Tafuta

Siku inayoisha na siku inayoanza kuitazamia kwa matumaini ha! Siku inayoisha na siku inayoanza kuitazamia kwa matumaini ha! 

Mapapa na Mwaka Mpya,Wakati wa Shukrani na Matumaini

Kadri ya mwaka 2026 unavyokaribia,tunawasilisha baadhi ya tafakari kutoka kwa Mapapa kuhusu kipindi hiki cha mpito kati ya mwisho wa 2025 na mapambazuko ya mwaka mpya.Ni mwaliko wa kutafakari thamani ya wakati,kutomaliza mwaka bila kumshukuru Mungu,kubaki mahujaji wa matumaini,kuandika ukurasa mpya tukimtumaini Bwana,kugundua upya wema,kujenga nyumba isiyobomoka.

Na Amedeo Lomonaco na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwaka mmoja unakaribia kuisha na mwingine unakaribia kuanza. Mtazamo wa Kanisa kwenye "mtiririko huu wa matukio" kati ya vipindi viwili tofauti lakini vinavyohusiana kwa karibu daima huunganishwa na Injili. Na unaenea katika upeo wa pande mbili: ule wa shukrani kwa Mungu na kumwamini Bwana. Shukrani na matumaini huwa funguo za kutafsiri yaliyopita yaliyopatikana na kukaribisha wakati ujao, pamoja na fursa zake na kutokuwa na uhakika kwake.

Maana  ya Wakati

Wakati wa "mpito" kutoka ukurasa ulio karibu kumalizika hadi ule ambao bado haujaanza ni mwaliko wa kutafakari wakati. Papa Paulo VI, katika Sala ya  Malaika wa Bwana  mnamo tarehe 2  Januari  1972, alihimiza kuzingatia thamani yake. "Kabla ya kuingia mwaka mpya, ni wakati wa kutenga muda kwake." “Wakati ni kipimo, mtu anaweza kusema, cha matukio yanayofuatana. Ni kipimo cha maisha yetu ya sasa. Kipimo kinachotia hofu, kwa sababu kinatuonyesha kwamba jana haipo tena, kwamba kesho haipo bado; leo pekee ipo, kiukweli, kwetu sisi ni wakati wa sasa pekee upo: tunaishi tu kwenye hatua inayosonga, wakati mmoja unaopita... Na hii inatufundisha kuishi kwa nguvu inayofaa wakati huu wa sasa, ambao sisi pekee ndio walimu, na ambapo uzoefu wetu pekee wa maisha ya sasa unajumuisha. Hiyo  inatufundisha thamani ya wakati.”

Papa Paolo VI (foto d'archivio).

Papa Paolo VI(kutoka hifadhi picha).

Msimalize mwaka bila kumshukuru Bwana

Maneno ya Mapapa katika hatua hii ya mwaka yanaambatana hasa na wimbo wa shukurani kwa Mungu(Te Deum): Papa Benedikto XVI, katika maadhimisho ya Masifu ya kwanza ya jioni  ya Sherehe ya Maria, Mama wa Mungu, mnamo tarehe 31 Desemba 2011, alizungumzia kwa usahihi nafasi hii maalum ya muda: "Mwaka mwingine unakaribia kuisha tunaposubiri mpya." Wasiwasi, matamanio, na matarajio hayawezi kutenganishwa na sifa kwa Bwana:“Kanisa linatushauri tusimalize mwaka bila kumshukuru Bwana kwa baraka zake zote. Ni katika Mungu kwamba saa yetu ya mwisho, saa ya mwisho ya wakati na historia, lazima iishe. Kusahau kusudi hili la maisha yetu kungemaanisha kuanguka katika utupu, kuishi bila maana. Kwa sababu hii, Kanisa linaweka midomoni mwetu wimbo wa kale wa Te Deum. Ni wimbo uliojaa hekima ya vizazi vingi vya Kikristo, ambao wanahisi hitaji la kuinua mioyo yao, kwa kujua kwamba sote tuko mikononi mwa Bwana mwenye rehema.”

Papa Benedetto XVI (Messa di Natale 24 dicembre 2012).

Papa Benedikto XVI(Misa ya Noeli tarehe 24 Desemba 2012).

Kubaki Mahujaji wa matumaini

Mwanzo mwa 2026 pia unaashiria mwisho wa Mwaka Mtakatifu wa Matumaini. Fadhila hii si mlango unaofungwa. Matumaini hayafi kamwe na ni "ya kuzaa," Papa Leo XIV alisisitiza katika Katekesi yake ya Jubilei mnamo tarehe 20 Desemba 2025: “Jubilei inakaribia kuisha, lakini tumaini ambalo Mwaka huu umetupati haliishi: tutabaki kuwa mahujaji wa matumaini! Tulisikia kutoka kwa Mtakatifu Paulo: "Kwa maana katika tumaini tuliokolewa". Bila tumaini, tumekufa; tukiwa na tumaini, tunaonekana. Tumaini huzalisha. Kwa kweli, ni fadhila ya kitaalimungu, yaani, nguvu kutoka kwa Mungu, na kwa hivyo, huzaa; haiui bali husababisha kuzaliwa upya. Hii ni nguvu ya kweli. Kinachotishia na kuua si nguvu: ni kiburi, ni hofu kali, ni uovu ambao hauzalishi chochote. Nguvu ya Mungu husababisha kuzaliwa. Kwa sababu hii, ningependa kukuambia hatimaye: kutumaini ni kuzaa Jubilei inakaribia kuisha, lakini tumaini ambalo Mwaka huu umetupa haliishi: tutabaki kuwa mahujaji wa matumaini! Tulisikia kutoka kwa Mtakatifu Paulo: "Kwa maana katika tumaini tuliokolewa" (Rm 8:24)."

 
Papa Francesco e due sposi (udienza giubilare 6 dicembre 2025).

Papa Francisko na wenye ndoa wapya(Katekesi ya Jubilei tarehe 6 Desemba 2025).   (@VATICAN MEDIA)

Karatasi nyeupe

Mwaka mpya, sasa katika safari yetu, unaonekana kwetu kutoka katika mtazamo usiojulikana. Mnamo tarehe 1 Januari 1986, Papa Yohane Paulo II alitualika kumtolea Bwana "hatua hii mpya na karatasi hii yeupe tu." “Mwaka Mpya unaonekana mbele yetu kama mahali pa ajabu, kama mahali ambapo tunapaswa kujaza maudhui, kama matarajio ya matukio na maamuzi yasiyojulikana ya kufanywa. Kama hatua mpya na eneo jipya katika mapambano kati ya mema na mabaya, katika ngazi ya kila mwanadamu na katika ngazi ya familia, jamii, mataifa: ya ubinadamu kwa ujumla.”

Papa Giovanni Paolo II (foto d'archivio).

Papa Yohane Paulo II(kutoka hifadhi picha).

Kurudisha Ukarimu

Ili kuandika kwenye ukurasa huu mtupu, lazima kwanza tutumie hazina ya fadhila. Mojawapo ya hizi, iliyotambuliwa na Papa Francisko mnamo tarehe 31 Desemba 2022, ina uwezo wa kuumba mahusiano ya kibinadamu na kuondoa kutojali: “Kaka  na dada wapendwa, naamini kwamba kurejesha wema kama fadhila ya kibinafsi na ya kiraia kunaweza kusaidia sana kuboresha maisha katika familia, jamii, na miji. Kwa njia hiyo kwa kutazamia mwaka mpya wa jiji la Roma, ningependa kuwatakia ninyi nyote tunaoishi hapa kukua katika fadhila hii ya ukarimu. Uzoefu unatufundisha kwamba, ikiwa unakuwa mtindo wa maisha, unaweza kuunda mshikamano mzuri na kugeuza mahusiano ya kijamii kuwa ya kibinadamu, kuondoa uchokozi na kutojali.”

Papa Francesco (foto d'archivio).

Papa Francisko(kutoka hifadhi picha).

Kujenga Nyumba Isiyoanguka

Kwa kutazama wakati ujao pia kunamaanisha kuwatazama wale wanaotusindikiza katika maisha yetu: familia zetu, wafanyakazi wenzetu kazini, majirani zetu. Shauku maalum ya Mwaka Mpya ilizungumziwa na Mtakatifu Papa Yohane XXIII katika ujumbe wake wa  tarehe 10 Januari 1960, kwa familia za Kikristo wakati wa Sikukuu ya Familia Takatifu: “Roho ya busara na kujitolea katika malezi ya watoto kwa uangalifu: na siku zote, katika kila hali, wasiwasi wa kusaidia, kusamehe, kuwahurumia, kuwapa wengine imani ambayo tungependa tupewe. Hivi ndivyo tunavyojenga nyumba ambayo haitaanguka. Tamaa tulivu ya usalama huu, ambayo ni dhamana ya amani ya milele, inatoka moyoni Mwetu ili kuwafikia kila mmoja wenu, ili kuongozana nanyi katika mwaka mpya: Inaungwa mkono na sala maalum, ambayo Tunaiinua kwa bidii Mbinguni kwa ajili ya familia ya kila mmoja wetu anayetusikia, hasa wale wasio na rasilimali, ajira, au afya, wanaokabiliwa na matatizo makali.”

Papa Giovanni XXIII (visita pastorale a Loreto, 4 ottobre 1962)

Papa Yohane  XXIII (Ziara ya Kichungaji huko Loreto, 4 Oktoba 1962).

Kutokana na maneno haya ya Papa Roncalli na tafakari za Mapapa, shauku inaenea hata tunapokaribia mwaka 2026: mwaka mpya uwe wakati mzuri kwa wote kujenga "nyumba ambayo haitaanguka," licha ya majeraha na kutokuwa na uhakika wa maisha, licha ya vitisho vya vita ambavyo bado vinatikisa familia ya wanadamu katika maeneo mbalimbali na mengi sana duniani.

Mama na mwaka mpya

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

31 Desemba 2025, 11:25