Papa akutana na mwigizaji Robert De Niro: "Ni furaha kukutana nawe."
Na Salvatore Cernuzio – Vatican.
Vicheko, kwanza kabisa. Vicheko vinachotokana na kuonana uso kwa uso ambao umeonwa na mamia yam amia ya mara kwa mara kwenye skrini na kwenye majarida, na sasa unakutana naye ana kwa ana. Kisha salamu, huku Papa Leo akisema kwanza: "Habari za asubuhi! Ni furaha kukutana nawe!" "Mimi pia,” akijibu. Hili ni tukio la Robert De Niro aliyekutana na Papa Leo XIV mjini Vatican. Mkutano mfupi ulifanyika asubuhi ya Ijumaa tarehe 7 Novemba 2025 katika Ukumbi wa Tronetto wa Jumba la Kitume la Vatican, huku kukiwa na ratiba yenye shughuli nyingi za Papa.
Mkutano mjini Vatican
Muigizaji maarufu aliyeshinda tuzo ya Oscar mara mbili, mwenye umri wa miaka 82, Mmarekani mwenye asili ya Kiitaliano (hasa, kutoka Molise), na ambaye amekuwa akijitangaza kwa fahari kila wakati, alitaka kuhitimisha ziara yake ya masaa 48 ya Roma kwa kushikana mikono na mzalendo mwenzake, Papa Leo.
Papa ambaye, kama marafiki wengi wa muda mrefu huko Chicago wanavyosimulia, alipenda kwenda kwenye sinema. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa: katika Ukumbi wa Tronetto, gumzo kwa Kiingereza, picha na wenzake watano, watoto wake wawili, Drena na Julian Henry, na washirika ambao De Niro hivi karibuni alifungua hoteli na mgahawa huko Roma na, hatimaye, zawadi ya rozari kwa kila mmoja wa waliokuwepo.
Heshima jijini Roma
Kwa upande wa De Niro, kuzamishwa katika uzuri wa kisanii wa Jumba la Kitume la Vatican, baada ya tarehe 6 Novemba, alipokuwa akitazama kutokea kwenye balcony ya Meya wa Jiji Bwana Roberto Gualtieri kwenye Kilima cha ‘Capitoline,’ yaani Jumba la Meya wa jiji la Roma alivutiwa na uzuri wa Majukwaa ya Kifalme.
"Roma ni zaidi ya jiji, ni kazi hai ya sanaa," nyota huyo alimwambia meya wa mji aliyempatia, heshima ya juu zaidi ya Roma, ishara ya jiji kuu Roma: ‘Mbwa Mwitu.’
Nyota huyo wa filamu mashuhuri, ambaye hata hivyo alisomea kujifunza lafudhi ya Sicilia, aliikubali kwa hisia: "Kuheshimiwa hapa, mahali ambapo pametoa mengi kwa ulimwengu wa utamaduni, sinema, na uzuri, kunagusa sana..." alisema mwenyewe. Zaidi ya hayo, mwigizaji huyo aliongeza maelezo ya wasifu: "Familia yangu ina mizizi nchini Italia, kwa hivyo utambuzi huu una maana kwangu binafsi."
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida letu: cliccando qui
