Tafuta

 2024.11.13 Matrimonio

Mafundisho ya Kanisa:Ndoa ya mke mmoja si kikomo,kuoa au kuolewa ni ahadi ya milele!

Chapisho la Mafundisho Tanzu ya Kanisa:'Una caro.'Katika Sifa ya Ndoa ya Mke Mmoja,inachunguza thamani ya ndoa kama muungano wa kipekee na mali ya pande zote mbili,muungano unaojumuisha yote unaoheshimu utu wa mwingine kupitia zawadi kamili ya nafsi.Umuhimu wa upendo wa ndoa na kuwajali maskini.Inalaani vurugu,kimwili na kisaikolojia:"Ndoa si kumiliki."Katika enzi ya ubinafsi na matumizi ya kila siku,kuwaelimisha vijana kuhusu upendo kama jukumu na tumaini kwa wengine.

Na Isabella Piro – Vatican.

"Umoja Usiogawanyika": hivi ndivyo Dokezo la Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa  (DDF) linavyofafanua ndoa, yaani, kama "muungano wa kipekee na mali ya pande zote mbili." Sio kwa bahati mbaya kwamba hati hiyo, iliyoidhinishwa na Papa Leo XIV mnamo tarehe 21  Novemba 2025, katika ukumbusho wa kiliturujia Siku Kuu ya Kuwakilishiwa kwa Bikira Maria Hekaluni na kuwasilishwa kwa waandishi wa habari  tarehe 25  Novemba 2025, unaitwa "Una caro (Mwili Mmoja). Kwa Sifa ya Ndoa ya Mume Mmoja na Mmke mmoja." Hati hiyo inaelezea kwamba ni ya wawili tu wanaweza kujitoa kikamilifu kwa mwingine; vinginevyo, itakuwa ni zawadi ya nafsi ambayo haiheshimu hadhi ya mwenzi.

Motisha ulio nyuma ya hati hii

Asili ya hati hii ni tatu: kwanza, kama Kardinali Víctor Manuel Fernández Mwenyekiti wa Baraza hilo alivyondika katika utangulizi, "kuna mwelekeo katika muktadha wa sasa wa maendeleo ya kiteknolojia duniani," ambao unamfanya mwanadamu ajifikirie kama "kiumbe asiye na mipaka" na kwa hivyo mbali na thamani ya upendo wa kipekee uliotengwa kwa mtu mmoja. Pia inataja majadiliano na Maaskofu wa Afrika kuhusu mada ya ndoa ya wake wengi, ikibainisha kwamba "tafiti za kina kuhusu tamaduni za Kiafrika" zinakanusha "maoni ya pamoja" kuhusu asili ya kipekee ya ndoa ya mke mmoja. Hatimaye, hati hii inabainisha ukuaji wa "wake wengi," au aina za umma za miungano isiyo ya mke mmoja, za nchi za Magharibi.

Umoja wa Ndoa na Muungano kati ya Kristo na Kanisa

Katika muktadha huo, hati ya DDF inatafuta kusisitiza uzuri wa umoja wa ndoa ambao, "kwa msaada wa neema," pia unawakilisha "muungano kati ya Kristo na bibi arusi wake mpendwa, Kanisa." Maana iliyokusudiwa hasa kwa ajili ya maaskofu, Dokezo kwa mujibu wa Kardinali Fernández Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa  anasisitiza pia kuwa inalenga kuwasaidia vijana, wachumba walioolewa kuelewa "utajiri" wa ndoa ya Kikristo, hivyo kuhimiza "tafakari ya amani na utafiti wa muda mrefu" juu ya mada hiyo.

Umoja ulioanzishwa kwa ridhaa ya bure

Hati hii imegawanywa katika sura saba, pamoja na Hitimisho, maandishi yanathibitisha kwamba ndoa ya mke mmoja si kizuizi, bali uwezekano wa upendo unaofungua umilele. Vipengele viwili vinaonekana kuwa vya kuamua: umoja wa pande zote mbili na upendo wa ndoa. Ya kwanza, "iliyoanzishwa kwa ridhaa ya bure" ya wanandoa wote wawili, inaonesha ushirika wa Utatu na inakuwa "motisha wenye nguvu kwa utulivu wa muungano." Inahusu "umoja wa moyo, ambapo Mungu pekee ndiye anayeona" na ambapo Yeye pekee ndiye anayeweza kuingia, "bila kuvuruga uhuru na utambulisho wa mtu."

Usichafue uhuru wa wengine

Inaeleweka kwa njia hii, "umoja wa kumilikiwa kwa haki kwa upendo wa pekee wa pande zote unamaanisha utunzaji mpole, hofu takatifu ya kuchafua uhuru wa mwingine, ambaye ana hadhi sawa na kwa hivyo haki sawa." Kwa sababu wale wanaopenda wanajua kwamba "mwingine hawezi kuwa njia ya kutatua kutoridhika kwake" na wanajua kwamba utupu wa mtu mwenyewe haupaswi kujazwa kamwe "kupitia utawala wa mwingine." Katika suala hili, Dokezo linalaani "aina nyingi za tamaa mbaya zinazosababisha maonesho mbalimbali ya vurugu dhahiri au hafifu, ukandamizaji, shinikizo la kisaikolojia, udhibiti, na hatimaye kukosa hewa." Huu ni "ukosefu wa heshima na heshima kwa hadhi ya mwingine."

Ndoa si umiliki

Kinyume chake, neno "sisi wawili" lenye afya linamaanisha "uwiano wa uhuru wawili ambao hauvunjwi kamwe, lakini huchaguana, kila wakati ukiacha kikomo ambacho hakiwezi kuzidi." Hili hutokea wakati "mtu hajipotezi katika uhusiano, haungani na mpendwa," akiheshimu kila upendo wenye afya "ambao haukusudii kumnyonya mwingine." Katika suala hili, Dokezo linasisitiza kwamba wanandoa wataweza "kuelewa na kukubali" wakati wa kutafakari au nafasi fulani ya upweke au uhuru unaoombwa na mmoja wa wanandoa, kwa kuwa "ndoa si umiliki," si "hitaji la utulivu kamili," wala ukombozi kamili kutoka katika upweke (kiukweli, Mungu pekee ndiye anayeweza kujaza utupu ambao mwanadamu anahisi), bali kuaminiana na uwezo wa kukabiliana na changamoto mpya. Wakati huo huo, wanandoa wanahimizwa kutokataana, kwa sababu "wakati umbali unakuwa wa mara kwa mara, 'sisi wawili' huwekwa wazi kwa kupatwa kwake kunakowezekana."

Sala, Njia ya Thamani ya Kukua katika Mapendo

Umoja wa pamoja pia unaonyeshwa katika usaidizi wa pande zote kati ya wanandoa katika kukomaa kama watu binafsi: katika hili, sala ni "njia ya thamani" ambayo wanandoa wanaweza kujitakasa na kukua katika upendo. Kwa njia hiyo, upendo wa ndoa unatimizwa, "nguvu ya kuunganisha," "zawadi ya kimungu" inayoombwa katika sala na kulishwa katika maisha ya sakramenti. Katika ndoa, inakuwa "urafiki mkubwa zaidi" kati ya mioyo miwili ya karibu, "ya jirani" inayopendana na kuhisi "nyumbani" ndani ya kila mmoja.

Ujinsia na Uzazi

Shukrani kwa nguvu ya upendo inayobadilisha sura, itawezekana pia kuelewa ujinsia "mwilini na rohoni," yaani, si kama msukumo au njia ya kutoka, bali kama "zawadi ya ajabu kutoka kwa Mungu" inayoongoza katika kujitoa mwenyewe na kwa manufaa ya mwingine, ikikumbatiwa katika ukamilifu wa nafsi yao. Upendo wa ndoa pia unaenea hadi kwenye uzazi, "ingawa hii haimaanishi kwamba hii lazima iwe kusudi dhahiri la kila tendo la ngono." Kinyume chake, ndoa hudumisha sifa yake muhimu hata kama haina watoto. Zaidi ya hayo, uhalali wa kuheshimu vipindi vya asili vya utasa unakumbukwa.

Mitandao ya Kijamii na Haja ya Haraka ya Ufundishaji Mpya

Hata hivyo, "katika muktadha wa ubinafsi wa matumizi ya baada ya kisasa" unaokana kusudi la umoja wa ngono na ndoa, uwezekano wa upendo mwaminifu unawezaje kuhifadhiwa? Waraka huo unasema jibu liko katika elimu: "Ulimwengu wa mitandao ya kijamii, ambapo unyenyekevu hupungua na unyanyasaji wa kiishara na wa kingono huongezeka, unaonesha hitaji la haraka la ufundishaji mpya." Kwa hivyo ni muhimu "kuandaa vizazi kukumbatia uzoefu wa upendo kama fumbo la anthropolojia," kuonesha upendo si kama msukumo tu, bali kama wito wa uwajibikaji na "uwezo wa matumaini katika mtu mzima."

Kuwajali Maskini, "Dawa" ya Kuzaliana kwa Pamoja

Upendo wa muungano wa ndoa pia unaonekana kwa wanandoa ambao hawajifungi katika ubinafsi wao wenyewe, lakini badala yake hujifungulia mipango ya pamoja ili "kufanya jambo zuri kwa jamii na ulimwengu," kwani "mwanadamu hujitimiza kwa kuhusiana na wengine na Mungu." Vinginevyo, ni ubinafsi tu, kujipenda, na uzazi wa ndani ambao lazima upingwe, kwa mfano, kwa kutumia "hisia ya kijamii" ya wanandoa wanaojitolea pamoja katika kutafuta manufaa ya wote. Katika muktadha huu, jambo kuo ni kuwajali maskini, ambao kama Papa Leo XIV alivyosema kwamba ni “jambo la kifamilia” kwa Mkristo, si “tatizo la kijamii” tu.

Upendo wa Ndoa kama Ahadi ya Ukosefu wa Mwisho

Kwa kumalizia, Ujumbe unarudia kwamba "kila ndoa halisi ni umoja unaoundwa na watu wawili, unaohitaji uhusiano wa karibu sana na unaojumuisha yote kiasi kwamba hauwezi kushirikiwa na wengine." Kwa hivyo, kati ya sifa mbili muhimu za kifungo cha ndoa, umoja na kutovunjika, ni ule wa kwanza unaoanzisha wa mwisho. Ni kwa njia hiyo tu ndipo upendo wa ndoa utakuwa ukweli unaobadilika, unaoitwa kwa ukuaji na maendeleo endelevu baada ya muda, katika "ahadi ya ukosefu wa mwisho."

Kutoka Kitabu cha Mwanzo hadi Majisterio ya Mapapa

Ikumbukwe kwamba Ujumbe pia unatoa muhtasari mpana wa mada ya ndoa ya mke mmoja: kutoka Mwanzo, kupitia Mababa wa Kanisa na uingiliaji kati mkuu wa kimahakama, na hatimaye kwa wanafalsafa na washairi wa karne ya 20, unachunguza hisia ya kuwa sehemu ya ndoa iliyohisiwa katika "sisi wawili." Kwa sababu mwishowe, kama Mtakatifu Agostino alivyosema,: "Nipe moyo unaopenda, nao utaelewa ninachosema."

Uwasilishaji wa Dokezo la "Una Caro" kuhusu Sakramenti ya Ndoa

Kwa maelezo kamili unaweza Kusikiliza maelezo:Bonyeza hapa kusoma kwa kina hati hii ya "Una Caro"

https://press.vatican.va/content/salastampa/it/bollettino/pubblico/2025/11/24/0898/01599.html

Dokezo UNA CARO
25 Novemba 2025, 11:48