Papa Leo XIV:Madhabahu ya Pompeii,ngome ya amani inayopaswa kulindwa
Vatican News
Upendo wa bidii wa Maria, kuanzia nyumba ya Nazareti hadi Kalvari, "unapata mwendelezo na, kana kwamba, unadumu 'katika kuwatunza wanyenyekevu, maskini, wanyonge, katika kujitolea kwake mara kwa mara kwa amani na maelewano ya kijamii.' Hiki ni kifungu kutoka katika Barua ya Kilatino iliyoandikwa na Baba Mtakatifu Leo mnamo tarehe 7 Oktoba 2025 katika, Siku kuu ya Mama Yetu wa Rozari, iliyoelekezwa kwa Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, ambaye Papa Leo XIV alimteua kuwa Mwakilishi wake mnano tarehe 12 Septemba katika sherehe za tarehe 13 Novemba 2025 wakati wa fursa ya kumbukumbu ya miaka 150 ya kuwasili kwa Ishara hii ya Picha ya Mama Yetu wa Rozari.
Katika maandishi hayo, Papa alikumbuka tukio hilo la tarehe 13 Novemba 1875, katika Bonde la "kutofarijika" wakati huo, lililoitwa hivyo kwa sababu ya hali ya kutelekezwa na ukiwa wa eneo ambalo Bartolo Longo, mwanzilishi wa Madhabahu ya Pompei, alikuwa amefika miaka michache kabla.Maadhimisho ya mwaka huu yanaadhimishwa karibu mwezi mmoja baada ya kutangazwa kuwa mtakatifu kwa "mfadhili wa ubinadamu," kama Papa alivyomwita katika mahubiri yake katika Misa mnamo tarehe 19 Oktoba 2025. Tangu siku hiyo ya Novemba miaka 150 iliyopita, uhusiano kati ya Bikira Maria na waamini umekuwa wa kipekee. "Shukrani kwa kazi ya upendo ya mtakatifu mpya Bartolo Longo, mwanzo huo unaoonekana kuwa wa unyenyekevu ulikuwa mwanzo wa matendo makuu ya upendo, ambayo yako mbele ya macho ya kila mtu,” Papa aliandika.
Maandishi yanasomeka tena kuwa "Kwa kuwa ngome kuu ya Amani hiyo ambayo lazima ipatikane na kutetewa kila mara, tumejifunza, kwamba Madhabahu katika Bonde la Pompei yanajiandaa kwa moyo wa shukrani kufanya upya kumbukumbu ya miaka 150 ya kuwasili kwa Picha ya Bikira Maria." Ni kwa sababu hiyo kwamba, kwa ombi la Askofu Mkuu Tommaso Caputo, Askofu Mkuu wa Pompei na Mjumbe wa Kipapa wa Madhabahu ya Bikira Maria wa Rozari Takatifu, Papa alichagua kumtuma Kardinali Parolin.
Miongoni mwa majukumu yake ni kuongoza sherehe ya Misa Takatifu, kuwabariki waamini na wageni wa matendo ya upendo, "akiwahimiza kuendeleza, katika Madhabahu ya imani na upendo, iliyoojengwa kutokana na juhudi za watu wengi," Papa Leo anaandika, "roho ya Kikristo na ya kutafakari ya Rozari, kulingana na msukumo uliotolewa na Mtakatifu Bartholomew wa hivi karibuni na kukuzwa na Mtangulizi wetu Papa Leo XIII, Papa wa Rozari."
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa ungependa kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu kwa kubofya hapa: cliccando qui
