Tafuta

2025.11.08 Katekesi ya Jubilei. 2025.11.08 Katekesi ya Jubilei.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV,Katekesi:Kutumaini ni kushuhudi.Isidore Bakanja

Isidori kiukweli,anajikuta akifanya kazi kama mfanyakazi wa shambani kwa bwana Mzungu asiye na adabu,ambaye hawezi kuvumilia imani yake na uhalisia wake.Huyo alichukia Ukristo na wamisionari waliowatetea wenyeji dhidi ya unyanyasaji wa wakoloni,lakini Isidori alivaa skapulari yake yenye picha ya Bikira Maria shingoni mwake hadi mwisho,akivumilia kila aina ya unyanyasaji na mateso,bila kupoteza tumaini.Ni kiini cha Tafakari ya katekesi ya Papa Leo Novemba 8 kuhusu sura ya Isidori Bakanja.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV ameongoza Katekesi ya Jubilei Jumamosi tarehe 8 Novemba 2025 na hasa kwa kuwasalimia washiriki wa Jubilei ya Ulimwengu wa Kazi, ambapo alitoa  wito wa kujitolea kwa pamoja katika asasi za kiraia ili kuongeza ajira na kuhakikisha vijana wanaweza kutimiza ndoto zao na kuchangia kwa manufaa ya wote wakati wa salamu zake. Lakini  katika katekesi yake, ilihusu mada "Kutumaini ni Kushuhudia, alitoa mfano wa Mwenyeheri Isidori Bakanja, wa Nchini Congo DRC. Kabla ya Katekesi hiyo, awali ya yote alizungukia waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kama kawaida, huku akibariki watoto wengi. Kwa mujibu wa taarifa za Vyom vya habari vatican, waamini wapatao 45,000 waliudhuria kutoka ulimwenguni kote.

Baada ya kufika lilisomwa somo: "Haya ndugu angalieni hali yenu ya wakati mlipoitwa: si wengi wenu mlikuwa na hekima ya ulimwengu, si wengi mlikuwa watu maarufu. Si wengi mlikuwa wa ukoo wa kifalme. Bali Mungu ameyachagua yaonekanayo dhaifu kwa watu, Mungu ameyachagua ayaabishe yenye nguvu(1Kor 1,26-27.)"

Katekesi ya Jubilie Novemba 8
Katekesi ya Jubilie Novemba 8   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV alianza na salamu  na kuwakaribisha wote na kusema: “Tumaini la Jubilei hutokana na mshangao wa Mungu. Mungu ni tofauti na vile tulivyozoea kuwa. Mwaka wa Jubilei unatusukuma kutambua utofauti huu na kuubadilisha kuwa maisha halisi. Hii ndiyo sababu ni Mwaka wa neema: tunaweza kubadilika! Daima tunaomba hili tunapomwomba Baba Yetu na kusema: "Duniani kama mbinguni." Mtakatifu Paulo anawaandikia Wakristo wa Korintho, akiwaalika kutambua kwamba miongoni mwao, dunia tayari imeanza kufanana na mbingu. Anawaambia wafikirie wito wao na kuona jinsi Mungu alivyowaleta pamoja watu ambao vinginevyo hawangekutana nao. Wale ambao ni wanyenyekevu zaidi na wasio na nguvu sasa wamekuwa wa thamani na muhimu (rej. 1 Kor 1:26-27). Vigezo vya Mungu, ambavyo huanza na vitu vidogo kila wakati, tayari huko Korintho ni "tetemeko la ardhi" ambalo haliharibu, bali huamsha ulimwengu. Neno la Msalaba, ambalo Paulo anashuhudia, huamsha dhamiri na kuamsha utu wa kila mtu.

Katekesi ya Jubilei, Papa Leo XIV Novemba 2025
Katekesi ya Jubilie Novemba 8
Katekesi ya Jubilie Novemba 8   (@Vatican Media)

Kwa njia hiyo Papa aliendelea kusema kuwa, "kutumaini ni kushuhudia: kushuhudia kwamba kila kitu kimebadilika tayari, kwamba hakuna kilichokuwa kama ilivyokuwa hapo awali. Hii ndiyo sababu Papa alipenda kuzungumza kuhusu shahidi wa matumaini ya Kikristo barani Afrika. Jina lake ni Isidori Bakanja, na tangu 1994 amehesabiwa miongoni mwa Wenyeheri, mlinzi wa Walei nchini Congo. Alizaliwa mwaka 1885, wakati nchi yake ilikuwa koloni la Ubelgiji, hakuhudhuria shule, kwa sababu hakukuwa na yeyote katika kijiji chake, lakini akawa mwanafunzi wa utengenezaji wa matofali. Papa aliendelea kuelezea kuwa "Bakanja kuwa alifanya urafiki na wamisionari Wakatoliki, watawa wa Kitrappist: walizungumza naye kuhusu Yesu, naye akakubali kufuata mafundisho ya Kikristo na kupokea Ubatizo, akiwa na umri wa miaka ishirini hivi. Kuanzia wakati huo, ushuhuda wake ukazidi kung'aa.

Katekesi ya Jubilei Novemba 8
Katekesi ya Jubilei Novemba 8   (@Vatican Media)

Kutumaini ni kutoa ushuhuda: tunapotoa ushuhuda wa maisha mapya, nuru huongezeka hata katikati ya magumu.Isidore, kiukweli, anajikuta akifanya kazi kama mfanyakazi wa shambani kwa bwana wake Mzungu asiye na adabu, ambaye hawezi kuvumilia imani yake na uhalisia wake. Bwana huyo alichukia Ukristo na wale wamisionari waliowatetea wenyeji dhidi ya unyanyasaji wa wakoloni, lakini Isidori alivaa skapulari yake yenye picha ya Bikira Maria shingoni mwake hadi mwisho, akivumilia kila aina ya unyanyasaji na mateso, bila kupoteza tumaini.

Katekesi ya Jubilie Novemba 8
Katekesi ya Jubilie Novemba 8   (@Vatican Media)

Kutumaini ni kutoa ushuhuda! Isidori alikufa, akiwatangazia Mapadre wa Kitrappist kwamba hana kinyongo; badala yake, aliahidi kuwaombea, hata katika maisha ya baada ya kifo, wale waliompelekea  katika hali hiyo. Baba Mtakatifu kwa njia hiyo kwa waamini na mahujaji aliendelea kusema kuwa “ni neno la Msalaba. Ni neno lililo hai, linalovunja minyororo ya uovu. Ni aina mpya ya nguvu, ambayo huwachanganya wenye kiburi na kuwaangusha wenye nguvu kutoka kwenye viti vyao vya enzi. Hivyo, tumaini huibuka. Mara nyingi, Makanisa ya kale ya Ulimwengu wa Kaskazini hupokea ushuhuda huu kutoka kwa Makanisa changa, unaowasukuma kutembea pamoja kuelekea Ufalme wa Mungu, ambao ni Ufalme wa haki na amani. Hasa Afrika, inahitaji uongofu huu, na inafanya hivyo kwa kutupatia mashahidi wengi vijana  wa imani. Kutumaini ni kutoa ushuhuda kwamba dunia inaweza kufanana na mbingu kweli. Na huu ndio ujumbe wa Jubilei.” Papa Leo alihitimisha.

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa ungependa kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu kwa kubofya hapa: cliccando qui


 

08 Novemba 2025, 11:02