Papa Leo XIV aanzisha Utume wa Bahari,ambao unakuwa chombo cha kisheria
Vatican News
Kwa maandishi ya mkono wake (chirograph) yaliyochapishwa Alhamisi, tarehe 13 Novemba 2025, Papa Leo XIV ameanzisha Utume wa Bahari kama chombo kikuu na kinachoratibu Utume wa Bahari. Wakati huo huo, Papa aliidhinisha Sheria zake.
Utunzaji wa Kanisa kwa "Watu wa Bahari"
Kanisa limesindikizana na watu wa baharini kwa muda mrefu, wanaoeleweka kama mabaharia, wavuvi, na familia zao, pamoja na watu wengine ambao maisha yao yanahusiana na uzambazaji na uvuvi baharini, mito, na maziwa. Katika maandishi ya mkono wake (Chirograph) yanataja "uingiliaji kati wa kichungaji na kisheria wa Kiti Kitakatifu, ambao umetoa mahitaji ya kiroho ya waamini ambao, kwa sababu za uhamaji wa kibinadamu, hawawezi kufurahia utunzaji wa kawaida wa kichungaji," kuanzia na Papa Pio X 1914 na motu proprio ya Iam pridem. Hizi zote ni ishara kwamba Kanisa linajali mahitaji ya kipekee ya kiroho ya wale wanaoishi na kufanya kazi katika mazingira ya baharini.
Katika suala hilo, hati ya Papa inakumbusha Hati ya Kitume ya Papa ya Apostolatus Maris kuhusu Utunzaji wa Kiroho wa Wahamiaji na Watu Wanaohama, ya mnamo tarehe 24 Septemba 1977, ambayo ilirekebisha kanuni na vitivo kwa kuzingatia Mtaguso wa Pili wa Vatican. Kisha katika motu proprio ya Stella Maris wa Mtakatifu Yohane Paulo II, ya kunako tarehe 31 Januari 1997, ambayo ilisasisha kanuni zilizotolewa hapo awali. Hatimaye, kifungu cha Papa Francisko kwamba mwelekeo wa Utume wa Bahari ukabidhiwe kwa Baraza la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu, ambalo wakati huo lilichukua jukumu la utunzaji wa kichungaji wa wahamiaji na watu wanahama hama. Kwa hivyo, Maandishi ya yake Papa (chirograph) yanasema, kuanzishwa kwa chombo hiki kikuu na kinachoratibu kunatokana na "hamu kubwa kwamba huduma ya kiroho ya Kanisa katika uwanja wa huduma ya kichungaji ya bahari iendelee kwa shauku na ukarimu."
Mashauriano kuanzia mwaka 2022
Uundaji huu ni matokeo ya mchakato mrefu wa mashauriano ulioanza Oktoba 2022, kwa ushiriki wa wakurugenzi wa kitaifa na maaskofu wakikuza Utume wa Bahari katika mabara mbalimbali, na kuendelea mwaka 2025 kwa mashauriano yaliyolenga zaidi kuhusu malengo na muundo wa Utume wa Bahari. Mashauriano hayo yalifanywa na kuratibiwa na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu, ambalo, kwa mujibu wa kifungu cha 166 § 1 cha Katiba ya Kitume Praedicate Evangelium, linatumia mwelekeo wa Utume wote wa Bahari na kusimamia chombo chake kikuu.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here
