Tafuta

Papa akibariki Picha itakayowekwa katika Basilika ya Kipapa la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta. Papa akibariki Picha itakayowekwa katika Basilika ya Kipapa la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta.  (ANSA)

Imewakilishwa Picha ya Papa itakayowekwa katika Basilika ya Mtakatifu Paulo

Katika ukumbi mdogo wa Ukumbi wa Paulo VI,Papa Leo XIV aliweza kuiona na kuipenda kazi ya kisanii ya mviringo"mosaic"ya kwake ambayo itawekwa katika Basilika ya Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta.

Vatican News

Jumatano tarehe 14 Januari 2026, Papa Leo XIV aliweza kutazama katika ukumbi mdogo wa Ukumbi wa Paulo VI, picha ya mduara wa "kimosaic" iliyoundwa na Karakana  ya Vatican katika Kiwanda cha Mtakatifu Petro(Fabbrica di San Pietro,) ambayo, kwa kufuata utamaduni, kazi ambayo utengenezwa baada ya uchaguzi wa kila Papa mpya.

Il Papa e il tondo musivo a lui dedicato

Papa akitazama Picha iliyotengenezwa kwa ajili yake(@Vatican Media)

Mzunguko huo wa picha ya kimosaic, unaojulikana kama clypeus, itawekwa katika Basilika ya Mtakatifu Paulo Nje ya Kuta, karibu na picha ya Papa Francisko katika sehemu ya kulia ya Basilika hiyo kwa urefu wa takriban mita 13. Ikiwa na kipenyo cha sentimita 137, mzunguko huo, kulingana na taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican ilitengenezwa kwa enamel za vitreous na dhahabu kwenye muundo wa chuma. Vigae takriban 15,000 viliundwa kwa kutumia mbinu ya kale ya kimosaic iliyokatwa na vilikuwa vimeunganishwa na gundi ya kiutamaduni ya Vatican. Na vile vinavyoonesha uso wa Papa Leo XIV vina thamani kubwa.

Papa akiwapokea waliowakilisha Picha hiyo
Papa akiwapokea waliowakilisha Picha hiyo   (@Vatican Media)

Kazi hiyo inaonesha mchoro wa picha wa Bwana Rodolfo Papa, ya mafuta kwenye turubai yenye ukubwa sawa na Mzunguko huo wa picha ya kimosaic, iliyoundwa maalum kwa ajili ya kubadilishwa kuwa mosaic. Kisha itahifadhiwa, pamoja na mfululizo mzima wa picha za mapapa, katika Kiwanda cha 'Fabbrica di San Pietro' mjini Vatican.

Papa akishangaa kazi hiyo
Papa akishangaa kazi hiyo   (@Vatican Media)

Kazi hiyo iliwasilishwa kwa Papa Leo XIV na Kardinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Basilika ya Mtakatifu Petro, Kardinali James Michael Harvey, Mkuu wa Basilika ya Mtakatifu Paulo Nje ya Kuta, na abate wa Monasteri ya Mtakatifu Paulo, Padre Donato Ogliari.

Picha ya pamoja
Picha ya pamoja   (@Vatican Media)

Waliungana na Bwana Rodolfo Papa na Paolo Di Buono, Mkurugenzi wa Mafunzo ya(Studio ya Musa ya Vatican,) na mwishoni mwa mkutano, Papa alisali pamoja na wale waliokuwepo kando ya kazi hiyo.

Il Papa insieme al cardinale Gambetti, il cardinale Harvey e l'abate Ogliari

Papa akiwa na Kardinali Gambetti, Harvey na Abate Ogliari(@Vatican Media).

Papa akibariki kazi hii
Papa akibariki kazi hii   (@Vatican Media)
Picha ya Papa Leo XIV

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

15 Januari 2026, 10:02