Papa Leo XIV akutana na Rais wa Afrika Kusini
Jumamosi tarehe 8 Novemba 2025,Papa Leo alikutana na Rais wa Afrika Kusini.Kiini cha mazungumzo ni jukumu la Kanisa nchini kukuza mazungumzo na upatanisho.
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari mjini Vatican imetaarifa kuwa, “Asubuhi ya leo, tarehe 8 Novemba 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV alimpokea Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mheshimiwa Cyril Ramaphosa, katika Ikulu ya Vatican.”
“Wakati wa mazungumzo yao ya kirafiki, taarifa inaeleza “shukrani za pande zote zilitolewa kwa mchango muhimu ambao Kanisa Katoliki hutoa kwa Afrika Kusini, hasa katika maeneo ya elimu na huduma za afya, na kujitolea kwake kuendelea kukuza mazungumzo na upatanisho ndani ya jamii.”
08 Novemba 2025, 14:38
