Tume ya Kipapa ya Jiji la Vatican yabadilisha sheria kuhusu rais
Vatican News
Sio Makardinali pekee bali pia "wajumbe wengine" wanaweza kushikilia wadhifa wa Rais wa Tume ya Kipapa ya Jiji la Vatican, wakiwemo wanaume na wanawake. Hii imeanzishwa na Barua Binafasi ya Motu Proprio ya Papa Leo XIV, iliyochapishwa tarehe 21 Novemba 20 25 ambayo inafuta Kifungu cha 8 cha Sheria ya Msingi iliyotolewa mnamo Juni 2023, kwa kuzingatia "mahitaji ya utawala ambayo yanazidi kuwa magumu na ya lazima." Kuanzia tarehe 1 Machi 2025, kwa amri ya Papa Francisko, mtawa, Sista Raffaella Petrini, aliteuliwa kuwa Rais wa Tume ya Kipapa ya Jiji la Vatican na Gavana. Yeye ndiye mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi hizi mbili, ambayo inajumuisha kazi za kisheria na kiutawala katika Nchi ya Jiji la Vatican.
Makala Mpya
Jarida la Ofisi ya Habari ya Vatican la mnamo tarehe 25 Februari 2025, kuhusu uteuzi wa Makatibu Wakuu wa Gavana, lilifafanua kwamba Papa Francisko alikuwa amerekebisha Sheria ya Msingi ya Jimbo la Jiji la Vatican. Kuchapishwa kwa Motu Proprio ya Leo XIV leo hii kunaimarisha mabadiliko yaliyotakiwa na mtangulizi wake. Hasa zaidi, Kifungu cha 8 cha Sheria ya Msingi kiliweka: "Tume ya Kipapa inaundwa na Makardinali, ikiwa ni pamoja na Rais, na wanachama wengine, walioteuliwa na Papa Mkuu kwa muhula wa miaka mitano." Katika Motu Proprio ya tarehe 21 Novemba 2025, makala husika inafutwa na kubadilishwa na yafuatayo: "Tume ya Kipapa ya Jimbo la Jiji la Vatican inaundwa na Makardinali na wanachama wengine, ikiwa ni pamoja na Rais, walioteuliwa na Papa Mkuu kwa muhula wa miaka mitano."Marekebisho haya yanafungua uwezekano kwamba "wanachama wengine" ambao si makardinali, kama vile watu wa kawaida na wanawake, wanaweza pia kuongoza Tume.
Uamuzi wa Papa
Papa Leo alihalalisha uamuzi wake kwa kuelezea, katika barua yake ya kitume, kwamba: "Gavana ameitwa kuchangia, kwa muundo wake, kwa utume unaofaa kwa JimSerikali ya Jiji la Vatican, kutekeleza kazi hii kwa kumtumikia Mrithi wa Petro, ambaye anawajibika moja kwa moja kwake." Katika kutimiza "kazi hii ngumu," Gavana hutumia "aina ya uwajibikaji wa pamoja katika ushirika, ambao," Papa alisisitiza, "ni mojawapo ya kanuni za huduma ya Curia Romana, kama ilivyotakiwa na Papa Francisko na kuanzishwa katika Katiba ya Kitume Praedicate Evangelium (Hubirini Injili ) ya tarehe 19 Machi 2022, pia inatumika kwa Nchi ya Vatican. Kwa hivyo, "aina hii ya uwajibikaji wa pamoja" inafanya iwe "sahihi kuimarisha baadhi ya suluhisho zilizotengenezwa hadi sasa ili kukabiliana na mahitaji ya utawala ambayo yanazidi kuwa magumu na ya haraka." Motu Proprio, ilisainiwa Novemba 19, na ambayo imechapishwa tarehe 21 Novemba 2025 na ambayo inaanza kutumika kuanzia siku hii
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe: cliccando qui
