Tafuta

2025.12.29:Wanachama wa Chama cha Kitaifa cha Manispaa ya Italia 2025.12.29:Wanachama wa Chama cha Kitaifa cha Manispaa ya Italia  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV kwa Manispaa za Italia:Siasa zinapaswa kukuza amani ya kijamii!

Papa Leo XIV akikutana na wawakilishi wa Chama cha Kitaifa cha Manispaa za Italia(ANCI),aliorodhesha changamoto zinazokabili miji leo hii ikiwa ni pamoja na mgogoro wa idadi ya watu,umaskini,vurugu,kutengwa na uchafuzi wa mazingira na aina za upweke zinazowakumba watu wengi.Ni pamoja na mfadhaiko,umaskini na kutelekezwa. Ameonya dhidi ya"kamari kuwa ni janga linaloharibu familia."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatatu tarehe 29 Desemba 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na Wajumbe wa Chama cha Kitaifa cha Manispaa za Italia(ANCI), ambapo katika hotuba yake alionesha furaha ya kukutana nao. “katika kipindi hiki cha Noeli na hitimisho la Mwaka wa Jubilei: Neema ya siku hizi iangaze kwa hakika hata huduma zenu na uwajibikaji wenu. Kufanyika Mwana wa Mungu, kunatufanya kukutana na mtoto, ambaye ni mnyenyekevu mdhaifu ambaye anakutana na nguvu za mfalme Herode. Kwa namna ya pekee, kuuawa kwa wasio na hatia kulingana na agizo lake, halina maana ya kupoteza mstakabali tu kwa jamii, bali ni onesho la madaraka yasiyo ya kibinadamu, ambayo hayatambui uzuri wa upendo kwa sababu, unadharau hadhi ya maisha ya binadamu. Kinyume chake, kuzaliwa kwa Bwana kunaonesha mantiki ya dhati zaidi kwa kila madaraka, ambayo awali ya yote ni uwajibikaji na huduma. Ili mamlaka yoyote yaweze  kujieleza katika tabia hizi, inahitaji kujionesha fadhila ya unyenyekevu, ya ukarimu na ya kushirikishana."

Papa Leo alisisitiza kuwa katika jitihada za umma, kwa namna ya pekee, wao wanatambua jinsi ilivyo muhimu kusikiliza kama mwanendo wa kijamii ambao huamsha fadhila hizi. Hii kiukweli  ya kuweka umakini kwa ulazima wa familia na watu, kwa kuwa na utunzaji hasa kwa walio wadhaifu zaidi, na kwa ajili ya wema wa wote. Mgogoro wa kupungua kwa  watu, na ugumu wa familia na wa vijana, upekwe wa wazee, na kilio cha kimya kwa maskini, uchafuzi wa mazingira na migogoro ya kijamii, ni hali halisi ambayo haiwaachi bila kujali. Papa aliongeza “wakati mnatafuta kutoa jibu, ninyi mnajua vizuri kwamba miji yetu siyo eneo lisilo na jina, lakini ni nyuso na historia za kulinda kama tunu za thamani.  Katika kazi hiyo mnageuka kuwa mameya siku baada ya siku, kukua kama  wasimamizi wa haki na wa kuaminika.

Papa na mameya wa miji ya Italia
Papa na mameya wa miji ya Italia   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV, alisisitizia kuhusu hilo, kwamba wawe na mfano wa Mtumishi wa Mungu Giorgio La Pira, ambaye katika hituba kwa Baraza la Wilaya ya Firenze alithibitisha “Una haki moja tu kwangu: kuninyima imani yako! Lakini huna haki ya kuniambia: Mheshimiwa Meya, usiwajali wale wasio na kazi (wale waliofukuzwa kazi au wasio na ajira), wasio na makazi (waliofukuzwa), wasio na msaada (wazee, wagonjwa, watoto). Ni wajibu wangu wa msingi. Ikiwa mtu anateseka, nina wajibu kamili: kuingilia kati kwa kila njia, kwa hatua zote ambazo upendo unapendekeza na ambazo sheria hutoa, ili mateso hayo yapunguzwe.  Hakuna kanuni nyingine ya mwenendo kwa meya kwa ujumla, na kwa meya Mkristo hasw(Maandiko, VI, p. 83).

Mshikamano wa kijamii na maelewano ya kiraia yanahitaji, kwanza kabisa, kuwasikiliza walio wadogo na maskini zaidi: bila kujitolea huku, "demokrasia inadhoofika, inakuwa ni uwakilishi wa majina, utaratibu, hupoteza uwakilishi wake, na huondolewa katika mwili kwa sababu inawatenga watu katika mapambano yao ya kila siku ya utu, katika kujenga hatima yao" (Papa Francisko, Hotuba, Novemba 5, 2016). Katika kukabiliana na magumu na fursa za maendeleo, ninawasihi muwe walimu wa kujitolea kwa manufaa ya wote, na kukuza muungano wa kijamii kwa matumaini.

Chama cha Kitaifa Italia cha mameya
Chama cha Kitaifa Italia cha mameya   (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV kadhalika alisema kuwa Mwishoni mwaJubilei alipenda kushirikisha nao umuhimu wa mada ambao kwa Mtangulizi wake mpendwa Papa Francisko alielekeza katika Tamko la Kutangaza Jubilei hiyo. Yeye aliandika kuwa: "Kila mtu anahitaji kugundua upya furaha ya kuishi, kwa sababu wanadamu, walioumbwa kwa mfano na sura ya Mungu (taz. Mwa 1:26), hawawezi kuridhika na kuishi tu au kutafuta riziki, kuzoea hali ya sasa huku wakiruhusu kuridhika na hali halisi za kimwili tu. Hii inatuweka tu katika ubinafsi na kuharibu matumaini, na kusababisha huzuni inayokaa moyoni, na kutufanya tuwe na uchungu na kutovumilia (Spes non confundit, 9)." Kadhalika "Miji yetu kwa bahati mbaya inajua mitindo ya ubaguzi, vurugu, na upweke ambao unahitajika kukabiliana nao. Papa alipenda "kutoa umakini kwa namna ya pekee juu ya Janga la mchezo wa kamari, ambao unaharibu familia nyingi. Takwimu zinaonesha ongezeko kubwa la upweke nchini Italia katika miaka ya hivi karibuni."

Wajumbe wa chama cha kitaifa cha Mameya Italia
Wajumbe wa chama cha kitaifa cha Mameya Italia   (@Vatican Media)

Kama Caritas Italia inavyosisitiza katika Ripoti yake ya hivi karibuni kuhusu Umaskini na Kutengwa kwa Jamii, ni tatizo kubwa kwa elimu, afya ya akili, na uaminifu wa kijamii. Hatupaswi kusahau aina nyingine za upweke ambazo watu wengi wanakabiliwa nazo: matatizo ya akili, mfadhaiko, umaskini wa kiutamaduni na kiroho, na kutelekezwa kijamii. Hizi ni ishara zinazoonesha hitaji la matumaini. Ili kuionesha kwa ufanisi, siasa inaitwa kujenga uhusiano halisi wa kibinadamu kati ya raia, na kukuza amani ya kijamii. Padre  Primo Mazzolari, kuhani makini katika maisha ya watu wake, alikuwa ameandika kuwa "Nchi haihitaji maji taka tu, nyumba, barabara, mifereji ya maji, na njia za wanaotembea kwa miguu. Nchi pia inahitaji jinsi ya kuhisi, kuishi, jinsi ya kutazamana, na jinsi ya kuungana,"(Hotuba huko Bologna 2006, 470).  Shughuli za usimamizi zinapatikana namna hiyo ukamilifu wake kwa sababu inafanya kukua talanta za watu, kwa kuwapatia ukuu wa kiutamaduni na kiroho wa miji.

Chama cha Kitaifa cha Mameya Italia
Chama cha Kitaifa cha Mameya Italia   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV alisisitiza kuwa “wawe na ujasiri wa kutoa matumaini kwa watu, kwa kubuni pamoja mtakabali ulio bora kwa ajili ya ardhi zao, katika mantiki ya uhamasishaji fungamani wa kibinadamu. Wakati wakuwshukuru kwa uwajibikaji wo katika huduma ya jumuiya, Papa alisema anavyowasindikiza katika sala, ili kwa msaada wa Mungu waweze kukabiliana kwa muafaka wa uwajibikaji wao wakishirikishana jitihada zao na wahudumu na wazalendo wao. Kwao na familia zao, Papa Leo XIV amewapatia baraka ya kitume na kuwatakia heri ya mwaka mpya.

29 Desemba 2025, 11:54