Tafuta

Papa Leo XIV:Wasaidieni na kuwaelimisha vijana

Katika ujumbe wa video uliotumwa kwa Mkutano wa Kitaifa wa kuhusu madawa ya kulevya ulioandaliwa Roma na serikali ya Italia,Papa Leo XIV anasisitiza tabia ya vijana kujitenga wanapokabiliwa na kutokuwa na uhakika wa mustakabali na"ulimwengu usio na matumaini."Anatoa wito kwa taasisi kukuza utamaduni wa mshikamano na kuwasikiliza, haswa wale walio katika mazingira magumu zaidi.Madawa ya kulevya ni dalili ya kuharibika kwa jamii na Ulimwengu usio na Matumaini.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alituma ujumbe wake kwa njia ya video kwa Mkutano wa 7 wa Kitaifa kuhusu “Madawa ya Kulevya,” ulioandaliwa jijini  Roma na Waziri Mkuu wa  Baraza la Mawaziri, ambao ulifunguliwa tarehe  Novembatarehe 7 -8 Novemba 2025  na  ambao ni Mkutano wa siku mbili wa wadau wa umma na binafsi wanaohusika katika kuzuia, matibabu, na kupona, unaohudhuriwa na Rais wa Italia Bwana Sergio Mattarella.  Papa Leo XI alirudia kuonesha  wasiwasi wa vijana ambao mara nyingi huanguka katika uraibu, sio tu kwa pombe au dawa za kulevya, bali pia kwa mtandao. Wakati huo huo, anazungumzia kuhusu dhiki ya vijana wanaoishi "wakati wa majaribu na maswali," hawawezi, wanakabiliwa na vichocheo elfu, kutofautisha mema na mabaya na kwa hivyo hawawezi kuweka mipaka ya maadili.

Madawa mapya ya kulevya

Papa alitoa orodha ndefu ya aina za madawa mapya ya kulevya yanayotokana na kuongezeka kwa matumizi ya intaneti, kompyuta, na simu za mikononi, ambayo huleta zaidi ya faida dhahiri tu. Matumizi kupita kiasi mara nyingi husababisha madawa ya kulevya na matokeo mabaya ya kiafya, kama vile kamari na ahadi za kulazimishwa, picha mbaya za mitandaoni, na uwepo wa mara kwa mara kwenye majukwaa ya kidijitali. Na lengo la madawa ya kulevya huwa ulevi, unaoathiri tabia na maisha ya kila siku.

Matukio haya, Leo XVI alisema, "ni dalili ya dhiki ya kiakili au ya ndani ya mtu binafsi na ya kuharibika kwa maadili na marejeo chanya kijamii, hasa kwa vijana wa kike na kiume, wakati ambapo watu wanajaribu kupata maana katika maisha yao. Njia hii inajitokeza katika ulimwengu uliounganishwa sana ambapo watu wanafikiri wanaweza kufanya chochote bila mipaka ya maadili, ambapo mipaka kati ya mema na mabaya inazidi kuwa hafifu. Kuongezeka kwa biashara ya dawa za kulevya na matumizi ya dawa za kulevya, kutafuta pesa rahisi kupitia mashine  zinazopangwa, na madaya ya kulevya kupitia mtandaoni, ikiwa ni pamoja na maudhui yenye madhara, yanaonesha kwamba tunaishi katika ulimwengu usio na matumaini, usio na fursa kubwa za kibinadamu na kiroho.

"Vijana wanahitaji kuunda dhamiri zao"

Vijana wa kike na kiume Papa anasisitiza wanahitaji kuunda dhamiri zao, kukuza maisha yao ya ndani, na kuanzisha uhusiano mzuri na wenzao na watu wazima katika mazungumzo yenye kujenga, ili kuwa waumbaji huru na wenye uwajibikaji wa maisha yao wenyewe.  Hapo ndipo unakuja mwaliko wa Papa Leo XIV kuwa ni kutenda kwa njia ya pamoja, katika juhudi za kuzuia zinazotafsiriwa kuwa uingiliaji kati wa jamii kwa ujumla. Ni wito wake kwa Serikali, vyama vya kujitolea, Kanisa, na jamii kujibu kilio cha vijana cha kuomba msaada, pamoja na kiu yao kubwa ya maisha,"hivyo kutoa uwepo wa kujali unaowasaidia kujenga nia yao.

Kwa hivyo, Papa alibanisha kuwa, ni muhimu kuongeza kujithamini kwa vizazi vipya ili kukabiliana na hisia ya kutokuwa na usalama na kutokuwa na utulivu wa kihisia unaosababishwa na shinikizo la kijamii na asili ya ujana." Fursa za kazi, elimu, michezo, mtindo wa maisha wenye afya, mwelekeo wa kiroho wa kuwepo: hii ndiyo njia ya kuzuia madawa ya kulevya. PapaLeo XIV aliwaomba wanaoshiriki "mapendekezo ya vitendo" ili kukuza utamaduni wa mshikamano na uungwana, kuwafikia wengine, kusikiliza, katika safari ya kukutana na uhusiano na wengine, hasa wanapokuwa katika mazingira magumu zaidi na dhaifu.

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa ungependa kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu kwa kubofya hapa: Just click here.

07 Novemba 2025, 16:12