Tafuta

Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 700 tangu Mtakatifu Ansgar alipoanza utume wake huko Copenhagen, Denmark. Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 700 tangu Mtakatifu Ansgar alipoanza utume wake huko Copenhagen, Denmark.  

Jubilei ya Kumbukizi ya Miaka 700 ya Utume wa Mt. Ansgar, Denmark

Maadhimisho haya yanafanyika Dominika tarehe 25 Januari 2026 Sikukuu ya Kuongoka kwa Mtakatifu Paulo Mtume na Mwalimu wa Mataifa, sanjari na kilele cha Maadhimisho ya Juma la 60 la Kuombea Umoja wa Wakristo linalonogeshwa na kauli mbiu: “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.” Efe 4:4. Papa Leo anasema, maskini wanapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza katika maisha na utume wa Mama Kanisa! Ushuhuda!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV amemteua Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, kuwa ni Mwakilishi wake wa Kitume, katika kilele cha Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 700 tangu Mtakatifu Ansgar alipoanza utume wake huko Copenhagen, Denmark. Katika maadhimisho haya Kardinali Parolin anaambatana na Monsinyo Niels ENGLEBRECHT, Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Copenaghen pamoja na Padre Marcos ROMERO BERNÚS,, Paroko wa Parokia ya Kanisa kuu la “Sant’Ansgar.” Maadhimisho haya yanafanyika Dominika tarehe 25 Januari 2026 Sikukuu ya Kuongoka kwa Mtakatifu Paulo Mtume na Mwalimu wa Mataifa, sanjari na kilele cha Maadhimisho ya Juma la 60 la Kuombea Umoja wa Wakristo linalonogeshwa na kauli mbiu: “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.” Efe 4:4. “Hata kama Wakristo wenyewe, katika hali ngumu ya maisha, wamepotoshwa na maambukizi ya mazoea yaliyojikita kwa hiari katika mafundisho ya kidunia au maadili ya kisiasa na kiuchumi, bado utendaji wa upendo unabaki kuwa msingi thabiti wa maisha na utume wa Kanisa. Kwa maana Kanisa kama Mama na Mwalimu, akisukumwa na hitaji la kukumbuka Injili kila wakati, hawezi kamwe kusahau maskini wake mwenyewe, akiweka historia nzima ya upendo wa Mungu kwa kusudi la Mungu, ambaye aliishi ndani yetu ili tuwe huru kutoka katika utumwa, hofu, dhambi na nguvu za kifo. Rej. Waraka wa Kitume wa Papa Francisko: "Dilexit nos” yaani “Alitupenda” Waraka wa Kitume juu ya upendo wa kibinadamu na wa Kimungu wa Moyo Mtakatifu wa Yesu Kristo. Nn 15-16.

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican
Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

“Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba ingawa alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikubali kuwa maskini, ili kwa umaskini wake ninyi mpate kuwa matajiri.” 2Kor 8:9. Baba Mtakatifu Leo XIV katika ujumbe huu anasema, kwa wazi, upendeleo wa maskini kama hao kwa upande wa Mungu kwanza ulimfanya yule mtawa mchanga wa Daraja la Mtakatifu Benedikto, aitwaye Ansgar, kuwasha kwanza kwa upendo safari hiyo ya Mataifa ya Denmark katika mwaka wa 826 pamoja na Harald, ambaye wakati huo alikuwa Mfalme mpya, aliyezaliwa upya kwa shida kutoka kwenye chemchemi takatifu, ambayo iliruhusu mbegu ya Injili kupandwa katika ardhi ya Skandinavia, kumbukumbu ambayo inafikia kilele chake tarehe 12 Januari 2026. Mtakatifu Ansgar pamoja na Mtakatifu Paulo, Mwalimu wa watu wa Mataifa, wana uwezo wa kutoa ushuhuda wa Injili ya Kristo Yesu kwa maneno na maonyo, ili ujumbe wa wokovu uenezwe kwa ari na saburi kila mahali. Ndiyo maana tukio hili linafaa liadhimishwe kwa heshima na taadhima kama fursa ya kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu, kwa wale ambao wako kwenye safari hii ya toba, wongofu wa ndani na utakaso wa maisha; pamoja na kuhamasisha kila mwamini aweze kuwa na hisia ya maisha ya Kikristo yenye bidii, imani thabiti na malengo zaidi.

Hayati Papa Francisko akiwa na viongozi wa Serikali kutoka Denmark.
Hayati Papa Francisko akiwa na viongozi wa Serikali kutoka Denmark.

Kumbe, Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Kardinali Pietro Parolin, ili kama mwakilishi wa Kitume aweze kuadhimisha Fumbo la Ekaristi Takatifu, kama kilele cha maadhimisho haya kwenye Kanisa kuu la Havne, lililo tabarukiwa na Mtakatifu Ansgar. Baba Mtakatifu Leo XIV anamwomba Kardinali Pietro Parolin, kumfikishia salam na matashi mema kwa watu wa Mungu nchini Denmark, ili waweze kujazwa na matunda ya kiroho, utakatifu pamoja na hamasa ya kupyaishwa upya. Baba Mtakatifu anahitimisha barua hii ya uteuzi kwa kumweka chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria na ya Mtakatifu Ansgar, aweze kuwasilisha vyema ujumbe wa neema ya mbinguni, ambao Baba Mtakatifu Leo XIV anapenda kuuwakilisha kwa watu wa Mungu nchini Denmark.

Miaka 700
20 Januari 2026, 15:39