Tafuta

Papa Leo XIV:Utume wa familia Takatifu ni kiota na chimbuko la Wokovu wa Mungu!

Katika Dominika ya Mwisho wa Mwaka Desemba 28 Papa Leo XIV alisema:Kwa bahati mbaya,ulimwengu huwa na "Herode" wake daima,pendeleo zake za mafanikio kwa gharama yoyote,nguvu zisizo za kawaida,ustawi mtupu na wa kijuu juu,na mara nyingi hulipa matokeo katika upweke,kukata tamaa,mgawanyiko na migogoro.Tusiruhusu mizuka hii kuziba mwali wa upendo katika familia za Kikristo.Kinyume chake,tuhifadhi ndani yake maadili ya Injili.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tukiwa katika Oktava ya Noeli, Dominika tarehe 28 Desemba ya kila Mwaka, Mama Kanisa anawakumbuka Watoto Mashahidi, ambapo kwa mwaka huu, imeangukia katika Dominika ya Familia Takatifu ya Yesu Maria na Yosefu. Ni katika Mkutadha huo, ambapo Baba Mtakatifu Leo XIV akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume mjini Vatican, ametoa tafakari yake. Akianza tafakari hiyo  alisema “Leo tunaadhimisha Siku kuu ya Familia Takatifu na Liturujia inapendekeza kwetu  simulizi ya “kumbilia Misri(Mt 2,13-15.19-23).  Ni wakati wa majaribu kwa ajili ya Yesu, Maria na Yosefu.”

Papa Leo aliendelea kusema kuwa  “katika picha ya mwana wa Noeli, inamulika kiukweli karibu kwa ghafla, kivuli cha kushangaza cha hatari ya kifo, ambacho kina asili yake katika maisha ya wasi wasi wa Herode, mwanaume mkatili na mwagaji damu,  aliogopa kwa ukatili wake, lakini hasa kwa sababu hii alikuwa peke yake sana na alikuwa ametawaliwa na hofu ya kupinduliwa. Anaposikia kutoka kwa Mamajusi kwamba "mfalme wa Wayahudi" amezaliwa (tazama Mt 2:2), akihisi nguvu zake zikitishiwa, anaamuru kuuawa kwa watoto wote wa enzi ya Yesu. Katika ufalme wake, Mungu anafanya muujiza mkuu zaidi katika historia, ambapo ahadi zote za kale za wokovu zinatimizwa, lakini hawezi kuuona, akiwa amepofushwa na hofu ya kupoteza kiti chake cha utawala, utajiri wake,na mapendeleo yake.

Sala ya Malaika wa Bwana
Sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Katika Bethlehemu kuna nuru, kuna furaha: wachungaji wengine wamepokea tangazo la mbinguni na wamemtukuza Mungu mbele ya Pango la  Kuzaliwa kwa Yesu (tazama Lk 2:8-20), lakini hakuna hata moja kati ya haya linaloweza kupenya ulinzi wa kivita wa jumba la kifalme, isipokuwa kama mwangwi uliopotoka wa tishio, ili kuzuiwa na vurugu zisizo na upofu. Hata hivyo, ugumu huu wa moyo unaakisi zaidi thamani ya uwepo na utume wa Familia Takatifu. Katika ulimwengu wa kidikteta na wenye tamaa unaowakilishwa na mtawala dhalimu, Familia Takatifu ndiyo kiota na kitovu cha jibu pekee linalowezekana kwa wokovu: lile la Mungu, ambaye, kwa ukarimu kamili, hujitoa kwa wanadamu bila kusita au madai.

Na ishara ya Yosefu, ambaye, kwa utii kwa sauti ya Bwana, akimpeleka mchumba wake na  Mtoto kwenye usalama, inafunuliwa hapa katika umuhimu wake wote wa ukombozi. Kiukweli, huko Misri, mwali wa upendo wa nyumbani ambao Bwana aliukabidhi uwepo wake duniani unakua na kupata nguvu ya kuleta nuru kwa ulimwengu mzima. Tunapotazama kwa mshangao na shukrani fumbo hili, hebu tufikirie familia zetu wenyewe, na nuru ambayo inaweza pia kutoka kwao hadi kwa jamii tunayoishi.

Umati wa waamini katika sala ya Malaika wa Bwana
Umati wa waamini katika sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Kwa bahati mbaya, ulimwengu huwa na "Herode" wake daima, pendeleo  zake za mafanikio kwa gharama yoyote,nguvu zisizo za kawaida,ustawi mtupu na wa kijuu juu,na mara nyingi hulipa matokeo katika upweke,kukata tamaa,mgawanyiko, na migogoro.Tusiruhusu mizuka hii kuziba mwali wa upendo katika familia za Kikristo. Kinyume chake, tuhifadhi ndani yake maadili ya Injili: sala, kupokea sakramenti mara kwa mara, hasa Kitubio  na Komunyo, upendo mzuri, mazungumzo ya dhati, uaminifu, uthabiti rahisi na mzuri wa maneno na ishara nzuri kila siku.

Hii itawafanya kuwa mwanga wa matumaini kwa mazingira tunayoishi, shule ya upendo na chombo cha wokovu mikononi mwa Mungu(Papa Francisko, Siku X ya Familia Duniani, 25 Juni 2022). Kwa njia hiyo "tuombe basi kwa Baba wa Mbingu, kwa maombezi ya Maria na Mtakatifu Yosefu, abariki familia zetu na familia zote za Ulimwenguni, ili kwa kukua katika mfano wa Mwanaye aliyefanyika Mwili, ziweze kuwa ishara ya ufanishi kwa wote ya uwepo wake na kwa upendo wake usio na kikomo."

Kutazama kwa juu umati wa waamni katika sala ya Malaika
Kutazama kwa juu umati wa waamni katika sala ya Malaika   (@Vatican Media)
Tafakari Papa Desemba 28

Wito wa kuombea Amani

Hata hivyo Baba Mtakatifu mara baada ya Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 28 Desemba 2025 katika siku kuu ya Familia Takatifu, aliomba kuombea amani. Kwa mwanga wa Noeli ya Bwana, tuendelee kuombea amani. Leo, hasa, tuombee familia zinazoteseka kwa sababu ya vita, watoto, wazee, na walio katika mazingira magumu zaidi. Tujikabidhi pamoja kwa maombezi ya Familia Takatifu ya Nazareti.”

Papa ameomba tuombee amani
Papa ameomba tuombee amani   (@Vatican Media)

Akianza Papa Leo XIV alisema,  “Kaka na dada wapendwa, ninawasalimu nyote, Warumi na mahujaji kutoka nchi mbalimbali. Hasa, ninawasalimu vijana wa Clusone, Gerenzano, na San Bartolomeo huko Bosco, waliopataka kipamaia wa Adrara Mtakatifu Martino, vijana na wahudumu wa madhabahu wa Brescia, washiriki wa hija vijana wadogo kutoka Kitengo cha Kichungaji cha Sarezzo, na maskauti wa Treviso. ""Pia ninawasalimu waelimishaji wa Kitendo cha Kikatoliki cha Limena na wale wa Morciano ya Romagna, viongozi wa Kituo cha  Pio X cha Portogruaro, kundi la wakujitolea wa Borgomanero, waamini wa Mtakatifu  Cataldo na Serradifalco, na wanachama wa Pro Loco wa Mtakatifu Egidio wa Monte Albino." Papa alihitimisha kwa kuwatakia wote Dominika njema!

Papa baada ya Angelusi Des 28

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida kwa kubofya hapa: Just click here.

 

28 Desemba 2025, 12:15