Mwaka 2025 kutoka Francisko hadi Leo kwa ishara ya Jubilei!
Na Salvatore Cernuzio – Vatican.
Maombolezo na furaha; uwanja unoalia kwa ajili ya Papa wa Amerika Kusini anayetwaliwa mbinguni, na uwanja huo huo unaofurahi kwa ajili ya Papa wa Amerika Kaskazini anayepanda kwenye kiti cha Kitume cha Mtume Petro. Upapa unaoisha na ule unaoanza na sherehe mpya, safari mpya, hati mpya, na mipango mipya. Kati ya Misa, Katekesi, rozari, mikesha, hija kwenye Mlango Mtakatifu, mikusanyiko mikubwa ya vijana na zaidi. Mwaka 2025 umekuwa mfano: mfano wa Kanisa likiendelea na safari yake zaidi ya mabadiliko ya historia na wakati.
Mwaka usiosahaulika kwa wanadamu kati ya kifo cha Papa Francisko na kuchaguliwa kwa Papa Leo XIV, katikati ya Jubilei, Mwaka Mtakatifu uliowekwa wakfu kwa ajili ya matumaini ambao uliofunguliwa na Papa Francisko, na utafungwa tarehe 6 Januari 2026 na mrithi wake Papa Leo XIV. Kuna mifano michache na iliyo mbali sana katika historia: Mapapa wawili katika wakati wa ajabu kwa watu wa Mungu. Kwamba watu walikuwa mstari wa mbele katika nyakati zilizoashiria zaidi mwaka 2025, ambao kwa bahati mbaya ulishuhudia kuzidi kwa mvutano wa kijiografia wa vita vya kimataifa na kuzidisha "vipande" vya kile, ambacho kwanza Papa Francisko na kisha Papa Leo, walikiita "Vita vya Tatu vya Dunia."
![]()
Papa Francisko alifungua Mlango Mtakatifu wa Mtakatifu Petro,Desemba 24(VATICAN MEDIA)
Ulimwenguni Roma
Zaidi ya mahujaji milioni 30 kutoka ulimwenguni kote walitembelea Roma wakati wa miezi ya Jubilei, katika nyakati za kawaida na katika matukio maalum zaidi ya 30 yaliyotolewa kwa sekta mbalimbali za Kanisa na jamii, na pia wakati wa kipindi kigumu cha kulazwa kwa Papa Francisko hospitalini ya Gemelli mnamo tarehe 14 Februari, ambacho kilimalizika na kifo chake tarehe 21 Aprili na mazishi yake siku tano baadaye tarehe 26 Aprili 2025. Zaidi ya watu 250,000 walihudhuria Misa ya mazishi ya Papa Jorge Mario Bergoglio; karibu mara mbili ya idadi hiyo walitoa heshima kwa Hayati Papa wakati mwili wake ulikuwa katika Basilika ya Mtakatifu Petro. Waamini wengi pia walihudhuria ibada za Rozari za jioni kwa ajili ya afya ya Papa, ambazo zilifanyika wakati wa kukaa kwake hospitalini, au kusali katika Uwanja wa Hospitali hiyo ya Gemelli, ambapo wengi wao, walikuwa vikundi na watu binafsi, waliendelea na hija yao baada ya kupitia Mlango Mtakatifu.
Kulazwa Hospitalini kwa Papa Francisko
Papa Francisko alionekana na ulimwengu katika mwezi mzima wa Januari, kuanzia na Sala ya Malaika wa Bwana, uliooneshwa na wito wa kusitisha vita “visivyo vya kibinadamu” na maumivu kwa akina mama waliopoteza watoto wao, na katikati mwezi Februari, hadi, kiukweli, kulazwa kwake hospitalini kwa kile kilichoonekana kuwa Ugonjwa wa bronchitis “ya kawaida”, ambayo baadaye ilijidhihirisha kuwa maambukizi ya vijidudu yenye milipuko kadhaa na maboresho ya polepole.
Katika Juma zilizofuata, licha ya afya yake kuwa mbaya, Papa aliendelea na shughuli zake, ikiwa ni pamoja na Katekesi yake ya Kawaida na ile ya jubilei (ya kwanza mwezi Januari tarehe 12), mikutano ya asubuhi na alasiri, na simu za jioni kwa Parokia huko Gaza. Kisha utawala wa Kanisa ukaja na uteuzi mbili muhimu, awali kwa: Sista Simona Brambilla, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Maisha Yaliyowekwa Wakfu na Vyama vya Kitume (Januari 6) na Sr Raffaella Petrini, Gavana wa Mji wa Vatican kunako tarehe 15 Februari 2025. Wanawake wawili, watawa wawili, wakiongoza Mabaraza muhimu kwa mara ya kwanza katika Curia Romana.
Miongoni mwa taarifa za kimatibabu, minyororo ya maombi, habari za kweli, na habari za uongo katika vyombo vya habari ulimwenguni kote vilisikika, huku kulazwa kwa muda mrefu kwa Jorge Mario Bergoglio hospitalini bado kulichorwa katika kumbukumbu ya ujumbe wake wa sauti unaogusa moyo, uliorekodiwa kwa lugha ya Kihispania na kwa sauti hafifu, kutoka hospitalini kuwashukuru waamini kwa msaada wao, na picha ile ya pekee kutoka siku hizo ya Papa akiwa amevaa vazi la zambarau katika Kanisa kwenye ghorofa ya kumi hospitalini.
Kurudi Vatican na kuaga kwa mara ya mwisho katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Mnamo tarehe 22 Machi 2025, madaktari walitangaza kuruhusiwa kwa Papa Francisko kutoka hospitalini. Mnamo tarehe 23 Machi 2025, alijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza kutokea kwenye balcony ya Hospitali ya Gemelli, huku akitoa maneno machache yasiyo na hisia, sauti yake ikiwa dhaifu, na uso wake ukiwa umechakaa. Kisha akarudi Vatican, baada ya kusimama kwa muda mfupi huko Mtakatifu Maria Mkuu, Basilika ambayo baadaye ikawa makao yake ya milele ya mabaki yake. Lakini wakati huo, kaburi lenye jina la Franciscus juu yake halikuwa la kufikirika, hasa baada ya ulimwengu kumuona Papa akionekana hadharani mara tatu: mara moja katika Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa Jubilei ya Wagonjwa; mara moja wakati wa kutembelea kaburi la Mtakatifu Pio X na sanamu ya Benedikto XV; na mara moja, ya mwisho ya kihistoria, kutokana na mabadiliko ya matukio,
kwa Urbi et Orbi ya Pasaka, pamoja na salamu ya karibu ya "Pasaka Njema" na safari katika Kigari cha Kipapa (Popemobile) kupitia Uwanja wa Mtakatifu Petro. Ya kwanza baada ya kulazwa hospitalini, na ya mwisho maishani mwake. Mikono yake na mwili wake wote ulikuwa dhaifu, lakini macho yake yalijaa furaha ya kufanikiwa katika uhamasishaji huu mpya wa umma, ambapo aliwashukuru washirika wake faraghani akisema: "Asante kwa kunirudisha uwanjani."
![]()
Mazisihi ya Papa Francisko(VATICAN MEDIA).
Kifo cha Papa
Siku iliyofuata, saa 3:50 asubuhi, Camerlengo, Kardinali Kevin Joseph Farrell alitangaza: "Asubuhi ya leo, tarehe 21 Aprili 2025, Papa Francisko alirudi katika Nyumba ya Baba." Sababu: kiharusi kilichofuatiwa na kushikwa kwa moyo. Kutoka hapo, sura mpya katika Kanisa ilianza, na heshima ya kihisia na endelevu ya watu huko Mtakatifu Marta na kisha huko Mtakatifu Petro, baada ya kuhamishwa kwa mwili wake, kuwekwa mihuri katika nyumba ya Jumba la Kitume, ibada ya kufunga jeneza, kisha mazishi mazito, msafara wa Jeneza kupitia mitaa ya Roma, na mazishi huko Mtakatifu Maria Mkuu, chini ya kaburi la marumaru nyeupe, mahali pa mtiririko wa mara kwa mara wa mahujaji na waamini wengi hata leo hii.
Mkusanyiko na Uchaguzi Mkuu wa Papa Leo XIV
Mnamo tarehe 27 Aprili 2025, Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin aliadhimisha Misa ya kwanza ya Novendia(yaani Misa 9 kabla ya uchaguzi Mkuu). Kufikia tarehe 28, makadinali 180, wakiwemo wale kutoka Majimbo Katoliki ya mbali zaidi na wale walio na zaidi ya miaka themanini bila haki ya kupiga kura, walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya mkutano wa kwanza wa jumla wa kujiandaa na (Conclave) uchaguzi Mkuu wa Papa. Tukio hilo, ambalo kwa karne nyingi limevutia na kuvutia umakini wa ulimwengu kwa tamaduni, taratibu, na usiri wake, lilisherehekewa mnamo tarehe 7 Mei 2025. Hii itakumbukwa katika historia kama moja ya Conclave za haraka zaidi katika historia, huku uchaguzi, wa Mei 8, katika mizunguko minne ya upigaji kura, wa Mrithi wa 267 wa Petro. Naye ni Robert Francis Prevost, Papa wa kwanza kutoka Marekani (aliyezaliwa miaka 69 mapema huko Chicago), lakini akiwa na roho ya nchini Peru baada ya kukaa zaidi ya miaka 22 akitumikia nchi ya Amerika Kusini kama mmisionari, Padre wa Parokia, Katekista, na Askofu. Papa kutoka kundi la Jumuiya ya Kitawa ile ya Mtakatifu Agostino, ambalo alihudumu kwa vipindi viwili kama Mkuu Shirika Ulimwenguni; Papa mwenye shahada ya hisabati na sheria ya Kanisa(Canon Law); Papa aliyeijua Curia Romana, kwa kuwa kama Mkuu wa Baraza la Kipapa la Maaskofu.
![]()
Misa ya Papa Leo XIV ikiwa ni mwanzo wa huduma ya Mtume Petro(@Vatican Media).
Upapa unaanza
Papa Leo XIV, jina lililochaguliwa kwa heshima ya Papa Leo XIII, mwandishi wa Waraka wa Kitume wa Rerum Novarum, ambao ulikuwa na sura ya kwanza ya Mafundisho Jamii ya Kanisa. Katika kuonekana kwake kwa mara ya kwanza, akiwa ameshikana mikono, amevaa mozzetta nyekundu na stola, na macho yake yakiwa yamejaa machozi ya hisia kali, Papa mpya aliyechaguliwa alitamka neno "Amani" kama neno la kwanza katika hotuba yake iliyoandikwa. Alirudia mara kumi zaidi. Alitoa wito wa "amani isiyo na silaha na kupokonya silaha”kutoka kwa Kanisa na ulimwengu; usemi ambao umekuwa alama ya Upapa wake. Kauli nyingine inayofafanua mpango wake ni ile aliyoshirikisha Baraza la Makardinali wakati wa Misa ya kwanza katika Kikanisa cha Sistine, siku moja baada ya kuchaguliwa kwake: ya "Kutoweka ili Kristo abaki."
Kufanya kazi kwa ajili ya Amani
Kipindi cha Papa Leo XIV kilianza mnamo Mei 8 na Misa ikiashiria uzinduzi wa upapa wake katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mbele ya umati wa wawakilishi waamini na wa kitaasisi kutoka ulimwenguni kote. Papa wa Marekani mara moja alikuwa sauti ya amani, akirudia wito kwa "watu wakuu wa ulimwengu" kutoka (Loggia delle Benedizioni) dirisha la Baraka ambapo alisali sala ya Malkia wa Mbingu ya kwanza tarehe 11 Mei 2025 na kusema: "Msipigane tena."
Papa Leo alizungumza kwa simu na marais wa Urusi na Ukraine, Putin na Zelensky. Zelensky alikutana na mwisho mara tatu, mara mbili huko Castel Gandolfo, ambapo, baada ya miaka kumi na miwili, Papa alirejesha nyumbani kwake wakati wa kiangazi, akiishi huko Villa Barberini na kuacha Jumba la Papa kama jumba la makumbusho lililo wazi kwa umma. Papa Leo XIV alipendekeza Vatican kama mahali pa upatanisho na mazungumzo ili kukomesha vurugu nchini Ukraine. Aliimarisha kazi ya kidiplomasia kwa maeneo yote ya migogoro ambayo yanaendelea "nyuma ya pazia." Akitazama mgogoro katika Mashariki ya Kati, alimpokea Rais wa Israeli Isaac Herzog (Septemba 4), ambaye pia alizungumza naye kwa simu baada ya shambulio la Sydney dhidi ya Jumuiya ya Wayahudi hivi karibuni, na kukutana na Rais wa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina, Mahmoud Abbas kunako (Novemba 5). Alirudia kwa uharaka wa kusitisha mapigano huko Gaza, misaada ya kibinadamu, na hitaji la suluhisho la serikali mbili.
Kisha Papa alilaani, kama katika hotuba yake kwa kikao cha jumla cha (Umoja wa Kazi za Misaada za Makanisa ya Mashariki(ROACO) kuwa “vurugu za kishetani” zinaathiri Mashariki ya Wakristo, akiwasihi waache “mantiki ya mgawanyiko na kulipiza kisasi” na wasisaliti hamu ya watu ya amani “kwa propaganda ya uwongo wa silaha.” Wito huu ulitolewa kwa nguvu zaidi katika ujumbe wa hivi karibuni wa Siku ya 59 ya Amani Duniani, ambapo Papa Leo XIV alilaani “upuuzi wa uhusiano kati ya watu” usiotegemea haki na uaminifu bali “kwa hofu na utawala wa nguvu.”
![]()
Papa akitia saini katika"Dilexi te", Wosia wake wa kwanza wa Kitume(@Vatican Media).
Dilexi Te na umakini wa mwisho
Sauti ya nguvu, kama zile zilizoelezea hotuba ya Papa Leo XIV aliyohutubia mnamo tarehe 23 Oktoba 2025 kwa Harakati Maarufu alizopokea mbele ya katekesi ya Jubilei yao mjini Vatican. Papa Leo alisisitiza umuhimu wa kupigania "haki takatifu"(ardhi, nyumba, kazi), alilaani ongezeko la dhuluma za kijamii, kuenea kwa dawa mpya za kulevya, "uharibifu wa dhamana" unaosababishwa na teknolojia mpya, na unyanyasaji wa kinyama kwa wahamiaji ("kutendewa kama takataka") na maskini. Wasiwasi wake kwa maskini umeakisiwa katika Wosia wake wa Dilexi te, ambao ni wa kwanza wa kitume uliochapishwa mnamo tarehe 4 Oktoba 2025. Mpango ulioanzishwa na Papa Francisko na kuzinduliwa upya na Papa Leo XIV.
Vijana, wahusika wakuu wa 2025
Kutoka kwa mtangulizi wake Papa Leo XIV, pia alirithi ahadi zote za Jubilei na kutangazwa kwa watakatifu wawili vijana, Carlo Acutis na Pier Giorgio Frassati. Sherehe mbili zilikuwa zimepangwa awali chini ya upapa wa Papa Francisko, moja wakati wa Jubilei ya Vijana wadogo au barubaru, na nyingine wakati wa Jubilei ya Vijana, lakini zote mbili ziliahirishwa kutokana na kifo chake. Papa Leo XIV aliwatangaza waamini hao wawili walei kuwa watakatifu pamoja mnamo tarehe 7 Septemba 2025, katika Misa kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro iliyohudhuriwa na maelfu ya waamini, hasa vijana.
Vijana. Hapa kuna pia wahusika wakuu wengine wa Mwaka Mtakatifu na mojawapo ya mambo muhimu ya upapa wake: Jubilei iliyowekwa kwao kuanzia Julai 28 hadi Agosti 3, 2025. Zaidi ya vijana milioni moja wa kiume na wa kike wa rika na asili zote walijaa Roma kwa juma hilo, baadaye wakimiminika Tor Vergata kwa ajili ya mkesha na Misa na Papa. Tamasha la nyuso, rangi, na bendera, huku Papa akiwahimiza vizazi vipya kutoridhika na mambo ya juu juu na mahusiano ya mtandaoni, bali kujenga vifungo halisi, kushinda uhusiano wa karibu na ukosefu wa mawasiliano, kujenga amani na kutamani utakatifu. Zaidi ya Tor Vergata, picha nyingine ya kukumbukwa ya Jubilei ya Vijana ni picha ya Papa, kwa kushangaza, katika gari lake kando ya Njia ya Conciliazione na Uwanja wa Mtakatifu Petro ili kuwasalimia umati uliokusanyika kwa ajili ya sherehe ya ufunguzi wa Jubilei.
"Ninyi ni nuru ya ulimwengu!" Askofu wa Roma alipiga kelele kwa umati uliomkaribisha kwa sauti ya "Lío" hiyo, "kelele" iliyopendwa sana hata na Papa Francisko. Mshangao mwingine, unaowahusisha tena vijana, ni ule ambao Papa alitoa mnamo tarehe 17 Oktoba 2025 huko Ostia wakati wa ziara yake katika meli ya Med25 Bel Espoir, chombo ambacho kilikuwa kikizuru bandari za Mediterania kwa miezi kadhaa kikiwa na vijana 25 wa mataifa na dini tofauti ndani yake. Picha ya kukumbukwa ya Papa Leo ndani ya Meli akiwa na walinda amani wakiimba na kupiga gitaa ni ukumbusho. Aliwaalika kutoa "ishara za matumaini" katikati ya chuki na vurugu.
![]()
Jubilei ya vijana huko Tor Vergata(@Vatican Media).
Ziara ya Uturuki na Lebanon
Mwangwi wa mwaliko huu pia ulisikika katika mandhari tata ya Lebanon, pamoja na Uturuki katika Ziara yake ya kwanza ya Kitume (Novemba 27 - Desemba 2). Safari hii ilipangwa, angalau katika sehemu ya Uturuki, kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Kwanza wa Kiekumene wa Nicea. Papa Leo XIV alitembelea Ankara kwa mipango ya kitaasisi na kisha aliruka hadi Istanbul, ambapo alikutana na Patriaki wa Constantinople, Bartholomew I, ambaye alisherehekea naye maadhimisho ya ukumbusho huko İznik, ambayo sasa ni Nicea, kwenye mwambao wa ziwa ambapo mabaki ya Basilika ya Mtakatifu Neophytos yapo. Hapo ni mahali, pa mkutano wa kiekumeni. Nchini Lebanon, Papa Leo XIV alitembelea mji mkuu Beirut, ambapo alisali kwenye bandari iliyoharibiwa na mlipuko wa 2020 na kuwakumbatia manusura na familia za waathiriwa. Alisherehekea Siky ya vijana ndogoWYD ndogo) huko Bkerké na vijana 15,000 kutoka Lebanon na Mashariki ya Kati. Alikutana na mapatriaki na wawakilishi wa makanisa ya Kikristo na viongozi wa dini zingine, ambao aliwaombea amani. Na aliwahimiza pande zinazopigana kuweka silaha zao chini.
Kukutana na Wafalme wa Uingereza
Kabla ya Ziara yake ya kimataifa, mnamo tarehe 20 Novemba 2025, Papa Leo XIV alifanya ziara yake ya kwanza nchini Italia, ya kwenda huko Assisi, kwa ajili ya kuhitimishwa kwa Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI). Katika mji wa Umbria, Papa alipiga magoti kwenye kaburi la Mtakatifu Francis, wa Assisi akimkabidhi hatima ya ubinadamu na Uumbaji. Papa pia alithibitisha tena kujitolea kwake kutunza nyumba yetu ya pamoja wakati wa kihistoria na wafalme wa Uingereza Charles III na Camilla, waliopitia asubuhi ya Oktoba 23, katika Kikanisa cha Sistine, ambapo sherehe ya kumsifu Mungu Muumba ilifanyika. Tukio linaloimarisha mazungumzo na njia ya kuelekea umoja.
![]()
Papa Leo XIV katika Bandari ya Beirut, huko Lebanon(@Vatican Media).
Uteuzi na Vitendo vya Utawala
Mnamo 2025, Papa Leo XIV pia alifanya uteuzi wake wa kwanza muhimu wa ndani (Monsinyo Filippo Iannone, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu; Padre wa Edward Daniang Daleng (OSA) kuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Nyumba ya Kipapa; Monsinyo Anthony Onyemuche Ekpo, kuwa Mkaguzi wa Sekretarieti ya Vatican na uteuzi wa Maaskofu Wakuu wa New York, Ronald Hicks, na Westminster, Charles Phillip Richard Moth. Kupitia motu proprio, rescripts, na chirographs, yaani Barua yake ya Mkono ya Papa Leo XIV alibadilisha usimamizi wa fedha wa Vatican, akiinyang'anya IOR haki yake ya kipekee ya uwekezaji na kuanzisha "jukumu la pamoja" na APSA; alirejesha Sekta ya Kati ya Jimbo la Roma; alichapisha Kanuni mpya za Curia Romana; alihimiza ujumuishaji wa watu wenye ulemavu katika jumuiya ya kazi ya Vatican; na alibadili Tume ya Michango kwa Vatican, iliyoanzishwa chini ya miezi 10 iliyopita.
Kuelekea 2026
Kwa hivyo, Papa Leo XIV, mwenye bidii na kujitolea kwa vitendo vya serikali, na pia kwa mamia ya Katekesi ya umma, na mikutano binafsi, na katika sherehe zote za Jubilei zilizowekwa kwa wafanyakazi, wafanyakazi wa afya, wanadiplomasia, harakati za kanisa na mashirika, waelimishaji, makatekista, maaskofu, mapadre, wanariadha na, hatimaye, mnamo Desemba 14, kwa wafungwa, ambapo alirudia wito wake kwa serikali kutoa msamaha au msamaha katika dakika hizi za mwisho za Jubilei. Jubilei itaisha mnamo tarehe 6 Januari 2025, kwa kufungwa kwa Mlango Mtakatifu wa Mtakatifu Petro. Basilika zingine tatu za Kipapa tayari zimefunga Milango yao Mitakatifu, kuanzia na ule wa Mtakatifu Maria Mkuu mnamo Desemba 25, Mtakatifu Yohane Lateran mnamo tarehe 27, na Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta mnamo tarehe 28 Desemba 2025.
Kwa hivyo, katika Sherehe ya Epifania, tendo la mwisho la Mwaka Mtakatifu litafanyika, likifuatiwa na tukio lingine muhimu kwa Kanisa na Papa: Mkutano Maalumu wa Makardinali aliouitisha tarehe 7 na 8 Januari 2026. Zitakuwa siku mbili za tafakari na maombi ya kutoa "msaada na ushauri" kwa Papa katika kuliongoza Kanisa la Ulimwengu. Serikali inayolenga kusikiliza, sinodi, na umoja wa Kanisa, kushinda mgawanyiko wote.
![]()
Papa Leo XIV(@Vatican Media).
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here
