Tafuta

2026.01.06 Tangu siku ya Epifania, Papa leo anayo fimbo Mpya ya kichungaji 2026.01.06 Tangu siku ya Epifania, Papa leo anayo fimbo Mpya ya kichungaji  (@Vatican Media)

Fimbo Mpya ya Kichungaji ya Papa Leo XIV!

Tangu tarehe 6 Januari 2026,Papa amekuwa akitumia fimbo mpya ya kichungaji ambayo,Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia inaelezea,"iko katika mwendelezo" na ile iliyotumiwa na watangulizi wake,ikiunganisha utume wa kutangaza fumbo la Kristo msalabani na udhihirisho mtukufu wa ufufuko.

Vatican News

Tarehe 6 Januari 2026 katika Sherehe ya Epifania yaani Tokeo la Bwana na kufungwa kwa Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Leo XIV alitumia Fimbo Mpya ya Kichungaji. Kama Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa ilivyoelezea kuwa "fimbo hiyo ni mwendelezo na zile zilizotumiwa na watangulizi wake, ikiunganisha utume wa kutangaza fumbo la upendo lililooneshwa na Kristo msalabani na udhihirisho wake mtukufu katika ufufuko." "Fumbo la Pasaka, kitovu cha mvuto cha ujumbe wa kitume, kwa hivyo inakuwa sababu ya tumaini kwa wanadamu, kwa sababu kifo hakina nguvu tena juu ya mwanadamu, kwani kile Kristo alidhani pia alikikomboa," taarifa inasomeka. Wahudumu  wa kichungaji wa Papa  XIV "hawamtoi Kristo tena amefungwa na misumari ya Mateso, bali na mwili wake mtukufu katika kitendo cha kupaa kwa Baba.

Fimbo Mpya ya Kichungaji ya Papa Leo XIV
Fimbo Mpya ya Kichungaji ya Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Kama ilivyo katika maono ya Kristo Mfufuka, inawatokezea wafuasi wake majeraha ya msalaba, kama ishara zinazong'aa za ushindi ambazo, bila kufuta maumivu ya mwanadamu, zinaubadilisha kuwa mwanzo wa maisha ya kimungu." Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa pia inakumbuka kwamba Fimbo hiyo ya kichungaji, "kama nembo ya kiaskofu, haikuwahi kuwa sehemu ya nembo sahihi ya Papa wa Roma. Kuhusiana na hiyo hata hivyo tangu Enzi za Kati za mapema, Mapapa wametumia ferula pontificalis yaani fimbo ya kichungaji  kama ishara ya nguvu zao za kiroho na kiutawala. Ingawa Mtindo wa Fimbo hiyo ya kichungaji halielezeki wazi, labda lilikuwa fimbo iliyobeba Msalaba rahisi juu yake.

Mapapa walipokea nembo hii baada ya kuchaguliwa kwao, walipochukua kiti chao katika Basilika ya Mtakatifu Yohane Lateran. Hata hivyo, matumizi ya Fimbo hiyo hayajawahi kuwa sehemu ya liturujia ya Kipapa, isipokuwa katika matukio fulani, kama vile kufunguliwa kwa Mlango Mtakatifu ili kugonga milango mara tatu, au wakati wa kuwekwa wakfu kwa makanisa, kuchora alfabeti za Kilatini na Kigiriki sakafuni, kama inavyohitajika na ibada." Alikuwa ni Papa Mtakatifu Paulo VI ambaye, mnamo tarehe 8 Desemba 1965, wakati wa kufungwa kwa Mtaguso wa Pili la Vatican, alitumia " fimbo ya kichungaji" ya fedha yenye umbo la Msalaba.

Papa Leo XIV na fimbo mpya ya kichungaji
Papa Leo XIV na fimbo mpya ya kichungaji   (@VATICAN MEDIA)

Mchongaji Lello Scorzelli, ambaye alipewa jukumu la kuunda, hivyo alitaka kuelezea wito wa Mtume Paulo, ambaye Papa alichagua kubeba jina lake: lile la kuwa shahidi na mtangazaji wa Kristo aliyesulubiwa (taz 1 Kor 2:2). Mtakatifu Paulo VI, bila kutumia tena Fombo hiyo (ferula,) alianza kutumia msalaba huu wa kichungaji mara nyingi zaidi katika sherehe za kiliturujia, kama walivyofanya warithi wake. Tunakumbuka ishara ya Mtakatifu Yohane Paulo II, ambaye, mwanzoni mwa huduma yake ya Kharifa wa Mtume Petro, alichagua kuinua Msalaba wa kichungaji ili kuonesha kitovu cha mafundisho yake, kama ilivyotangazwa katika mahubiri yake: "Mfungulieni Kristo milango.”

Papa Benedikto wa XVI pia alichagua kutumia Msalaba wa dhahabu uliokuwa umeegemea msalaba wa dhahabu, uliokuwa ukitumiwa hapo awali na Mwenyeheri Pio IX, na baadaye ule aliopewa, ukiwa na ishara ya Mwanakondoo wa Pasaka na monogramu ya Kristo kati kati ya Msalaba, ikiwakilisha umoja wa fumbo la Msalaba na Ufufuko, kitovu cha kerygma ya kitume.

09 Januari 2026, 11:37