Tafuta

2025.11.01 Wakati wa Mis Takatifu tarehe Mosi Novemba 2025,Papa leo alimtangaza Kardinali Newman kuwa Mwalimu wa Kanisa. 2025.11.01 Wakati wa Mis Takatifu tarehe Mosi Novemba 2025,Papa leo alimtangaza Kardinali Newman kuwa Mwalimu wa Kanisa.  (@Vatican Media)

Papa:Mtakatifu John Henry Newman Mlinzi wa Chuo Kikuu cha Urbaniana

Tunachapisha maandiko ya mkono ya Papa Leo XIV,kumtangaza Mtaalimungu mkuu kuwa "mfano unaong'aa wa imani na utafutaji wa wazi wa kweli,"Mlinzi wa Chuo Kikuu cha Kipapa.Kwa hiyo,Papa alikubali ombi lililotolewa na Kardinali Tagle,Chansela wa Chuo Kikuu cha Urbaniana.

Vatican News.

Papa Leo kwa mkono wake, ameandika na kuthibitisha Mtakatifu John Henry Newman  aweze kuwa Mtakatifu Mlinzi wa Chuo kikuu cha Kipapa cha Urubaniana. Katika maandishi hayo yanasomeka kuwa: “Kwa kuzingatia maombi ya, Kardinali Luis Antonio Gokim Tagle katika Wadhifa wake wa Chansela wa chuo Kikuu cha Urbaniana, ambaye alifanya mapendekezo yake kwa Uwakilishi wa Kipapa, na  Mkuu wa Chuo hicho cha Kipapa,

Ninathibitisha, kwamba Mtakatifu John Henry Newman, Kardinali wa Kanisa Takatifu la Roma na Mwalimu wa Kanisa, aliyezaliwa tarehe 21 Februari 1801 huko London na kifo chake tarehe 11 Agosti 1890 huko Edgbaston, aliyetangazwa kuwa Mtakatifu tarehe 13 Oktoba 2019 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, na alitangazwa kuwa Msimamizi wa Chuo cha Kipapa cha Urbaniana, ili aweze kuombea Taasisi hiyo ya kielimu, na awe kwa kila mmoja ambaye anafundwa kwa ajili ya huduma ya kimisionari ya Kanisa, mfano angavu wa imani na utafutaji wa wazi wa ukweli.

Hati hiyo iliwekwa saini  na Papa Leo mwenywe mjini Vatican tarehe 1 Novemba 2025 katika Siku Kuu ya Watakatifu Wote.

Uthibitisho wa Papa kwa Mwalimu wa Kanisa
03 Novemba 2025, 16:17