi na Baraza kwa Sanamu ya Mtakatifu Rose wa Lima na Picha ya Maria katika Bustani za Vatican.  2026.01.31 Uzinduzi na Baraza kwa Sanamu ya Mtakatifu Rose wa Lima na Picha ya Maria katika Bustani za Vatican.   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Mama Maria na Rose wa Lima kukumbusha mada ya Utakatifu!

Bikira Maria na Rose wa Lima ni mwaliko wa utakatifu katika ulimwengu.Ndivyo Papa Leo XIV alibainisha wakati wa uzinduzi wa Picha ya Maria na Sanamu ya Mtatakatifu Rose wa Lima,Mlinzi wa Peru katika Bustani za Vatican.Rais wa Baraza la Maaskofu wa Peru:"Nguvu ya Injili hufanya kazi kwa ajili ya matunda kupitia watu wa kawaida."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mtakatifu wa Nchi pendwa, kuwa Mtakatifu katika Ulimwengu wa leo hii, na shukrani kwa wasanii na wafadhili, Ndiyo moyo wa hotuba fupi ya Jumamosi tarehe 31 Januari 2026, ambayo  Baba Mtakatifu Leo XIV aliitoa kwa lugha ya Kihispania kabla ya kutoa baraka kwa sanamu mbili takatifu, zilizowekwa kwenye  njia ya Pio XII, katika Bustani za Vatican. Papa Leo alianza kusema kuwa “kaka na dada wapendwa, tumekusanyika hapa leo kwa ajili ya tukio la furaha: uzinduzi wa mosaic iliyowekwa wakfu kwa Bikira Maria na sanamu ya Mtakatifu Rose wa Lima hapa katika Bustani za Vatican. Ishara hii inafufua vifungo vya kina vya imani na urafiki vinavyounganisha Peru, kama mnavyojua, nchi mpendwa kwangu na Kiti Kitakatifu.”

Sanamu ya Mtakatifu Rose wa Lima
Sanamu ya Mtakatifu Rose wa Lima   (@Vatican Media)

Papa aliendelea kuwasalimu kwa dhati wale wote waliohudhuria, hasa wajumbe wa Baraza la  Maaskofu wa Peru, pamoja na Balozi wa Peru katika Kiti Kitakatifu na Gavana wa Jiji la Vatican. Tumekusanyika katika mahali hapa pazuri, ambapo kila kitu kinatuzungumzia kuhusu Muumba na uzuri wa uumbaji, ninapenda kutoa shukrani zangu kwanza kabisa kwa wasanii waliounda kazi hizi na kwa wote waliotuwezesha kufurahia tukio hili la furaha leo.” Papa akimbuka Mtakatifu wa Siku aliongeza “Na kwa Familia nzima ya Salesian, siku hii hii, sikukuu ya Mtakatifu Yohame Bosco, tumekusanyika hapa, na tunawapongeza wote.”

Uzinduzi wa Picha ya Mama Maria na Sanamu ya Mtakatifu Rose wa Lima katika Bustan za Vatican.

Isabel Flores de Oliva, aliyetangazwa Mtakatifu mwaka 1671 na Papa Clement X kama Mtakatifu Rose wa Lima, si tu Mtakatifu wa kwanza wa Amerika Kusini, bali pia mlinzi wa taifa la Andes, ambapo Papa Prevost alitumwa kama mmisionari wa Kiagostino mwaka 1985 na ambapo alihudumu kuanzia 2014 hadi 2023, kwanza kama msimamizi wa kitume na kisha kama Askofu wa Jimbo la Chiclayo. Watu hao wawili waliibuka, Mama yetu wa mbinguni na mtakatifu wa kwanza wa Amerika Kusini, Rose wa Lima wanakumbuka mada ya utakatifu. Katika suala hilo Papa aliongeza kusema kuwa “ hebu tukumbuke kile ambacho Mtaguso wa Pili wa Vaticanunasema: “Kwa hivyo ni wazi kabisa kwamba waamini wote, bila kujali hali au hali yao, wameitwa kwa ukamilifu wa maisha ya Kikristo na kwa ukamilifu wa upendo […]. Katika kufikia ukamilifu huu, waamini wanapaswa kutumia nguvu waliyopokea kulingana na kipimo cha kipaji cha Kristo, ili, wakifuata nyayo na matendo yake waendane na mfano wake, wakitii katika mambo yote mapenzi ya Baba, waweze kujitolea kwa moyo wote kwa utukufu wa Mungu na kwa huduma ya jirani yao.”

Maaskofu na Papa katika Bustani za Vatican
Maaskofu na Papa katika Bustani za Vatican   (@Vatican Media)

Hivyo, utakatifu wa Watu wa Mungu utazaa matunda mengi, kama historia ya Kanisa inavyoonesha vyema katika maisha ya watakatifu wengi” (Lumen Gentium, 40). Papa akitazama hali ya hewa ya mvua iliyokuwa ikinyesha alisema “Tunaweza pia kuzungumzia wingi wa baraka za Bwana kwa maji haya matakatifu yanayowashukia alasiri ya leo.”  Papa alieleza kuwa picha hizo “nzuri tunazotafakari leo zinatukumbusha ukuu wa wito ambao Mungu anatuita, yaani, wito wa ulimwengu wote wa utakatifu. Ninawahimiza kuwa, kwa neema ya Mungu, mashuhuda na mifano ya utakatifu huo katika ulimwengu wa leo. Kwa maana hiyo ndiyo mapenzi ya Mungu: utakaso wetu wenyewe (taz. 1 Ts 4:3;Ef 1:4). Bikira Maria na watakatifu wote waombee katika safari yetu ya kwenda nchi yetu ya mbinguni. Kwa shukrani, ninawabariki kutoka moyoni mwangu.

Papa Leo katika Uzinduzi wa Picha ya Mama maria na Mtakatifu Rose wa Lima
Papa Leo katika Uzinduzi wa Picha ya Mama maria na Mtakatifu Rose wa Lima   (@Vatican Media)

Shukrani kwa Wasanii na Wafadhili

Katika hotuba yake tena , Leo XIV awashukuru  Familia ya Kisalesian wakiwa wanaadhimisha Siku Kuu ya mwanzilishi wao , na pia aliwashukuru wasanii waliounda kazi hizo, "Familia de Artesanos Don Bosco" yaa (Familia ya Ufundi ya Don Bosco) na Baraza la Maaskofu wa Peru, kwa kuzitoa na kwa kuturuhusu "kufurahia tukio hili la furaha leo." Picha  ya Bikira ni kazi ya timu ya wasanii vijana wa Andes wakiongozwa na Lenin Alvarez. Sanamu ya Mtakatifu Rose wa Lima iliundwa na Edwin Morales, mchongaji kijana  kutoka Sierra del Peru Wakati wa baraka, Papa aliwaombea ulinzi wa Bikira Maria Mtakatifu  sana kwa wale "waliounda sanamu hiyo," akiomba kwamba "waandike mioyoni mwao picha wanayoitafakari kwa macho yao." 

Picha ya Mama Maria ikibarikiwa
Picha ya Mama Maria ikibarikiwa   (@Vatican Media)

Papa alisali hivi: Wawe na imani isiyotikisika na tumaini thabiti, pamoja na upendo wa bidii na unyenyekevu wa dhati. Wawe na nguvu katika mateso, heshima katika umaskini, uvumilivu katika shida, ukarimu katika ustawi, wafanye kazi kwa amani na kupigania haki ili, baada ya kusafiri njia za ulimwengu huu kwa upendo kwao na kwa ndugu zao, waweze kufika katika mji wa milele, ambapo Bikira Mtakatifu sana anaombea kama Mama na kung'aa kama Malkia.

PAPA MARIA NA ROSE WA LIMA

Papa alimsalimia  Askofu  Carlos García Camader, Askofu wa Lurín na Rais wa Baraza la  Maaskofu wa Peru, na Maaskofu wengine wa Peru, ambao tangu tarehe 26 Januari hadi 31 Januari wamekuwa katika Ziara yao ya Kichungaji mjini Roma na Vatican "Visita ad limina Apostolorum"; Jorge Fernando Ponce San Román, Balozi wa Peru anayewakilisha Nchi yake mjini Vatican na Sista Raffaella Petrini, Rais wa Tume ya Kipapa ya Mji wa Vatican na Gavana. 

Papa akibariki
Papa akibariki   (@Vatican Media)

"Maombi mbalimbali ya Maria yanayowakilishwa hapa," alisema rais wa Baraza la Maaskofu kwa lugha ya kihipania, akielezea Picha ya Maria kuwa  "yanaelezea utajiri wa kiroho wa taifa ambalo, kutoka milima na mabonde yake, kutoka miji yake na jamii za wanyenyekevu zaidi, limepata ndani ya Bikira,  Mama wa karibu, ambaye humfariji, humsaidia, na humwongoza Mwanawe kila wakati." Hatimaye, akizungumzia sanamu ya Mtakatifu Rose wa Lima, iliyowekwa kinyume na mosaic, Askofu alielezea kwamba "ushuhuda wake unaendelea kuangazia ulimwengu uliojeruhiwa na vurugu, njaa, na kutojali, akitukumbusha kwamba nguvu ya Injili hufanya kazi kwa ajili ya matunda maalum kupitia watu wa kawaida na wanyenyekevu."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

31 Januari 2026, 15:28