Tafuta

2025.11.05 Akili Unde na Tiba. 2025.11.05 Akili Unde na Tiba. 

Papa:Kutambua Uwezo Mbaya wa Teknolojia,Utu wa Binadamu Kipaumbele

Katika ujumbe kwa washiriki katika Kongamano la Kimataifa lililoandaliwa na Chuo cha Kipapa cha Maisha,kwa mada:"Akili unde na Tiba Changamoto ya Utu wa Binadamu,"Papa Leo XIV anaonya kuhusu hatari za maendeleo ya kiteknolojia ambayo"yanaathiri sana njia yetu ya kufikiri na kubadilisha uelewa wetu wa hali na jinsi tunavyojiona sisi wenyewe na wengine."Katika"kuwajali watu,mahusiano ya kibinadamu hayawezi kubadilishwa."

Vatican News.

Ikiwa maendeleo ya kiteknolojia yameleta, na yanaendelea kuleta, "faida kubwa kwa ubinadamu, hasa katika nyanja za dawa na afya, ili maendeleo ya kweli yatokee, ni muhimu kwamba utu wa binadamu na manufaa ya wote yabaki kuwa vipaumbele kamili, kwa watu binafsi na kwa vyombo vya umma. Ndivyo ulivyo mtazamo wa Baba Mtakatifu Leo XIV katika ujumbe wake kwa washiriki katika Kongamano la Kimataifa lililoandaliwa na Chuo cha Kipapa cha Maisha wenye mada: "Akili Unde na Tiba: Changamoto ya Utu wa Binadamu," linalofanyika kuanzia Novemba 10 hadi 12 jijini Roma ambapo ujumbe huo ulisomwa Jumatatu tarehe 10 Novemba na Rais wa Chuo cha Kipapa cha Maisha, Monsignor Renzo Pegoraro. Katika maandishi hayo, Papa anaangazia "uwezo mbaya wa teknolojia" na "utafiti wa kimatibabu unapowekwa katika huduma ya itikadi zinazopingana na binadamu," akituhimiza kuzingatia matukio ya zamani kama onyo. "Zana tulizonazo leo zina nguvu zaidi na zinaweza kuleta athari mbaya zaidi kwa maisha ya watu binafsi na watu," anaandika, hata hivyo, akikubali matokeo chanya ya kuzitumia "katika huduma ya mwanadamu."

Hatari ya Kupoteza Mtazamo wa Watu

Tunahitaji kutafakari kuhusu mapinduzi ya kidijitali yanayoongoza kwa kile ambacho Papa Francisko alikiita 'mabadiliko ya enzi kuu,” alisisitiza Papa Leo XIV  ambaye anatambua kwamba "maendeleo mapya ya kiteknolojia yanayofanana katika baadhi ya mambo na Mapinduzi ya Viwanda" yameenea zaidi. "Yanaathiri sana njia yetu ya kufikiri, yanabadilisha uelewa wetu wa hali na jinsi tunavyojiona sisi wenyewe na wengine. Kwa kuongezakwamba kwamba “leo tunaingiliana na mashine kana kwamba ni wazungumzaji, karibu kuwa mwendelezo wake. Lakini hii ina hatari ya kupoteza mtazamo wa nyuso za watu na kusahau jinsi ya kutambua na kuthamini yote ambayo ni ya kibinadamu kweli."

Walinzi na Watumishi wa Maisha ya Binadamu

Kwa Papa Leo XIV  kujitolea kwa wale wanaoshiriki katika Kongamano la Kimataifa la Chuo cha Kipapa cha Maisha "katika kuchunguza uwezo wa Akili Unde  katika tiba" ni "kwa umuhimu mkubwa." Kwa sababu udhaifu wa hali ya mwanadamu mara nyingi hudhihirika katika uwanja wa tiba, na ambapo hatupaswi kusahau heshima ya kila mtu, ambaye amekusudiwa, ameumbwa, na kupendwa na Mungu." Kwa sababu hiyo , Dokezo kuhusu Uhusiano kati ya Akili Unde na Akili ya Binadamu( "Antiqua et Nova,)" ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu  iliyoidhinishwa na Papa inasisitiza kwamba "wafanyakazi wa afya wana wito na jukumu la kuwa walinzi na watumishi wa maisha ya binadamu." Na, kulingana na Papa Leo XIV , "hiyo hiyo inaweza kusemwa kuhusu wale wanaohusika na matumizi ya Akili Unde katika uwanja huo."

AI inaboresha mahusiano ya kibinadamu

Katika "kuwajali watu," "mahusiano ya kibinadamu" hayawezi kubadilishwa, Papa alisisitiza, akiona "taaluma ya kimatibabu" ni muhimu sio tu kwa ujuzi maalum unaohitajika, lakini pia kwa uwezo wa kuwasiliana na kuwa karibu na wengine." Kwa hivyo, "vifaa vya kiteknolojia havipaswi kamwe kupunguza uhusiano wa kibinafsi kati ya wagonjwa na wataalamu wa afya." Badala yake, Akili Undea (AI) lazima iboreshe kweli "mahusiano ya kibinafsi na huduma inayotolewa," ili iwe "katika huduma ya utu wa binadamu na utoaji mzuri wa huduma ya afya." Hatimaye, ikikabiliwa na "maslahi makubwa ya kiuchumi ambayo mara nyingi yamo hatarini katika nyanja za dawa na teknolojia" na "mapambano" ya "udhibiti" wake, Papa Leo XIV alitoa wito wa "kukuza ushirikiano mpana," ikiwa ni pamoja na katika ngazi ya kimataifa, miongoni mwa wale "wanaofanya kazi katika sekta ya afya na katika siasa."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here

10 Novemba 2025, 16:50