Papa Leo XIV asali katika Kaburi la Hayati Papa Francisko
Na Salvatore Cernuzio - Vatican.
Kabla ya kuelekea Castel Gandolfo kwa siku yake ya kawaida ya kupumzika kila Juma, Baba Mtakatifu Leo XIV aliingia karibu saa 2:05 za Usiku, masaa ya Ulaya katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu ili kusali mbele ya kaburi la Papa Francisko.
Kwenye bamba la marumaru ambapo huwekwa waridi jeupe ambalo wanaweka kila mara katika kumbukumbu ya Mtakatifu Thérèse wa Lisieux, la uwepo wa kiroho wa kudumu katika maisha ya Papa wa Argentina ma hivyo Papa Leo XIV naye aliweka shada la waridi jeupe. Ilikuwa ishara ya heshima kwa mtangulizi wake, aliyezikwa kati ya Kikanisa cha Sforza na Kikanisa cha Pauline. Kikanisa cha mwisho ni nyumbani kwa Picha ya Salus Populi Romani, (yaani Afya ya Watu wa Roma) ambayo mara nyingi ilitembelewa na Papa Francis kabla na baada ya kila safari ya kimataifa au kulazwa hospitalini.
Kulingana na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Papa Leo XIV, pia alisimama kwa sala mbele ya Picha ya Maria kabla ya kuondoka kwenye Kanisa kuu karibu saa 2:15 usiku na kuendelea na safari yake kwenda Castel Gandolfo.
![]()
Pope Leo katika kaburi la Mtangulizi wake
Misa ya kumwombea kwa Papa Francisko
Mapema siku hiyo Novemba 3, Papa Leo XIV alikuwa ameadhimisha Misa katika Madhabahu ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa kuombea roho za Marehemu kwa ajili ya Papa Francisko na makardinali na maaskofu waliofariki mwaka 2025. Kwa "upendo mkubwa," Baba Mtakatifu aliitoa Misa hiyo kwa ajili ya mtangulizi wake, ambaye, alikumbuka katika mahubiri yake, kwamba "alikufa baada ya kufungua Mlango Mtakatifu na kutoa Baraka ya Pasaka kwa Roma na Ulimwengu wote. Shukrani kwa Jubilei, adhimisho hili kwangu kwa mara ya kwanza, linachukua maana maalum: lina ladha ya tumaini la Kikristo."
![]()
Papa Leo akisali mbele ya Picha Salus Populi Romani
Tumaini hili, Papa Leo XIV aliongeza baadaye katika tafakari yake, lilikuwa moja ambalo Papa Francisko na maaskofu wengine waliokufa katika miezi ya hivi karibuni "waliishi, walishuhudia, na kufundisha."
Ziara za awali kwenye kaburi katika Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu
Mnamo tarehe 10 Mei, siku mbili tu baada ya kuchaguliwa kwake katika Kiti cha Mtume Petro, Papa Leo alitembelea kaburi la Papa wa Argentina, ambalo hutembelewa kila siku na waamini na mahujaji wengi. Alasiri hiyo, Papa aliyechaguliwa hivi karibuni aliweka maua kwenye kaburi na kusimama kwa muda mfupi katika maombi. Alifanya vivyo hivyo tena tarehe 22 Juni, kufuatia maandamano ya Sherehe ya Mwili na Damu ya Kristo, kutoka Mtakatifu Yohane Lateran hadi Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku kwa kubonyeza hapa: Just click here
