Papa Leo XIV:ufahamu muhimu zaidi hupatikana tukiwa tumepiga magoti
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV, Alhamisi tarehe 6 Novemba 2025 alikutana na washiriki Mkutano Mkuu wa Mashirika mawili: Yesu na Maria na Masista Wamisionari wa Mtakatifu Charles Borromeo, (Scalabrinian). Akiwakaribisha wajumba hao katika hotuba yake Papa alitoa shukrani kwa huduma yao na kutoa matashi mema kwa Wakuu wakuu wa mashirika hayo waliochaguliwa hivi karibuni. Alikumbuka kwamba mashirika hayo mawili yalizaliwa katika hali tofauti lakini kutokana na upendo uleule kwa maskini, yakiunganishwa na karama ya pamoja ya huruma.
Akitafakari mada zilizochaguliwa kwa ajili ya mikutano yao mikuu, ya: “Yesu mwenyewe alikaribia” (Lk 24:15) na “Popote uendako, mimi nitaenda” (Ruth 1:16) – Papa Leo alisema hizi zinaonesha mpango wa Mungu na mwitikio wa kibinadamu. Katika Injili ya Mtakatifu Luka, “tunamwona Yesu akijiunga na wanafunzi wa Emau na kutembea nao, akiwaongoza kumtambua katika kuumega mkate.” Na wakati huyo katika Ruth, kwa upande mwingine, “tunamwona mwanamke kijana Mmoabu ambaye, ingawa angeweza kufanya hivyo, kumtelekeza mama mkwe wake Naomi, bali alimsindikiza hadi nchi ya kigeni ili kumtunza hadi mwisho.”
Papa Leo kwa njia hiyo alikumbuka kwamba Mtakatifu Claudine Thévenet, mwanzilishi wa Shirika la Yesu na Maria, na Mtakatifu Giovanni Battista Scalabrini, pamoja na MwenyeHeri Assunta Marchetti na Mtumishi wa Mungu Giuseppe Marchetti, waanzilishi wa Masista wa Scalabrini, walikabiliwa na nyakati za majaribu makubwa. Papa alisisitiza kwamba “lakini siri ya uaminifu kama huo inapatikana katika kukutana kwao na Yesu Mfufuka. Hapo ndipo yote yalipoanzia kwao na pia kwao."
Baba Mtakatifu leo XIV kwa njia hiyo alisisitiza wajumbe hao wa mikutano mikuu ya shirika huku akiwasisitiza watawa hao wamruhusu Yesu atembee pamoja nao na wasaidie kusoma tena historia yao katika mwanga wa Pasaka. Na kwa kukazia zaidi juu ya maombi alisema kwamba “ufahamu muhimu zaidi hupatikana tukiwa tumepiga magoti, na kile kinachokomaa katika vyumba vya mikutano kinahitaji kupandwa na kuchujwa mbele ya Hema na katika kusikiliza neno." Kwa mujibu wa Papa katika hotuba hiyo aliwasihii washiriki kutoa nafasi nyingi katika maombi na ukimya katika kipindi chote cha kazi yao huko akiwakumbusha kwamba ni kwa kumsikiliza Bwana tu ndipo tunajifunza kusikilizana kweli.
Akimnukuu Papa Francisko na Mtakatifu Yohane Paulo II, Papa Leo XIV aliwataka masisitia hao kutafuta uso wa Mungu katika kaka na dada zetu wanaohitaji na kuona katika kila mtu ahadi, tumaini, ufunuo wa uwepo wa Mungu. "Hili linahitaji ujasiri, kujiruhusu tupingwe na uwepo wa wale wanaoteseka, bila hofu ya kuacha usalama wetu wenyewe, na kuthubutu, ikiwa Bwana ataomba, kuingia kwenye njia mpya."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here
