Papa Leo XIV:Msalaba ulipandwa kama mbegu,ili kufufuka tena na kuzaa matunda mengi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Katekesi yake Papa Leo XIV tarehe 19 Novemba 2025 ikiwa ni mwendelezo wa Jubilei ya Matumiani, Yesu Kristo Tumaini letu, kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, alifafanua juu ya matumani ya kikristo katika kujibu changamoto za Ulimwengu ambazo ubinadamu unakabiliwa nazo katika ufafanuzi wa Injili kuhusu Ufufuko wa Yesu Kristo na hasa siku ya kutafutwa na Maria katika Kaburi kwenye bustani.
Papa alianza kusema: "Katika Mwaka huu wa Jubilei uliotengwa kwa ajili ya tumaini, tunatafakari uhusiano kati ya Ufufuko wa Kristo na changamoto za ulimwengu wa leo, ambazo ni changamoto zetu. Wakati mwingine Yesu, Aliye Hai, anataka kutuuliza pia: "Mnalia nini? Mnamtafuta nani?" Changamoto, kiukweli, haziwezi kukabiliwa peke yake, na machozi ni zawadi ya uzima yanaposafisha macho yetu na kufungua macho yetu.”
Papa alisisitiza kuwa, “Mwinjili Yohane anatuelekeza kwenye maelezo ambayo hayapatikani katika Injili zingine: “akilia karibu na kaburi tupu, Maria Magdalena hakumtambua Yesu aliyefufuka mara moja, lakini alidhani alikuwa mtunza bustani.” Hakika, tayari katika simulizi la mazishi ya Yesu, wakati wa machweo ya jua, iku ya Ijumaa Kuu, maandishi yalikuwa sahihi sana: "Na mahali pale aliposulubiwa palikuwa na bustani, na ndani ya bustani palikuwa na kaburi jipya, ambalo hakukuwa na mtu aliyelazwa bado. Kwa sababu ya siku ya Maandalizi ya Kiyahudi, na kwa sababu kaburi lilikuwa karibu, walimlaza Yesu” (Yh 19:40-41).”
Papa Leo aliendelea, “hivyo, katika amani ya Jumamosi (Sabato) na uzuri wa bustani, mapambano makubwa kati ya giza na nuru yaliyoachiliwa na usaliti, kukamatwa, kuachwa, kulaaniwa, kudhalilishwa, na kuuawa kwa Mwana, ambaye “akiwa amewapenda walio wake duniani, aliwapenda hadi mwisho”(Yh 13:1). Kulima na kutunza bustani ni kazi ya awali (taz. Mwa 2:15) ambayo Yesu alikamilisha.”
Neno lake la mwisho msalabani, “Imekwisha” (Yh 19:30), Papa aliongeza kusema, linatualika kila mmoja wetu kugundua upya kazi ile ile, kazi yake mwenyewe. Kwa sababu hiyo “akainama kichwa chake, akatoa roho yake” (Yh 19, 30). Papa Leo XIV aliendelea kusema kuwa “basi, Maria Magdalena, hakukosea kabisa kwa kuamini kwamba alikuwa akikutana na mtunza bustani! Kwa kweli, alikuwa na kusikia jina lake tena na kuelewa kazi yake kutoka kwa Mtu mpya, yule ambaye katika andiko lingine la Yohana anasema: "Tazama, nafanya vitu vyote kuwa vipya" (Uf 21:5).
Papa Francisko, katika Waraka wake wa Laudato Si', alituonesha hitaji kubwa la mtazamo wa kutafakari: isipokuwa tujali bustani, tunakuwa waharibifu wake. Kwa hivyo, tumaini la Kikristo hujibu changamoto zinazowakabili wanadamu wote leo hii kwa kusimama katika bustani ambapo Msalaba ulipandwa kama mbegu, ili kufufuka tena na kuzaa matunda mengi. Mbinguni haipotei, bali hugunduliwa tena. Kwa hivyo, kifo na ufufuko wa Yesu ndio msingi wa kiroho cha ikolojia kamilifu, ambayo nje yake maneno ya imani hubaki bila mshiko wa ukweli na maneno ya sayansi hubaki mbali na moyo.
"Utamaduni wa ikolojia hauwezi kupunguzwa hadi mfululizo wa majibu ya haraka na ya sehemu kwa matatizo yanayoibuka ya uharibifu wa mazingira, kupungua kwa maliasili, na uchafuzi wa mazingira. Inahitaji mtazamo tofauti, njia ya kufikiri, sera, mpango wa elimu, mtindo wa maisha, na kiroho ambacho kinaweza kuunda upinzani" (Laudato Si', 111).
Kwa sababu hiyo Papa alieleza kuwa, tunazungumzia uongofu wa kiikolojia, ambao Wakristo hawawezi kuutenga na mabadiliko ya mwelekeo ambayo kumfuata Yesu kunahitaji kutoka kwao. Kugeuka kwa Mariamu asubuhi hiyo ya Pasaka ni ishara ya hili: ni kwa uongofu baada ya uongofu tu tunapita kutoka bonde hili la machozi hadi Yerusalemu mpya. Mpito huu, unaoanzia moyoni na ni wa kiroho, hubadilisha historia, hutuweka hadharani, na huamsha mshikamano ambao kuanzia sasa unalinda watu na viumbe kutokana na tamaa ya mbwa mwitu, kwa jina na kwa nguvu ya Mwanakondoo Mchungaji.
Kwa hivyo, wana na binti wa Kanisa wanaweza leo kukutana na mamilioni ya vijana na wanaume na wanawake wengine wenye mapenzi mema ambao wamesikia kilio cha maskini na cha dunia na kuruhusu mioyo yao kuguswa nacho. Wengi pia wanatamani, kupitia uhusiano wa moja kwa moja na uumbaji, maelewano mapya ambayo yatawaongoza kupita majeraha mengi.
Kwa upande mwingine, "mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, anga linatangaza kazi ya mikono yake. Mchana kwa mchana linazungumzia, na usiku kwa usiku linatangaza habari zake." Bila kusema, bila maneno, bila sauti yao kusikika, ujumbe wao huenea duniani kote, na ujumbe wao hadi miisho ya dunia" (Zab 18:1-4). Kwa kuhitimisha Papa alisema kuwa “Roho atupe uwezo wa kusikia sauti ya wasio na sauti. Kisha tutaona kile ambacho macho yetu hayawezi kuona bado: bustani hiyo, au Paradiso, ambayo tunaikaribia tu kwa kila mmoja kukubali na kukamilisha kazi yake mwenyewe.”
